Makamba amtaka Lipumba awataje vigogo wa dawa za kulevya CCM

Serendipity

JF-Expert Member
Jan 24, 2009
486
43
KATIBU Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba amemtaka mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba kuwataja kwa majina vigogo wa CCM wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya nchini.

Juzi, Profesa Lipumba alinukuliwa na vyombo vya habari(si Mwananchi) akisema anazo taarifa nyeti na za kweli kuhusu vigogo wa CCM wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya nchini.

“Hii ni nchi inayofuata sheria, hivyo kama Profesa Lipumba anao ushahidi na majina ya hao vigogo wa CCM wanaojihusisha na dawa za kulevya awataje,” alisema Makamba jana jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu huyo alisema endapo Profesa Lipumba atawaweka hadharani vigogo hao, atakuwa amelisaidia jeshi la polisi kutimiza wajibu wake.

“Ni muhimu Profesa Lipumba akawataja hao vigogo na atoe ushahidi ili polisi wafanye kazi yao,” alisema

Akizungumza juzi katika ufunguzi wa kikao cha Baraza Kuu la Taifa la CUF, Profesa Lipumba alisema anazo taarifa nyeti kutoka ndani ya CCM, kwamba vigogo wengi wanajihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

SOURCE: Mwananchi
 
nimemkumbuka amina chifupa...
RIP Amina Chifupa, lakini nakumbuka hata JK alishasema hadharani kwamba (anawafahamu kwa majina) wauza unga mashuhuri wote wa bongo!
I stand to be corrected....
 
Mimi siamini kama kunalolote litakalo fanyika ata kama majina hayo yatajwa na ushaidi ukawepo. Ni mambo mangapi yalisha semwa juu ya maouvu hapa nchini na ushaidi ukawepo, lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa zaidi ya kuwalindwa waliohusika na maovu hayo.
Mimi nilifikiri angesema kuwa ambao wanatuhumiwa kwa ufisadi wachukuliwe hatua kwani ushaidi upo.
Huyu mzee anatumika vibaya kwa kuwalindwa waalifu.
 
Very good mixer of drums, organs and all other equipments used when composing music. watacheza na mwisho nothing kitafanyika. hata mimi ningekuwa na wateja reliable ningefanya hii biashara kwani nchi haina mwenyewe
 
RIP Amina Chifupa, lakini nakumbuka hata JK alishasema hadharani kwamba (anawafahamu kwa majina) wauza unga mashuhuri wote wa bongo!
I stand to be corrected....

Sawa sawa kabisa, hayo ni kweli unless magazeti yalim-quote vibaya. Lakini kwa nini Babu Makamba anataka Lipumba awataje wakati AC (RIP) alishafanya hiyo kazi na matokeo yake hatukuyaona zaidi ya yeye.............!!!
 
Majina yote wanayo....wauza unga,pembe za ndovu,silaha,madini,ufisadi,hawawezi kutoa maamuzi magumu na mazito...wanalindana haina maana hata ukiwatajia watakwambia huna ushahidi!!!
 
Kama sijakosea Muungwana alisema "Ninayo majina..." sasa Makamba angeanzia na huyo swahiba wake au mnasemaje wakuu?
 
KATIBU Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba amemtaka mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba kuwataja kwa majina vigogo wa CCM wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya nchini.

Juzi, Profesa Lipumba alinukuliwa na vyombo vya habari(si Mwananchi) akisema anazo taarifa nyeti na za kweli kuhusu vigogo wa CCM wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya nchini.

“Hii ni nchi inayofuata sheria, hivyo kama Profesa Lipumba anao ushahidi na majina ya hao vigogo wa CCM wanaojihusisha na dawa za kulevya awataje,” alisema Makamba jana jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu huyo alisema endapo Profesa Lipumba atawaweka hadharani vigogo hao, atakuwa amelisaidia jeshi la polisi kutimiza wajibu wake.

“Ni muhimu Profesa Lipumba akawataja hao vigogo na atoe ushahidi ili polisi wafanye kazi yao,” alisema

Akizungumza juzi katika ufunguzi wa kikao cha Baraza Kuu la Taifa la CUF, Profesa Lipumba alisema anazo taarifa nyeti kutoka ndani ya CCM, kwamba vigogo wengi wanajihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

SOURCE: Mwananchi

Lipumba ni vema akawataja kwa majina bila woga.Asiogipe kwani jamii ipo inamlinda.
 
Mwenyekiti wake alisema majina anayo kwa nini asinge anza na yeye, ayataje kisha atoe ushahidi ili polisi wafanye kazi yao.
 
Hivi waandishi wetu wa habari kwa nini hawajifunzi kuuliza maswali?, na yawe maswali magumu.
 
Bosi wake Makamba alisema anayo-list mbona yeye hamkumwambia awataje?...aanze yeye Prof atafuata.

Huyo Kikwete tunamjua ni msanii, hii ni litmus test kwa Lipumba kama naye ni msanii au la.

Unless anasema alikuwa ana-m-parrot Kikwete bila ya kujua majina specific, which hardly shows leadership.
 
Back
Top Bottom