MAKAMBA akumbana na dhihaka.

Indume Yene

Platinum Member
Mar 17, 2008
2,943
699
Wanafunzi wamuita Makamba fisadi

na Joseph Zablon na Methord Milanz, Mkuranga (TD)

WANAFUNZI wa kidato cha tano na sita katika shule za sekondari za St. Mathew, juzi walimweka katika wakati mgumu Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba baada ya kuuzomea msafara wake na kudai kuwa ni wa ‘mafisadi’.

Makamba ambaye alikuwa katika ziara ya kichama Wilaya ya Mkuranga iliyopo mkoani Pwani, alikumbwa na sakata hilo baada ya kupokewa katika ofisi ya tawi la Kongowe na kwenda kufungua ofisi ya CCM ya Kata ya Kipala Mpakani ambayo imejengwa kwa uhisani wa mkurugenzi wa shule za St. Mathew, Thadeus Mutembei.

Mara baada ya kukagua ofisi hizo, msafara wa Makamba ulielekea katika majengo ya kidato cha tano na sita kwa ajili ya kunywa chai, na ndipo baadhi ya wanafunzi miongoni mwa waliokuwa wakimpungia mkono katibu mkuu huyo katika lango kuu la kuingilia, kupaza sauti na kusema; ‘mafisadi hao’.

Kauli hiyo ilionekana kumkera Makamba ambaye mara baada ya kushuka katika gari lake, aliwaita wanafuzi wa shule hiyo wote waliokuwa eneo hilo na kuwataka wamsikilize, na ndipo alipoanza kunukuu vifungu vya Kuran na Biblia, ambavyo vinaeleza kuwa wao kama viongozi wa nchi ni watumishi wa Mungu.

Alisema kuna wanafunzi getini wamewaita mafisadi, kitendo ambacho alidai kuwa kimemsikitisha mno kwani wao kama viongozi pia ni viongozi wa nchi na ni wazazi wao, hivyo kuwataka wafanye utafiti kama wasomi, walau kujua maana ya neno lenyewe badala ya kulitumia bila kujua maana yake.

Makamba ambaye alitaka apewe kamusi ili awaonyeshe tafsiri sahihi ya neno hilo alisema, kulingana na tafsiri ya neno hilo, fisadi ni mtu mwasherati, anayetembea na wake za watu, guberi, hivyo aliwataka wanafunzi hao kufanya utafiti kabla ili wawe na uhakika wa kile wanachofanya au kusema.

“Msituhukumu kwa makosa ya wengine, kama Makamba ni mzinzi ina maana CCM yote wanazini? Amri ya sita inasema usizini, sasa wewe kama unafanya hivyo ina maana mtu wa kulaumiwa au kuwajibishwa katika hilo ndio awe askofu?” alihoji na kuongeza kuwa kuna watu ambao makosa ya watu wachache wasio waadilifu wanayafanya yawe ya wote kitu ambacho si sahihi.

Katibu mkuu huyo aliutaka uongozi wa shule hiyo kutochukua hatua zozote kwa watoto hao kutokana na ukweli kuwa wanapotoshwa na vyombo vya habari kwani suala hilo ni lake na watoto hao na ameishawasamehe kama ilivyoandikwa katika vitabu vitakatifu.

“Yesu alisema samehe, sabini mara sabini, hivyo hili ni la kwangu na wao wanafunzi, tumemaliza labda mtafute la kwenu,” alisema Makamba huku watoto hao wakishangilia na kuwafanya waangue vicheko, na ndipo mkurugenzi wa shule hiyo, Mutembei alimuomba radhi katibu mkuu huyo na kusema kuwa hiyo ni saikolojia ya watoto kwani hata yeye huwa wanamtania.

Baada ya kuwaasa wanafunzi hao, Makamba aliingia ndani kujumuika na wenzake katika chai kabla ya kuweka jiwe la msingi la jingo la ofisi ya CCM Wilaya ya Mkuranga ambalo litagharimu zaidi ya shilingi milioni 50.

Makamba pia aligawa kadi mpya kwa wanachama wapya zaidi ya 100 waliojiunga na chama hicho wakitokea CUF, CHADEMA na CHAUSTA na alichangisha zaidi ya sh 400,000 kwa ajili ya mradi wa vijana wa chama hicho katika Kata ya Mkuranga na kuwataka wana CCM kutekeleza ilani ya chama hicho kwa viongozi kutoka katika ofisi zao na kwenda mitaani kusikiliza matatizo ya wananchi.

“Sifikirii kuona kiongozi toka asubuhi hadi saa 12:00 jioni yupo ofisini badala ya kwenda kusikiliza kero na matatizo ya wananchi,” alisema na kuongeza kuwa chama hicho kinawakaribisha wanachama na viongozi ambao awali walikosea na kwenda upinzani.

Nilisema na nitazidi kusema, bado muda haujafika ambapo wananchi wataweza kunyanyua chochote kitakochokuwa mbele yao na kutumia kuwatwanga FISADIZ. Sasa angalia hawa ni wanafunzi tu ambao wanalipiwa karo na wazazi wana hasira na FISADIZ. Sasa hao wazazi watakuwa vipi!! Watajaribu kuleta kamusi na kusema wanayotaka lakini ukweli utabaki pale pale FISADI IS FISADI.

