Makamba aitwa fisadi

Peasant

JF-Expert Member
Sep 27, 2007
3,949
687
Waheshimiwa wana JF, nimevutiwa na hiki kituko cha Makamba kuzomewa na kuitwa fisadi na vijana wa kidato cha tano na sita. Hii ni dalili njema kuonyesha kwamba kuna mwamko wa kweli katika jamii against mafisadi. I just can't wait to hear some more stuff from all over the country against the kingpins of ufisadi.
Hasivyokuwa na soni mzee huyu kaamua kunyumbulisha maana ya neno fisadi kuwa ni "MZINZI"! ili kudivert maana halisi waliyokusudia vijana wale. Kazi ipo, kama huyu ndo katibu mkuu wa chama tawala!Wanafunzi wamuita Makamba fisadi


na Joseph Zablon na Methord Milanz, Mkuranga
WANAFUNZI wa kidato cha tano na sita katika shule za sekondari za St. Mathew, juzi walimweka katika wakati mgumu Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba baada ya kuuzomea msafara wake na kudai kuwa ni wa ‘mafisadi'.

Makamba ambaye alikuwa katika ziara ya kichama Wilaya ya Mkuranga iliyopo mkoani Pwani, alikumbwa na sakata hilo baada ya kupokewa katika ofisi ya tawi la Kongowe na kwenda kufungua ofisi ya CCM ya Kata ya Kipala Mpakani ambayo imejengwa kwa uhisani wa mkurugenzi wa shule za St. Mathew, Thadeus Mutembei.

Mara baada ya kukagua ofisi hizo, msafara wa Makamba ulielekea katika majengo ya kidato cha tano na sita kwa ajili ya kunywa chai, na ndipo baadhi ya wanafunzi miongoni mwa waliokuwa wakimpungia mkono katibu mkuu huyo katika lango kuu la kuingilia, kupaza sauti na kusema; ‘mafisadi hao'.

Kauli hiyo ilionekana kumkera Makamba ambaye mara baada ya kushuka katika gari lake, aliwaita wanafuzi wa shule hiyo wote waliokuwa eneo hilo na kuwataka wamsikilize, na ndipo alipoanza kunukuu vifungu vya Kuran na Biblia, ambavyo vinaeleza kuwa wao kama viongozi wa nchi ni watumishi wa Mungu.

Alisema kuna wanafunzi getini wamewaita mafisadi, kitendo ambacho alidai kuwa kimemsikitisha mno kwani wao kama viongozi pia ni vi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom