Makamba aigawa CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makamba aigawa CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Nov 7, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Nov 7, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,854
  Likes Received: 83,338
  Trophy Points: 280
  Makamba aigawa CCM

  na Mwandishi Wetu
  Tanzania Daima~Sauti ya Watu

  MGOGORO unaotishia uhai wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) umeshika kasi baada ya baadhi ya wabunge wa chama hicho, kuzidi kumshinikiza Katibu Mkuu wao, Yussuf Makamba, ajiuzulu kwa madai ya kukidhoofisha chama huku kundi jingine likifanya juu chini kujaribu kumnusuru.

  Wakati kundi moja la wabunge likitoa kibano hicho kwa Makamba, kundi la viongozi wa CCM, Ofisi Ndogo Dar es Salaam na Dodoma, limejitokeza kumtetea kwa madai kuwa wabunge hawana uwezo wa kumtaka Makamba ‘aachie ngazi’. Kwa kufanya hivyo watakuwa wamekiuka kanuni na taratibu za chama.

  Vyanzo vyetu vya habari kutoka Dodoma ambako juzi kikao cha wabunge wa CCM kilifanyika, zinaeleza kuwa wabunge hao wamemtaka Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, kutengua uteuzi wa Makamba kwa sababu kadhaa zikiwamo kudaiwa kuwatumia watu wasiojulikana kufanya kampeni katika Jimbo la Tarime na kusababisha CCM ishindwe.

  Wabunge hao walitaka Makamba pamoja na baadhi ya wajumbe wa sekretarieti wang’oke, kwa madai kuwa wapo wenye vyeo zaidi ya vitatu wakati kuna baadhi ya makada wasio na cheo hata kimoja lakini wana uwezo - tena kuwashinda waliolimbikiziwa vyeo.

  Waliwataja viongozi wenye vyeo zaidi ya kimoja mbali ya Makamba, ambaye ni kiongozi mmoja wa juu serikalini mwenye wadhifa wa kitaifa ndani ya chama, na John Chiligani, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; mbunge na Katibu wa Uenezi na Itikadi Taifa wa CCM.

  Waliwataja wanachama wanaodaiwa kukumbatiwa na Makamba na aliowatumia kwenye kampeni za Tarime kuwa ni Richard Hiza Tambwe, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Propaganda; na Shaibu Akwilombe - wote waliojiunga na CCM hivi karibuni wakitokea vyama vya upinzani.

  “Kitendo cha Makamba kuwatumia Tambwe, Akwilombe na Steven Mashishanga kwenye kampeni hizo badala ya kuwatumia wenyeji wa eneo hilo, ndicho kilichochangia kwa kiasi kikubwa kulikosa jimbo hilo kwa vile hawakuwa wakijua siasa za Tarime zinavyofanywa,” alisema mmoja wa wabunge katika mkutano huo.

  Wabunge hao walitaja sababu nyingine ya CCM kushindwa Tarime kuwa ni kitendo chake cha kulala nyumbani kwa mfanyabiashara Mwita Gachuma, kwa madai kuwa hatua hiyo iliwagawa wana-CCM, kwani mfanyabiashara huyo amekuwa akitajwa kuwa na tofauti za kisiasa na kada mwingine wa chama hicho wa huko huko Tarime, Kisyeri Chambiri.

  Wabunge hao ambao baadhi yao ni wajumbe wa kikao cha Halmashauri Kuu ya (NEC), kinachokutana wiki hii Dodoma, wamepania kuleta hoja hiyo ndani ya kikao hicho na baadhi ya wajumbe wameshawasili kwa ajili ya kikao hicho.

  Wakati wabunge wakitoa shinikizo hilo kwa Makamba, viongozi wa Ofisi Ndogo ya CCM, Dar es Salaam na Dodoma, walisema wabunge hao hawana mamlaka ya kumwengua Makamba na kwamba wamekiuka kanuni na taratibu za chama.

  Taarifa iliyotolewa na Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya tawi la CCM, Ofisi Ndogo Dar es Salaam, imemtetea Makamba kuwa ni mtu safi. Shutuma zilizotolewa dhidi yake na baadhi ya wabunge ni za uongo.

  “Kamati imeshindwa kuelewa kama kweli taarifa hizo za kwenye vyombo vya habari zilitoka kwa wabunge wa CCM hadi hapo itakapothibitishwa na wao wenyewe,” ilisema taarifa hiyo.

  “Tumeshindwa kuamini kutokana na kufahamu kwamba kamati ya wabunge wa CCM ina majukumu yake yaliyoainishwa vizuri na hayahusiani hata kidogo na masuala ya kupinga au kutaka kumwondoa kiongozi yeyote katika ngazi ya chama. Kamati ya siasa ya tawi inaamini kuwa wabunge wetu ni waelewa, wenye ufahamu mkubwa wa majukumu yao na kwamba hawawezi kufikia uamuzi huo,” ilisema taarifa hiyo.

  Taarifa nyingine ya kumtetea Makamba ilitoka Dodoma ambako Kamati ya Siasa Tawi la Makao Makuu Dodoma ilisema kuwa tuhuma hizo hazina maana na kuwataka wana-CCM wazipuuze.

  Taarifa hiyo ilibeza tabia ya baadhi ya viongozi wa CCM kutumia vyombo vya habari badala ya vikao halali vya chama katika ngazi husika kuwa ni ukiukwaji wa katiba, kanuni na maadili ya uongozi.

  Katika hatua nyingine, kinyang’anyiro cha kuziba nafasi ya mjumbe wa NEC iliyoachwa wazi na Jaka Mwambi, kimeshika kasi na kuwagawa wajumbe katika makundi.

  Zaidi ya wagombea 30 wamejitokeza kuziba nafasi hiyo, lakini waliopendekezwa na kikao cha Kamati Kuu (CC) ni watatu. Nao ni Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba, Meneja Uhusiano wa Benki ya National Microfinance (NMB), Shy-Rose Bhanji, na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Salum Londa.

  Mwambi alikuwa mjumbe wa NEC lakini nafasi yake ilibaki wazi baada ya kuteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania Urusi. Nafasi hiyo itajazwa katika kikao cha NEC wiki hii.
   
 2. Single D

  Single D JF-Expert Member

  #2
  Nov 7, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 459
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hivi kumbe Mashishanga naye alikuwa Tarime?Alienda kama nani?
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Nov 7, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,854
  Likes Received: 83,338
  Trophy Points: 280
  Imetolewa mara ya mwisho: 07.11.2008 0130 EAT

  • Pinda akabidhiwa 'kitanzi' cha Makamba

  *Yeye akirusha kwa Mwenyekiti wa CCM

  Na Grace Michael, Dodoma
  Majira

  SHINIKIZO la wabunge wa CCM la kutaka kung'olewa kwa Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusuph Makamba, limechukua sura mpya baada ya wabunge wa chama hicho kuwasilisha hoja hiyo kwa Mwenyekiti wa Wabunge wa CCM, Bw. Mizengo Pinda, kwa madai kuwa anakigawa chama.

  Hatua hiyo ilijitokeza juzi jioni katika kikao cha wabunge hao ambacho kilipangwa kufanyika saa 10 jioni, lakini kikachelewa kutokana na mgongano wa wabunge hao ambao baadhi ya hoja zilizokuwa mezani lizipingwa.

  Kwa mujibu wa chanzo cha habari cha kuaminika kutoka ndani ya chama hicho, katika mambo yaliyozungumzwa ni hoja ya kutaka kung'olewa kwa Bw. Makamba katika kiti hicho, kwani amekuwa akifanya mambo yanayowagawa wana CCM.

  "Hoja hii tumeifikisha kwa Mwenyekiti wetu ambaye naye anasema hawezi kutoa jibu, bali atalifikisha kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa, ambaye ni Rais Jakaya Kikwete," kilisema chanzo hicho.

  Sababu za kutaka aachie nafasi hiyo ni madai ya kupokea wanachama kutoka vyama vya upinzani na kuwapa madaraka makubwa bila uchunguzi wa kutosha.

  "Mbali na hili, jingine ni la Tarime ambako alipeleka watu wasiokuwa na uzoefu wa kutosha katika masuala ya kampeni, lakini kubwa zaidi alifikia kwa mwanachama mmoja kitendo kilichowakera wana CCM wengine na kwa kufanya hivyo, ni kuwagawa wanachama," kilisema chanzo cha habari.

  Tuhuma nyingine ya Bw. Makamba ni kuwachonganisha wabunge hao na wananchi kwa kile alichokitangaza kuwa hawaendi majimboni mwao.

  Suala lingine lililoibuka ndani ya mkutano huo, ni wabunge hao kupendekeza baadhi ya mawaziri wenye nyadhifa kubwa ndani ya chama, kuchagua suala moja la ama kuachia ngazi ya uwaziri au nafasi ya uongozi katika chama.

  "Wapo hawa mawaziri hawana muda sasa wa kukitumikia chama vizuri, hivyo ifike mahali wachague kitu kimoja, kwani lengo letu sasa ni kukijenga chama na si kuendelea kukibomoa," kilisema chanzo kingine cha habari.

  Kitu kingine kilichoibuka ni wabunge wa viti maalumu kuingilia wenzao katika majimbo yao, hali inayoleta picha mbaya na kuonesha tamaa ya madaraka.

  Masuala haya mazito yalijitokeza wakati wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wanatarajia kuanza mkutano wao mjini hapa kesho, ambao unatarajiwa kuwa na ajenda nzito.

  Akizungumza juzi na gazetihili, Bw. Makamba alikanusha kuwapo kwa mpango huo, akisema ni hisia za mtu mmoja na kama zingekuwa za wabunge wa CCM angeshapata taarifa.

  Alitaka mawazo hayo yachukuliwe kama masuala ya mitaani na kwamba vikao maalumu ndivyo vinavyoweza kuamua hatima yake.

  Baadhi ya viongozi waliotoka Upinzani na kupewa nyadhifa ndani ya CCM ni Bw. Tambwe Hiza aliyekuwa CUF, Bw. Salum Msabah kutoka CUF na wengineo.
   
Loading...