Makamba adai ana miaka minne ya kuishi ambao afe kwa amani, azikwe kwa heshima | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makamba adai ana miaka minne ya kuishi ambao afe kwa amani, azikwe kwa heshima

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pdidy, Nov 8, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 8, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,520
  Likes Received: 5,752
  Trophy Points: 280
  Na Joyce Mmasi

  KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) amewaomba watu wanaomfuatafuata kumuacha ili afe kwa heshima kutokana na kubakiza miaka michache ya kuishi duniani.

  Makamba alitoa kauli hiyo juzi alipozungumza kwenye mahafali ya wanafunzi wa Shule za St Anne Marie eneo la Mbezi kwa Msuguli jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

  Aliwataka watu wasiomtakia mema kuacha kumfuatafuata na badala yake waachwe afe kwa heshima kwa kuwa amebakia miaka minne afikishe umri wa kuishi duniani.

  Akinukuu vifungu kwenye Biblia , Makamba alisema umri mtu kuishi duniani ni miaka 70 na wachache ni 74 na akasema yeye amefikisha umri wa miaka 71, hivyo anapaswa aachwe amalizie miaka mine iliyosalia ili azikwe kwa heshima.

  "Mimi nina miaka 71 sasa, nimebakiza miaka mine tu nife, lakini kuna watu wananifuata ooh Makamba kafanya hivi, wanataka kuniharibia bure, kwanini wasiniache nife nizikwe kwa heshima" alisema Makamba na kuwaacha watu wakiangua kichezo.

  Akizungumzia utendaji kazi kwa walimu nchini, Makamba aliwataka kuongeza upendo kwa watoto wanaowafundisha ili kuweka kichocheo kwa wanafunzi wapende kusoma na kuwa na bidii katika masomo.

  Makamba alisema, walimu ni watu muhimu wanaoweza kudumaza au kupandisha kiwango cha kufaulu kwa wanafunzi na kwamba penye upendo pana elimu, na mwalimu mzuri ni yule anayeonyesha upendo kwa wanafunzi na kwa masomo anayofundisha.

  Katibu Mkuu aliwakumbusha walimu nchini kwamba wanafunzi wengi ni vijana na ni taifa la kesho na akasema kwa kuwalea katika maadili ya kupenda kusoma ni kusaidia kujenga taifa imara lenye wasomi wengi na wazuri.

  Alilaumu tabia ya baadhi ya walimu wanaogoma kufundisha akisema mwalimu anapogoma kufundisha asifikiri anamgomea mwajiri wake au serikali na badala yake wajue kuwa wanawagomea watoto hao.

  Awali akizungumza wakati akimkaribisha, Mkuu wa shule hizo Nelson Theonest alisema wanafunzi wote waliomaliza shule waliandaliwa vizuri na wote wapo tayari kujiunga na shule zingine kila mmoja kwa kiwango chake na akawapongeza wanafunzi wote kwa adabu na utii walioonyesha shuleni hapo kwa muda wote waliokuwa wakisoma. Katika mahafali hayo, jumla ya wanafunzi 359 wadarasa la saba, kidato cha nne na cha sita, walimaliza shule na kukabidhiwa vyeti vyao
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Nov 8, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,520
  Likes Received: 5,752
  Trophy Points: 280
  kwa mtaji huu wa kushiirikiana na mafisadi mbona minne mingi sana;;huyu babu ajasoma vizuri kwenye biblia....kaama anataka afe vizuri aache ufisadi..aachane na njaa za kushirikiana na wakina lowassa..rostam...na mafisadi wengineo...aache kushambulia wale wanaoitakia nchii hii mema...nje ya hapo hata akikaa miaka 8 wacha 4 tutmfwata na kumsema huko aliko ata iwe makaburini KINDONI...tutapeleka malalamiko yetu huko kwa alichowafanyia watanzania.......d u hera war am saying babu...we mtu mzuri sana aukuwa hivyo tatizo ulivyoonjeshwa shubiri ya mafisadi na kupkea vijisent vya kampeni ndio kichwa kimenata asali...babu asali ikiyeyuka hata ufanye nini aisadii.....MI USAHURI WANGU OMBA WATANZANIA WAKUOMBEE UBADILIKE USIISHI MAISHA YA KIFISADI UISHI MAISHA YANAYOMPENDEZA MUNGU...
   
 3. S

  Selemani JF-Expert Member

  #3
  Nov 9, 2009
  Joined: Aug 26, 2006
  Messages: 871
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  One day when you are 71 yrs old, with unprecedented wealthy of political experience. You will understand.
   
 4. a

  alles JF-Expert Member

  #4
  Nov 9, 2009
  Joined: Oct 14, 2006
  Messages: 356
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pdidy hapo ulipoitoa habari ya makamba(Mwananchi news paper) chini yake kuna habari ya kushtua kidogo inasema "Chadema sasa hali si shwari waendesha vikao vya siri kuwajadili wanachama"Kafulira, Danda Juju na Shida Salum(Mama yake Zitto) out.Please kama unatime ipost JF wajumbe waicheck.Nilipo sina access mzuri ya net.
   
 5. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #5
  Nov 9, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Ni kweli,filosofia yangu binafsi ni kwamba mtu akishafika miaka ya sabini asiruhusiwe kugombea kiti chochote umri huu wengi huwa wamekataa tamaa ya maisha hivyo huyaangalia mambo yaende bila kujihangaisha.

  Umri huu mara nyingi huwaza kufa ,nakujaribu kuchuma mali za kuwaachia watoto/ndugu.

  Mgombea wa urais inatakiwa anapogombea asizidi miaka 70, mgombea wa urais anatakiwa kupimwa afya kabla ya kuingia ktk kinyang'anyiro cha urais asiwe na gonjwa la kudumu.
   
 6. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #6
  Nov 9, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Njaa si mchezo,du!
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Nov 9, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,776
  Likes Received: 83,117
  Trophy Points: 280
  Tangu lini fisadi akazikwa kwa heshima? Heshima kutoka wapi na heshima za kipi alichokifanya mpaka astahili kuzikwa kwa heshima?
   
 8. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #8
  Nov 9, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Man this forl is very interesting. Now i know the trick nikifikisha miaka 69 nitaiba sana na nikifikisha 71 nitawaomba watu waniache nife salama.

  Ntawapuuza walimu na kuwaminya kisawsawa, nikikaribia kuondolewa kwenye nafasi yangu nitawasifu sana kwa mchango wao. Sounds smart
   
 9. RasJah

  RasJah JF-Expert Member

  #9
  Nov 9, 2009
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 697
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hii Graduation ya aina yake na yenyewe, mbona kama haijakaa vizuri, Graduation gani ya darasa la saba, form four na Six pamoja??
   
 10. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #10
  Nov 9, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Hivi kwa nini hawa wana siasa wana alikwa sehemu kama hizi? Mtu anaenda kwenye mahafali ya wanafunzi badala awape wosia kama mtu mzima anaanza kuongelea matatizo yake ya kisiasa. Na siyo kwenye mahafali tu hata wakialikwa sehemu zingine kama kanisani au misikitini bado ni siasa tu. There is a time and place for verything GODDAMN IT!
   
 11. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #11
  Nov 9, 2009
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  aaagrrr hii ndo hotuba ya kutoa kwa wanafunzi wa sekondari? ....na jukwaa la siasa atasema nini?
   
 12. I

  Irizar JF-Expert Member

  #12
  Nov 9, 2009
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 217
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ohhh Makamba ni kituko, jamani hata kama ukiwa mzee ukiwa mwizi ni lazima tuseme. Ukizeeka siyo ticket ya kuwsifia na kuwabeba MAFISADI.
   
 13. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #13
  Nov 9, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,520
  Likes Received: 5,752
  Trophy Points: 280
  mkuu nimeshaituma nimeandika CHADEMA HAKUKALIKI
   
 14. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #14
  Nov 9, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,520
  Likes Received: 5,752
  Trophy Points: 280
  weeeeeeeeeee njaaaaaaaaaa baba achana na nja huyu mzeeeee nema imemkuta uzeni sasa zile resi za kula chako mapema za ujanani anazifanya uzeeeni ndio mmaaana wakina rostam wanakula kuku pembeni yake......ngrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
   
 15. Original Pastor

  Original Pastor JF-Expert Member

  #15
  Nov 9, 2009
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 1,256
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mdogo wangu Januari vipi? mama anasema amebakiza miaka nne kweli umejiandaa na mazishi? ya Mzee? maana ametamka mwenyewe. Tunaomba ushauri
   
 16. W

  WildCard JF-Expert Member

  #16
  Nov 9, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kinachoudhi zaidi ni hadhira alooitumia kueleza "wosia" wake huu. Mtoto wa darasa la saba unamweleza suala la wewe kuendelea kubaki madarakani ili iweje! Makamba amechoka. CCM haijawahi kuwa KATIBU MKUU mzee kama huyu.
   
 17. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #17
  Nov 9, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,520
  Likes Received: 5,752
  Trophy Points: 280

  we unamwona katibu huyo ndie ndondocha wao anaefanya ccm inashinda kila uchaguzi
   
 18. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #18
  Nov 9, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Hii ni kufru na kibri cha hawa watu wanaopata madaraka kidogo ya kidunia na baadaye wanamsahau muumba.

  Nakumbuka maneno hata aliwahi kutamka hata Nyerere katika moja ya birthday yake na kusema kuwa haoni sababu yeye asifikishe miaka 80. Je alifika?

  Haya tumuone makamba naye? Tumuombee
   
 19. W

  WildCard JF-Expert Member

  #19
  Nov 9, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Ryan Giggs/Man U; Makamba/CCM?
   
 20. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #20
  Nov 9, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,520
  Likes Received: 5,752
  Trophy Points: 280
  Oooooooooooooh yeaahh.......Drogba/chelsea
   
Loading...