Makamba atangaza wanaotaka kugombea uspika kutoka CCM, je ni sahihi ?

Mpasuajipu

JF-Expert Member
Oct 22, 2010
836
49
Jamani mmemsikia Makamba? eti wanachama wa CCM wanaotaka kugombea ubunge wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania waanze kuchukua Form za kugombea nafasi hiyo. Je ni sahihi wakati hata nusu ya matokeo ya ubunge na urais bado wakiyabanibania. Au sheria inasemaje?
 
aaaahhhh mzee ni mzeee mambo ndio yanaanza ye kamaliza au katumwa na shehe yahya
 
Jamani mmemsikia Makamba? eti wanachama wa CCM wanaotaka kugombea ubunge wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania waanze kuchukua Form za kugombea nafasi hiyo. Je ni sahihi wakati hata nusu ya matokeo ya ubunge na urais bado wakiyabanibania. Au sheria inasemaje?

Mkuu wanatafuta sababu ya kutengeneza fujo.
 
Jamani mmemsikia Makamba? eti wanachama wa CCM wanaotaka kugombea ubunge wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania waanze kuchukua Form za kugombea nafasi hiyo. Je ni sahihi wakati hata nusu ya matokeo ya ubunge na urais bado wakiyabanibania. Au sheria inasemaje?

Acha biasness! Kasema hata vyama pinzani wameruhusiwa kuanza mchakato. Kwani wewe ulitaka asemaje? Slaa akachukue fomu? Makamba hana wajibu wa kutangazia wanachama wa vyama vingine. Zaidi ni dhahiri CCM wameshinda, labda waamue kuwaachia tu!
 
sioni kama kuna tatizo llolote... sas unadhani atakua bize na kitu ganiw akati wanachofanya sasa hakihitaji uchawi?
 
Yote hii ni kutafuta njia ya kuondoa attention ya watu kwenye matokea ambayo bado wameyabania ili waweze kuchakachua.
 
Jamani mmemsikia Makamba? eti wanachama wa CCM wanaotaka kugombea ubunge wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania waanze kuchukua Form za kugombea nafasi hiyo. Je ni sahihi wakati hata nusu ya matokeo ya ubunge na urais bado wakiyabanibania. Au sheria inasemaje?

Ni sawa na hata wewe unaweza kugombea uspika sheria inaruhusu.
 
Jamani mmemsikia Makamba? eti wanachama wa CCM wanaotaka kugombea ubunge wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania waanze kuchukua Form za kugombea nafasi hiyo. Je ni sahihi wakati hata nusu ya matokeo ya ubunge na urais bado wakiyabanibania. Au sheria inasemaje?

Mkuu siyo ubunge ni uspika, na hii habari siyo breaking news, ni habari ya tangu asubuhi, tuwe makini kidogo.
 
Huyu mzee ana behave kama character fulani hivi kama hawa waganga waganga wa kienyeji. Kwangu mimi hana hadhi ya General Secretary wa rulling party. Tabia za watu kama hawa ndio zinanifanya nikatishwe tamaa kabisa na uwezo wao wa kuleta mabadiliko ya muda mrefu (long term strategies/plans). Mtu kama huyu kweli ukimwambia akupe vision ya Tanzania ya 2035 kweli anajua? I dont think he even cares for long term issues. Yeye inaonekana ana deal na mambo yanavyotokea kila anapoamka asubuhi na yuko tayari kufanya kila hila ili apate sifa CCM na aendelee kuwepo madarakani
 
sina hakika kama ni sahihi! Kwani bunge ni chombo huru kinatumiwa na vyama vyote, iweje 4m za kugombea zipatikane ofisini kwake? Yeye ni nani? Si kawaida amechawiwa huyu mzee? Mwisho wako uko waja kujipachika vyeo visivyo vyako. Nyooo huna aibu kikongwe wewe tumekuchoka sio siri... 0
 
jamani mmemsikia makamba? Eti wanachama wa ccm wanaotaka kugombea ubunge wa bunge la jamhuri ya tanzania waanze kuchukua form za kugombea nafasi hiyo. Je ni sahihi wakati hata nusu ya matokeo ya ubunge na urais bado wakiyabanibania. Au sheria inasemaje?

makamba na jk hawamtaki sitta arudi kwenye nafasi yake walitaka hata yeye na mkewe wakose ubunge....makamba ametangaza hili baada ya kuona sitta leo ameshinda uubunge na kutangaza nia ya kugombea au kutetea nafasi yake ya usipika....anafaa lakini wao wantaka wampe edward lowassa ili kumuuandaa kugombea urais....
 
wao kwao ni itifaki tuu ila tayari wameshampitisha KINANA!!!!!!!!!!!!!!!!

Kinana is a good person but sio kila kazi anaweza kufanya ....waulizeni kilichomkimbiza Arusha mjinii???.....alafu kuna genge lao na kina Bashe..na mtandao wa wafanyabiashara wenye common roots ambaoo hukutana bagamoyo kwenye hotel ya mmoja wao..they both share the same problem ...na wana mikakati ya kukamata dola!!
 
mheshimwa kinana ni good person.....mhhhhhhhhhhhhh
 
Jamani mtoa mada alitaka kujua kama kauli ya Makamba ni shahihi.

Jibu ni sahihi kwa sababu zifuatazo.

1. Kila Chama kinatakiwa kifanye utaratibu wake wa kumpata mgombea uspika kupitia chama hicho.
2. Kama ilivyo katika ubunge, wagombea wanaowakilisha vyama tofauti watapigiwa kura. Ila kura hizo zitapigwa na wabunge wateule tu katika kikao chao cha kwanza kabla kula kiapo. Spika mteule atakula kiapo mbele ya wabunge wateule na kisha kuwaapisha wabunge wenzake.
3. Utaratibu wa CCM ni kwamba wanachama wao wataomba. Majina yao yatapigiwa kura na wabunge wateule wa CCM (kama kamati ya chama). Hii ni sawa ya kura ya maoni katika ubunge. Kamati kuu itakaa na itapendekeza jina moja ambalo litawasilishwa kwa ajili ya kupigiwa kura na wabunge wote.
4. Hivyo utaratibu wa sasa ni kwa ajili ya kuanza mchakato wa kura ya maoni ndani ya CCM.

Ikumbukwe kuwa si lazima spika awe mbunge hivyo hamna uhusiano wa matokeo ya ubunge na mchakato wa kuomba uspika.

Naomba kuwasilisha
 
Jamani mmemsikia Makamba? eti wanachama wa CCM wanaotaka kugombea ubunge wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania waanze kuchukua Form za kugombea nafasi hiyo. Je ni sahihi wakati hata nusu ya matokeo ya ubunge na urais bado wakiyabanibania. Au sheria inasemaje?

katiba ibara 84.-(1) Spika atachanguliwa na wabunge akiwa yeye ni mbunge au mwenye sifa za kuwa mbunge.
 
makamba na jk hawamtaki sitta arudi kwenye nafasi yake walitaka hata yeye na mkewe wakose ubunge....makamba ametangaza hili baada ya kuona sitta leo ameshinda uubunge na kutangaza nia ya kugombea au kutetea nafasi yake ya usipika....anafaa lakini wao wantaka wampe edward lowassa ili kumuuandaa kugombea urais....

Mimi nitafurahi zaidi akikaa kule kwenye benchi ili aweze kuongeza nguvu katika kuchangia hoja. Yeye amekaa kule anajua sheria za mle hivyo tunategemea kuongeza nguvu kwa akina Kabwe, Mnyika, Mdee na Mwakyembe.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom