Elections 2010 Makamba aanza zogo jipya!

Ng'wanza Madaso

JF-Expert Member
Oct 21, 2008
2,268
333
By Waandishi wetu
20th November 2010


headline_bullet.jpg
Achochea walibwagwa ubunge wakatae matokeo
headline_bullet.jpg
Pia wa udiwani, aagiza wote wafungue kesi kortini
headline_bullet.jpg
Gharama zote za mawakili kubebwa na CCM


Makamba2%286%29.jpg

Yusuf Makamba

Baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupoteza majimbo 53 ya ubunge katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 31, mwaka huu, Katibu Mkuu wake, Yusuf Makamba sasa ameamua kila mgombea ubunge na udiwani aliyeshindwa afungue kesi ya kupinga matokeo.


Hatua hii inayotafsiriwa kama kukutaa kutambua matokeo ya uchaguzi wa wabunge na madiwani, inathibitisha mtikisiko ndani ya chama hicho na wagombea wote walioshindwa wa ubunge na udiwani wametakiwa kufungua kesi mahakamani katika kipindi cha siku 30 kuanzia kutangazwa kwa matokeo hayo.


NIPASHE ina taarifa za barua ya siri iliyoandikwa na Makamba kwenda kwa Makatibu wote wa CCM nchini ikiwataka wagombea wote wa CCM walioshindwa uchaguzi, kufungua kesi mahakamani.


Barua hiyo ambayo NIPASHE imeiona yenye kumbukumbu namba CCM/OND/636/VOL.11/122 iliyoandikwa Novemba 9, 2010, ikiwa imesainiwa na Makamba na inaonyesha kuwa ilipokewa na makatibu wa CCM wa mikoa.


Katika barua hiyo, Makamba anawataka wagombea wa ubunge kufungua kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania huku wagombea udiwani walioangushwa kwenda kufungua kesi katika mahakama za mahakimu wakazi ndani ya siku 30, tangu ulipofanyika uchaguzi huo Oktoba 31, mwaka huu.


Makamba anawaagiza makatibu wa CCM wa mikoa kwa kushirikiana na makatibu wa CCM wa wilaya na kata kuwasaidia wagombea hao walioshindwa kwenye uchaguzi kuandaa hoja za malalamiko na vielelezo kwa ajili ya kupeleka mahakamani.


Aidha, Makamba ameagiza kuwa baada ya hoja hizo za malalamiko kukamilika zipelekwe katika ofisi ndogo ya CCM jijini Dar es Salaam au kuwasiliana moja kwa moja kwa mawakili ambao ni makada wa CCM ili kuandaa hati za malalamiko ndani ya muda huo.


“Kwa barua hii, mshirikiane na makatibu wa CCM wilaya/kata na wagombea husika kuandaa hoja za malalamiko na vielelezo/ushahidi na kuwasilisha CCM ofisi ndogo Dar es Salaam au kuwasiliana na mawakili ambao ni makada wetu moja kwa moja ili kuandaa hati za malalamiko ndani ya muda huo,” ilisema sehemu ya barua hiyo ya Makamba.


Katika barua hizo, Makamba pia amewaahidi wagombea wasiokuwa na uwezo wa kifedha kuwa chama kitachangia gharama za mawakili ili kuwasaidia kufanikisha azma hiyo.


“Chama Cha Mapinduzi Makao Makuu kitachangia gharama za mawakili kwa wagombea ambao hawana uwezo wa kifedha,” ilisema sehemu ya barua hiyo.


Katibu huyo wa CCM Taifa anahitimisha barua yake kwa kuwataka makatibu wa CCM wa mikoa kusimamia ipasavyo maagizo hayo ili kuhakikisha kuwa kesi hizo zinafunguliwa mahakamani.


Akizungumzia barua hiyo,Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilaya ya Mbeya Mjini, John Mwambigija, alisema shinikizo hilo la CCM kwa wagombea wake kukimbilia mahakamani linaonyesha kuwa chama hicho kinataka ushindi wa nguvu badala ya kuridhika na maamuzi ya wananchi.


Alisema kwa kuwa chama hicho kina fedha nyingi, kinataka kuzitumia kuzima demokrasia, na ndiyo sababu kubwa ya kuwataka wagombea wake walioangushwa kwenye uchaguzi kukimbilia mahakamani huku kikiwaahidi kuwasaidia gharama za kuendesha kesi.


Uchunguzi umebainisha kuwa baada ya agizo hilo kuwafikia mmoja wa viongozi wa CCM wa Wilaya ya Mbeya Mjini, ameonekana akiwaita wagombea wa udiwani walioshindwa akiwataka wakafungue kesi mahakamani.


Aidha, mapema wiki hii, aliyekuwa mgombea ubunge wa CCM katika Jimbo la Mbozi Magharibi na kuangushwa, Dk. Lucas Siyame, aliwaambia waandishi wa habari jijini Mbeya kuwa anakusudia kufungua kesi Mahakama Kuu kupinga matokeo ya uchaguzi huo, kwa madai kuwa msimamizi wa uchaguzi aliyatangaza matokeo hayo yaliyompa ushindi mpinzani wake kupitia Chadema bila kuhakikiwa na mawakala wake, hali ambayo inadaiwa na Mwambigija kuwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Makamba.


Mkoani Mbeya, CCM ilipoteza majimbo mawili ya Mbeya Mjini na Mbozi Magharibi ambayo yaliangukia mikononi mwa Chadema huku katika Jimbo la Mbeya Mjini CCM ikipoteza kata 14, ambapo kata 12 zilinyakuliwa na Chadema na kata mbili zilichukuliwa na NCCR-Mageuzi.


NIPASHE lilipomtafuta Makamba jana kuzungumzia agizo hilo, alijibu kuwa ni umbeya na kwamba barua hiyo haiwahusu waandishi wa habari.


“Hiyo barua inakuhusu nini. Huo ni umbeya, acha umbeya, tukiandika barua zetu unazipataje?” alihoji kisha akakata simu.


Kabla Makamba hajatoa agizo hilo, aliyekuwa Meneja wa kampeni wa CCM, Abdurrahman Kinana, aliahidi kuwa chama chake kitatoa msaada kwa wagombea walioshindwa ikiwa wataamua kwenda mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi.


Kinana alitoa kauli hiyo wakati Tume ya Uchaguzi ilipokuwa ikikaribia kukamilisha zoezi la kutangaza matokeo, baada ya CCM kufanya tathmini ya uchaguzi huo na kubaini kuwa kingepoteza majimbo ya ubunge 50.


Imeandikwa na Emmanuel Lengwa (Mbeya) na Restuta James (Dar).

SOURCE: NIPASHE
 
Du! huyo mzee kila kukicha anakuja na PUMBA MPYA, toka nimemfahamu over 15 years sijapata kusikia akiongea habari za maana, sijui hata huko aliko amefikaje.
 
Kwahiyo anataka kutumia rungu la Kikwete kuwa rais kuwashinikiza mahakimu kuwanyang'anya ushindi wabunge wa upinzani? Huyu mzee vipi jamani? kwanza kuna wabunge wao (CCM) wengi tu ambao wametangazwa wahindi huku ikionyesha wazi kuwa walishindwa kwenye masanduku ya kura. Makamba please usituletee migogoro nchini kwetu. Si CCM mmesema mnaendeleza amani na utulivu mbona unataka kuchafua hali ya hewa sasa? Kwa maana nina uhakika wa asilimia 100 % hakuna mbunge wala diwani wa upinzani aliyeshinda kwa kura za mezani. Kwa maana hiyo wananchi waliowachagua hao wabunge na madiwani hawatakuwa tayari kuona mbuge/diwani wao waliyemchagua ananyang'anywa ushindi mahakami kisa mahakimu wako chini ya serikali ya Kikwete.
 
Huna jipya Makamba, subiri kufukuzwa kazi kwa kukigawanya chama!

Ndiyo maana ulifukuzwa ualimu wa shule!
 
Hii ni technique ambayo CCM wameiona ni muafaka ya kufload mahakama na kesi zisizokuwa na miguu wala kichwa za uchaguzi ili kuwasaidia akina Makongoro ambao ni dhahiri kama haki itafuatwa watapoteza viti walivyopewa na wasimamizi wa uchaguzi. Mbinu hii ni kuzifanya kesi ziwe nyingi na kupoteza muda wa kuzisikiliza ili kama ni maamuzi ya kutengua yafanyike mwishoni mwa 2014.

Hakuna jipya zaidi ya hilo. Ila pamoja na kuwa wao wanaweza chezea hela za walipa kodi kwa kesi za kimagilini sisi wananchi tutawachangia wapinzani halisi ili kuhakikisha haki yao haipotei.
 
huku arusha kwetu wakibadilisha matokeo itabidi watu wao wote wa serikali wawatafutie mji mwingine...mziki wetu wanautambua hasa wanapotaka kuchakachua haki yetu....
 
Hivi ni mawazo ya Makamba au kuna baraka za chama? Kweli Tanzania demokrasia bado. Makamba alitaka CCM ipate 100%? Hivi jaji mkuu na mwanasheria wa serikali wanalionaje hili? Kuwalazimisha walioshindwa kufungua kesi mahakamani jamani hii inaonyesha kuwa chama kina mushkeli. Hata sisi wakereketwa tunaanza kutia mashaka hiki chama kinakotupeleka. Uchaguzi siyo vita kuna kushinda na kushindwa unapogeneralise walioshindwa wote kufungua kesi hapo tunaanza kujiuliza kama ni maamuzi ya kikao au mtu binafsi? Mwenyekiti wa CCM na wakuu wengine mlitazame hili jambo
 
Huna jipya Makamba, subiri kufukuzwa kazi kwa kukigawanya chama!

Ndiyo maana ulifukuzwa ualimu wa shule!

Mkuu in the presence of Kikwete Makamba kufukuzwa kazi sahau. Si unamuona alivyo na jeuri mpaka anasema mtoto wake asipopewa uwaziri atashangaa? Iko siri kubwa hapo.
 
huku arusha kwetu wakibadilisha matokeo itabidi watu wao wote wa serikali wawatafutie mji mwingine...mziki wetu wanautambua hasa wanapotaka kuchakachua haki yetu....



acha kudanganya watu
 
hiyo nundu jamaa kashonea hirizi maana ikianza kuwasha anaamua jinsi anavyojua hata kama ni pumba. Kazi manyo CCM mwaka huu.
HATUDANGANYIKI! Hatumtambui Mkwere, usiku hata mchana, wakati wa njaa au shibe. HATUDANGANYIKII.
 
那坑洼裤袜 mahakimu wote ni wao watashinda tuuuu,haya jamani ni makamba huyo asiwaumize kichwa kwanini hizo pesa zisitumike kwa kazi nyingine?

mapinduziii daimaaaaaa
 
sijui hata huko aliko amefikaje.

hata mie nimekua najiuliza hili swali bila majibu, wakati mkuu wa mkoa alikua haonyeshi sana lakini sasa hivi, UBUKI (Upungufu wa Busara Kichwani) unajidhihirisha kila kukicha
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom