Makamba akiri wanaccm wanadanganyika kwa nje tu ila mioyoni hawadanganyiki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makamba akiri wanaccm wanadanganyika kwa nje tu ila mioyoni hawadanganyiki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Joss, Oct 18, 2010.

 1. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Alikuwa anazungumza na wanaccm wa Arusha kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi.
  Angalia kwenye nyekundu.....


  BAADA ya kimya cha muda mrefu, katibu mkuu wa CCM, Yusuph Makamba ameibuka na kuwataka viongozi wa dini nchini kuacha kuwachagulia waumini wao wagombea kwenye uchaguzi mkuu ujao.
  Kwa muda mrefu tangu kampeni zianze, Makamba amekuwa kimya, akikataa kuzungumzia masuala ya kampeni za chama chake kwa maelezo kuwa yupo mapumzikoni mkoani Tanga.

  Lakini jana, Makamba alikuwa na mkutano na wanachama wa CCM kwenye Kata ya Kaloleni mjini hapa jana na kuwambia kuwa katika siku za karibuni baadhi ya viongozi wa dini wamekuwa wakiwataka waumini wao kuchagua wagombea wa fulani jambo ambalo katibu huyo wa CCM alidai kuwa si haki.

  "Kuna baadhi ya viongozi wa dini wamekuwa wakitoa maneno yanayoonyesha wanawachagulia waumini wao wagombea... naomba muanze kuwauliza ni wapi katika vitabu vyao vimewaeleza wawalazimishe kuwachagulia viongozi," alisema Makamba.
  Katibu huyo, wa CCM bila kuwataja viongozi hao, huku akinukuu maneno ya vitabu vitakatifu vya Biblia na Quran, alisema kila mtu ana haki ya kumchagua kiongozi bora ambaye anamtaka na sio kuchaguliwa.

  Kumekuwepo na tuhuma hizo za viongozi wa dini kuwashawishi waumini wao kuwachagua wagombea wanaowataka, lakini hadi sasa hakuna kiongozi wa dini aliyekemewa wala kuonywa kwa kosa la kuwatajia waumini wake jina la mgombea anayemtaka.
  Hata hivyo, Makamba alisema viongozi bora ni wawale wanatokana CCM ambayo aliielezea kuwa ni chama chenye rekodi ya kuwasaidia wananchi katika kukabiliana na umasikini, ujenzi wa barabara na kuwawekea huduma muhimu.

  "Waulizeni hao akina (mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Dk Willibrod) Slaa na (mgombea urais kwa tiketi ya CUF, Prof Ibrahim) Lipumba je wamewahi kujenga barabara; je wamewahi hata kuwasaidia; lakini Kikwete leo ni sawa na mtu ambaye ametoka vitani. Ana jambo la kujivunia kwa kuwa katika miaka mitano kuna mengi amefanya," alisema Makamba.
  Katika mkutano huo, Makamba aliwataka wakazi wa Arusha kujiepusha na siasa za udini na kuwataka kuchagua kiongozi bora bila kujali dini yake wala kabila lake.

  "Nina jambo moja muhimu nataka kuwaambia... kuna hili la udini nawaomba muache udini chagueni viongozi bora kama Kikwete na Dk Batilda na madiwani wa CCM kwa kuwa wanawapenda na wataweza kuwasaidia," alisema Makamba.

  Makamba katika mkutano huo, pia aliomba wanachama wa CCM wilayani Arusha kuvunja makundi na kumchagua mbunge aliyepitishwa na chama hicho, Batilda Buriani hata kama mwanzoni hakuwa katika kundi lao.

  Makamba aliwaonya wanaccm kuwa hatawaeleka kama jimbo la Arusha likipotea hivyo ni wajibu wao kushikamana sasa na kuachana na upinzani ili CCM ishinde kiti cha urais, ubunge na nafasi nyingi za udiwani.
  "Najua wapo hapa baadhi yetu wana mashati ya kijani lakini moyoni sio wenzetu, naowaomba kuanzia leo tushirikiane... Batilda apite kwa kuwa ushindi wake ni wetu sote CCM," alisema Makamba.
   
 2. N

  Nanu JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Huyu naye!!! Katika watu ambao wanaiua CCM ni Makamba mmojawapo!!!
   
 3. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Kweli January ana baba. Hata kama sisi wengine baba zetu hawajapata nafasi ya kwenda hata shule, nafikiri wana uwezo wa kujenga hoja makini kuliko huyu. Hao akina Lipumba na Slaa wangejenga barabara na madaraja kwa hela ya vyama vyao au? Waliwahi kushika serikali halafu wakashindwa kufanya hayo anayoyasema Makamba? Mbona yeye anatumia bilioni 50 kwa ajili ya kampeni, kwa nini asitumie hizo kununulia madawa hospitalini? Mbona wamenunua magari zaidi ya 200 ya chama kwanin hizo hela asingezitumia kuwajengea wananchi barabara. Hili jamaa ni zuzu kweli kweli, I am sorry to say so!! but anakera kushinda maelezo.
   
 4. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ataota moto wa chuma cha pua mwaka huu...! Alikuwa usingizini ndio akaibukia Arusha na pumba nyingine! Akumbuke kuwa ndiye yeye anaeneza Uongo na chuki za Ukabila kuwa baadhi ya Vyama ni vya kikabila na kutaja mfano ni CHADEMA, akisema eti ni cha Mtei na Ndesamburo, just because wao waanzilishi na ni Wachagga? Aibu hii! Kumbe watanzania wanaona mbali kuliko yeye, ndio maana wanampuuza kila neno lake. Na ndio yeye anawasema viongozi wa dini kuwa wanawaamuru wananchi wamchague kiongozi yupi, huyu jamaa amwogope Mungu! Hakuna kiongozi aliyemtaja mgombea, labda ktk dini yake wanafanya hivyo, awaseme wao na si upande wa wakristo! Na hata hivyo, kura ni siri, na hakuna kiongozi wa hini atakayeenda ktk sanduku la kura na Askofu, Mchungaji au Shehe amwambie piga kura hii au pale, wasiwasi wake nini? Serikali ilikwepa kuwafundisha wananchi uraia ili walsielewe wanaenda wapi, au wapigeje kura, na sasa Makamba na Serikali wanaogopa ili-khali viongozi wa dini wanafundisha tu uraia, wanawafundisha wananchi namna ya kumpata kiongozi wao bora kwa maisha yao, Kosa lipo wapi? Kuwaelimisha wananchi? Mnataka wabaki tu malimbukeni muwatawale bila mwisho?? Sasa Yametimia! Watanzania wanazo akili kuliko hata viongozi walio madarakani...Kijani watavaa, hela watatumia lakini cha moto kinakuja Oktoba 31...KURA YA MABADILIKO! Mwaka huu hakuna kulala, Kiongozi makini lazima ashike hatamu mwaka huu na hakuna wa kuzuia hata wananchi wakitishiwa nyau, Arusha na mikoa yote wameshaamua, CCM bye bye! ......RIP!
   
Loading...