Makamba aanza rasmi kuwapigia debe watoto wake ubunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makamba aanza rasmi kuwapigia debe watoto wake ubunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwenda_Pole, Oct 18, 2009.

 1. Mwenda_Pole

  Mwenda_Pole JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2009
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 260
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  HARAKATI za kuwania ubunge kwenye majimbo mbalimbali mkoani Tanga zimeshika kasi, huku kukizuka malalamiko katika baadhi ya maeneo kuwa baadhi ya vigogo wa CCM wameanza mchezo mchafu; akiwemo Katibu Mkuu, Yusuf Makamba ambaye anadaiwa kumwandalia njia kijana wake.

  Makamba anadaiwa kuwa ameingia katika baadhi ya majimbo na kuendesha kampeni za kuwang'oa wabunge waliopo na kuwawekea mazingira ya ushindi watoto wake.

  Hata hivyo Makamba alikanusha kufanya kampeni hizo chafu kwa sababu yeye ni kiongozi wa juu wa chama na kwamba, wanaosema hivyo wamkome kabisa kumsingizia.

  Inadaiwa kuwa mtendaji mkuu huyo wa CCM ameandaa kundi maalumu linaloendesha kampeni kwa mgongo wa Jumuiya ya Vijana (UVCCM) likiwa na kauli mbiu ya kutaka majimbo yote ya Tanga yanyakuliwe na wabunge vijana.

  Malalamiko dhidi ya Makamba yameenea katika majimbo ya Bumbuli na Korogwe Vijijini ambako anadaiwa ameanza mikakati ya kumuandaa mtoto wake Januari Makamba, ili awanie ubunge katika moja ya majimbo hayo.

  Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi Jumapili umebaini kwamba, mwezi uliopita Makamba aliandaa ziara ya kutembelea kata za Jimbo la Bumbuli, lakini akakumbana na vikwazo na kulazimika kubadilisha msimamo na kuondoka.

  Viongozi wa CCM waliopo wilayani Lushoto walidai kuwa akiwa katika jimbo hilo alikuwa akifanya mikutano ya ndani ya wanachama wa CCM akiwashawishi wasimchague Mbunge wa sasa,William Shellukindo katika uchaguzi ujao badala yake atamleta kijana wake Januari kuchukua nafasi hiyo.

  Inadaiwa kuwa katika mikutano hiyo ya ndani Makamba alieleza wazi kuwa asingependa Shellukindo apewe tena nafasi ya ubunge kwa kuwa yupo mstari wa mbele katika kuendesha mapambano dhidi ya mafisadi.

  Diwani wa Kata ya Baga CCM, Charles Ndege alisema mchezo unaofanywa na Makamba katika Jimbo la Bumbuli sio wa kuunyamazia kwa sababu unaleta mvurugano miongoni mwa wanachama wa CCM.

  Alisema wananchi wanashangaa kuona kiongozi kama Makamba, anaamua kucheza mchezo mchafu wa kupiga vita wanaopambana na ufisadi.

  "Hata nikipelekwa popote sitanyamaza, Makamba amefanya vikao vya siri katika kijiji cha Mahezangulu, Kwebaga na vijiji vingine, akimponda Shellukindo," alisema Ndege na kudai kuwa kundi la UVCCM linalopita vijijini linaongozwa na baadhi ya viongozi wake wa Wilaya ya Lushoto.

  Diwani huyo alisema miongoni mwa mambo yanayofanywa na timu hiyo ya vijana, ni kuonyesha picha ya Januari ambayo alipiga pamoja na Rais Jakaya Kikwete, wakidai kuwa rais ameagiza achaguliwe kuwa mbunge wa jimbo hilo.

  Mbali na Januari anadaiwa pia kumuandaa binti yake, ili awanie nafasi ya ubunge wa viti maalumu kupitia Jumuiya ya Wanawake (UWT), Mkoa wa Tanga.

  Alipohojiwa na Mwananchi Jumapili kuhusiana na taarifa hizo, Mbunge wa Jimbo la Bumbuli, William Shellukindo alisema hata yeye amesikia, lakini hana hofu kwa wagombea kwenda kuwania nafasi hiyo huku akisisitiza kuwa wafuate taratibu badala ya kutumia mchezo mchafu.

  "Hilo mimi nimelisikia wananchi wakilalamika, lakini ninachosema ni kwamba, kama wanajiamini hakuna haja ya kutumia mchezo mchafu wa kuanza kampeni kabla ya wakati, badala yake wasubiri muda ufike halafu wapige kura wataamua," alisema Shellukindo.

  Katika Jimbo la Korogwe Vijijini linaloshikiliwa na Lous Mhina, wanaCCM wamedai kuwa, Makamba amekuwa akipima upepo kuona iwapo mtoto wake Januari anaweza kulichukua.

  "Makamba anafanya vikao vya siri na kuwapanga wapiga debe maalumu kwa ajili ya mtoto wake huyo, lakini mbona anaanza kampeni mapema?

  Inakuwaje yeye ni kiongozi halafu anakuwa wa kwanza kuvunja utaratibu tuliojiwekea ndani ya chama," alisema kada mmoja wa CCM anayeishi Kata ya Mashewa wilayani Korogwe.

  Mwananchi Jumapili ilipozungumza na Mbunge wa jimbo hilo alisema siyo rahisi jimbo lake kutwaliwa na mtu mwingine kama baadhi ya watu wanavyodhani.

  "Mimi si mtu wa kujisifu, lakini kuna mambo mengi ya maendeleo nimeyafanya na wananchi wanatambua hilo. Makamba namheshimu kama Katibu Mkuu wangu wa CCM na pia mzee wangu; hivyo sitegemei kama atakuwa mstari wa mbele katika kuongoza mchezo mchafu. Lakini hayo nimeyasikia,"alisema Mhina.

  Alipoulizwa na gazeti hili kwa njia ya simu kuhusiana na tuhuma hizo, Makamba, alikanusha vikali na kusisitiza kuwaƂ yeye ni kiongozi wa ngazi za juu wa CCM, hivyo hawezi kushiriki katika kampeni za mchezo mchafu.

  "Mimi na Shellukindo ni kitu kimoja, huyu ni kada wetu muhimu sana bungeni na ni kiongozi anayeheshimika si kwa Tanzania pekee hata nje ya nchi, amesaidia mambo mengi katika taifa hili. Hao wanaosema hivyo wanikome," alisema Makamba.

  Kuhusu Jimbo la Korogwe Vijijini, Makamba alisema yeye ni mzaliwa wa huko na kutaja eneo la Mahezangulu kuwa ndipo nyumbani kwake na kwamba, huwa anakwenda huko wakati wowote hivyo si kufanya kampeni.

  "Mimi nilishasema sigombei ubunge, hili nilitangaza rasmi tena pale Korogwe, sasa suala la Januari kama anagombea, hilo mimi siwezi kumuingilia kwani naye ni mwanaCCM na ana matakwa yake," alisema Makamba.

  Chanzo: Mwananchi 17.10.2009
   
 2. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Ni tabia ya waafrika kurithishana madaraka.
   
 3. kui

  kui JF-Expert Member

  #3
  Oct 19, 2009
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 6,478
  Likes Received: 5,146
  Trophy Points: 280
  Not fair
   
 4. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #4
  Oct 19, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  haya mambo tutayaona sana, je na sisi baba zetu wasio na title nchini mtetezi wetu ni nani au ndo tutaendelea kutawaliwa na hawa wanaorithishwa? kazi kweli kweli
   
 5. J

  JokaKuu Platinum Member

  #5
  Oct 19, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,794
  Likes Received: 5,065
  Trophy Points: 280
  ..damu nzito kuliko maji.
   
 6. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #6
  Oct 19, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mzee Makamba hana jipya wala sera. Sijui kizazi chake kitakuwaje?

  Anaepitishwa na mwizi nae lazima atakuwa mwizi.......
   
 7. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #7
  Oct 19, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  dah kweli akina sie tutaendelea kubaki hivi hivi
   
 8. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #8
  Oct 19, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  Hata Makamba nae.......Mmh
   
 9. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #9
  Oct 19, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  let him do what he wants to do, akipenda hata aseme awe mgombea binafsi na amuwekee hela kumpigia campaign huyo jamaa, kumpigia kura ndio utakuwa upunguani wenyewe. Si yeye tu bali robo tatu ya wabunge wanaolipwa milioni saba kwa mwezi na amna lolote wanaolifanya.

  Its time to get rid of useless politicians OK Lowassa anatusumbua lakini kuna mijitu mingine tunaweza kuitoa kwa kutoichagua tena if only upinzani ungejifunza kuwa chama kimoja.
   
 10. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #10
  Oct 19, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Wanataka waendeleze libeneke la kulindana..................tu
   
 11. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #11
  Oct 19, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,482
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Kumbe walitakaje? ampigie debe mtoto wa Burn ambaye hamjui? nadhani hoja ingekuwa iwapo January Makamba anauwezo kuwa mbunge.
   
 12. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #12
  Oct 19, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  If he is that intelligent as the hype sorrounding him. he needs to prove his ability instead of letting daddy do the talking. We need intelligence at this moment in time, but prove your self. This is why i take my hat off to Zitto he is not scared of criticism and never shy away to defend himself.
   
 13. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #13
  Oct 19, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,482
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  you need to go and tell that to mzee kabwe in Mets Kigoma cause he is doing exactly the same thing mzee makamba is doing for January. my problem is i cant find anywhere where its written parents shoulnt support their children in whatever they are doing.
   
 14. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #14
  Oct 19, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  To what extent is a parent supposed to call the shots for his son. He/they need to prove their worthiness to us. Or else this is just a fisadi method of inheriting positions in our democracy. Therefore if voters have any intelligence we do not need this sort of cultural.

  It has stop before it takes off. Look at Zitto for instance he is not perfect, but not a coward like this fools who cower behind dads' backs.
   
 15. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #15
  Oct 19, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  tunayo nafasi badoo ni kujiamini na kuaminii mabadilikoo yanawezekanaa..

  Obama ameonyeshaa njiaa..
   
 16. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #16
  Oct 19, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,482
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  For your information, January doesnt need his dad's back on this, he can easily grab the constituency with his own influence. I think mzee Makamba is just being a parent, something that everyone would have done. Do you have anything against tyhis family?
   
 17. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #17
  Oct 19, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  No Sir. i have nothing against nobody. Matter of fact i like the young to take over, according to the post the dad is doing all the work. It appears to be the case, January doesnt say anything.

  If you ask me he is a tricky customer, what are his views on anything, he is going to run with a CCM ticket if anything we know what they represent. My argument are we breeding a future Fisadi or a politicians.

  the difference between the two is, one is just happy to receive and enjoy life (ridhwani) and the other receives but questions (Zitto), so where is January going to stand.
   
 18. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #18
  Oct 19, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,482
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  unfortunately i dont know him (January) personally to answer your question but in any case for his dad to stand on his side i dont see anything wrong. Good that you dont have anything against their family but i smell prejudice on ''watoto wa vigogo''
   
 19. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #19
  Oct 19, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,661
  Likes Received: 1,496
  Trophy Points: 280

  FL ulitaka kugombea? kwa move hii mbona tuliitegemea? kwa mtu kama yeye..sio kitu cha ajabu kabisa na anaona kawaida kabisa!
   
 20. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #20
  Oct 19, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,402
  Likes Received: 685
  Trophy Points: 280
  It will be fair like it or not!!!
   
Loading...