Kazi kwako Kamanda wa Polisi Pwani, sijui mtawafungulia hawa vijana kesi kama wale waliomzomea FISADI mwingine MKAPA. Kama jibu litakuwa ndiyo basi muanze kuandaa ujenzi wa magereza nyingi maana mtawafunga watanzania karibia wote wanaochukia ufisadi.
 
Huyu Makamba sio mzima kwa kweli...

Sasa ina maana alikuwa anajaribu kutuambia nini...anajaribu potosha kizazi kichanga kwa kukipa maana za maneno toka nwenye Kamusi?

Hivi CCM hawaoni aibu kuwa na Mtu mwenye "a Secretary of low calibre'" kama Makamba?
 
Afadhali wamempasha kwani ni aibu sana...wamezidi ufisadi mpaka watoto wanawazomea.Hii inabidi waendelee na hata mawaziri wote wazomewe kwani serikali nzima ni mafisadi hakuna mtakatifu humo.
Kama kuna kiongozi yeyote ambaye si fisadi serikalini ajitokeze tummulike.
 
Mzee wa mistari yule akibanwa kwenye hoja hukimbilia kwenye biblia na Quran....Mufilisi kabisa
 
Ile style ya kuwazomea mawaziri kipindi walipokuwa wanazunguka mikoani wakati wakijaribu kuwapoza wananchi baada ya kumtimua Zitto bungeni naamini yaanza kurejea. Kiongozi wa Chama tena ngazi ya juu kuzomewa si taswira nzuri. Hapo ndipo waone kuwa wananchi wamechoka.
 
Makamba kuanza kuhubiri na kutoa maana ya ufisadi haitasaidia kitu. SISIEMU wanatakiwa kutubu kwa wananchi, hata Biblia inasema "Kumbuka ni wapi ulipoanguka ukatubu na urudie upendo wa kwanza". Tatizo ni kwamba SISIEMU haitaki kukubali ukweli kuwa imekosa na inapaswa kutubu. Watafanya hivyo baada ya kuona kuwa hakuna mtu anayewasikiliza.

Kipindi mfumo wa vyama vingi unaingia nchini hawa SISIEMU walianza kuonyesha picha za Idd Amini, Mauaji ya Rwanda na kuwaambia wananchi mkichagua vyama vingi yatatokea mauaji kama ya Rwanda. Lakini wananchi hawaku-pay attention, na mfumo huo ukakubaliwa. Hayo mauaji yako wapi? Wakishaona maji yamefika shingoni ndipo wataanza kutafuta excuses.
 
5 distinct results returned.

fisadi , pl mafisadi { English: corrupt person , pl corrupt people }
noun 5/6an, [ photos: upload ]

fisadi , pl mafisadi { English: destroyer , pl destroyers } [derived: Arabic]
noun 5/6an, [ photos: upload ]
Swahili Example: lilichumwa na kutupwa na fisadi asiyejua uzuri wa ua [Sul]

fisadi , pl mafisadi { English: evil person } [derived: Arabic]
noun 5/6an, [ photos: upload ]

fisadi , pl mafisadi { English: libertine }
noun 5/6an, [ photos: upload ]

fisadi , pl mafisadi { English: seducer , pl seducers }
noun 5/6an, [ photos: upload ]
 
Makamba hana uwezo wa kujibizana hata na hawa vijana kwani huenda kielimu wamemzidi sana kwani wao wapo kidato cha tano na sita ,hivi huyu aliishia kidato cha ngapi?
 
5 distinct results returned.

fisadi , pl mafisadi { English: corrupt person , pl corrupt people }
noun 5/6an, [ photos: upload ]

fisadi , pl mafisadi { English: destroyer , pl destroyers } [derived: Arabic]
noun 5/6an, [ photos: upload ]
Swahili Example: lilichumwa na kutupwa na fisadi asiyejua uzuri wa ua [Sul]

fisadi , pl mafisadi { English: evil person } [derived: Arabic]
noun 5/6an, [ photos: upload ]

fisadi , pl mafisadi { English: libertine }
noun 5/6an, [ photos: upload ]

fisadi , pl mafisadi { English: seducer , pl seducers }
noun 5/6an, [ photos: upload ]


No matter how you define the term, they still fit in. Lakini at least yeye anakataa kuitwa fisadi kwa definition ya ufuska, naona hapa kuna mwanga fulani, definition nyingine amezikubali, hilo naona ni confession nzuri. Ni vyema Makamba akipongezwa.
 
No matter how you define the term, they still fit in. Lakini at least yeye anakataa kuitwa fisadi kwa definition ya ufuska, naona hapa kuna mwanga fulani, definition nyingine amezikubali, hilo naona ni confession nzuri. Ni vyema Makamba akipongezwa.

Kwanza zimekuja maana za kutosha na Kisha Mkuu Katibu kapingana na moja tu ya Uzinifu...

Nadhani hii ni hatua nzuri kwamba wamekubali kwamba ufisadi mwengine wote wanao isipokuwa huo wa Kuzini!!! Daah Makamba akili chache mno!
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom