nickname
JF-Expert Member
- Dec 20, 2009
- 544
- 147
Yusuf Makamba
Hatua hii inayotafsiriwa kama kukutaa kutambua matokeo ya uchaguzi wa wabunge na madiwani, inathibitisha mtikisiko ndani ya chama hicho na wagombea wote walioshindwa wa ubunge na udiwani wametakiwa kufungua kesi mahakamani katika kipindi cha siku 30 kuanzia kutangazwa kwa matokeo hayo.
NIPASHE ina taarifa za barua ya siri iliyoandikwa na Makamba kwenda kwa Makatibu wote wa CCM nchini ikiwataka wagombea wote wa CCM walioshindwa uchaguzi, kufungua kesi mahakamani.
Barua hiyo ambayo NIPASHE imeiona yenye kumbukumbu namba CCM/OND/636/VOL.11/122 iliyoandikwa Novemba 9, 2010, ikiwa imesainiwa na Makamba na inaonyesha kuwa ilipokewa na makatibu wa CCM wa mikoa.
Katika barua hiyo, Makamba anawataka wagombea wa ubunge kufungua kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania huku wagombea udiwani walioangushwa kwenda kufungua kesi katika mahakama za mahakimu wakazi ndani ya siku 30, tangu ulipofanyika uchaguzi huo Oktoba 31, mwaka huu.
Makamba anawaagiza makatibu wa CCM wa mikoa kwa kushirikiana na makatibu wa CCM wa wilaya na kata kuwasaidia wagombea hao walioshindwa kwenye uchaguzi kuandaa hoja za malalamiko na vielelezo kwa ajili ya kupeleka mahakamani.
Aidha, Makamba ameagiza kuwa baada ya hoja hizo za malalamiko kukamilika zipelekwe katika ofisi ndogo ya CCM jijini Dar es Salaam au kuwasiliana moja kwa moja kwa mawakili ambao ni makada wa CCM ili kuandaa hati za malalamiko ndani ya muda huo.
Kwa barua hii, mshirikiane na makatibu wa CCM wilaya/kata na wagombea husika kuandaa hoja za malalamiko na vielelezo/ushahidi na kuwasilisha CCM ofisi ndogo Dar es Salaam au kuwasiliana na mawakili ambao ni makada wetu moja kwa moja ili kuandaa hati za malalamiko ndani ya muda huo, ilisema sehemu ya barua hiyo ya Makamba.
Katika barua hizo, Makamba pia amewaahidi wagombea wasiokuwa na uwezo wa kifedha kuwa chama kitachangia gharama za mawakili ili kuwasaidia kufanikisha azma hiyo.
Chama Cha Mapinduzi Makao Makuu kitachangia gharama za mawakili kwa wagombea ambao hawana uwezo wa kifedha, ilisema sehemu ya barua hiyo.
Katibu huyo wa CCM Taifa anahitimisha barua yake kwa kuwataka makatibu wa CCM wa mikoa kusimamia ipasavyo maagizo hayo ili kuhakikisha kuwa kesi hizo zinafunguliwa mahakamani.
Akizungumzia barua hiyo,Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilaya ya Mbeya Mjini, John Mwambigija, alisema shinikizo hilo la CCM kwa wagombea wake kukimbilia mahakamani linaonyesha kuwa chama hicho kinataka ushindi wa nguvu badala ya kuridhika na maamuzi ya wananchi.
Alisema kwa kuwa chama hicho kina fedha nyingi, kinataka kuzitumia kuzima demokrasia, na ndiyo sababu kubwa ya kuwataka wagombea wake walioangushwa kwenye uchaguzi kukimbilia mahakamani huku kikiwaahidi kuwasaidia gharama za kuendesha kesi.
Uchunguzi umebainisha kuwa baada ya agizo hilo kuwafikia mmoja wa viongozi wa CCM wa Wilaya ya Mbeya Mjini, ameonekana akiwaita wagombea wa udiwani walioshindwa akiwataka wakafungue kesi mahakamani....
Source : NIPASHE 20th Novemba 2010