Makamanda wamdindia Lowassa. Wasema kama amechoka CHADEMA arudi alikotoka

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,375
Wadau, amani iwe kwenu.

Hivi sasa Ufipa kunafukuta. Moto unawaka chini kwa chini na mpaka sasa makamanda wamegawanyika baina ya pande mbili. Kuna CHADEMA Siasa na CHADEMA Uanaharakati. Hali hii imejitokeza baada ya Lowasa kutamka kuwa CHADEMA sasa imegraduate kutoka Uanaharakati na kuwa chama cha siasa.

Tangu jana, baadhi ya makamanda wamenukuliwa wakisema kuwa CHADEMA kina misingi yake na hakiwezi kwenda kinyume na misingi ambayo imekifanya chama hicho kuwa imara eti kutokana na utashi wa mtu mmoja.

Wengine wamesikika wakisema kuwa ni kwa sababu ya siasa ya maandamano ndiyo iliyomvuta Lowasa kwenda CHADEMA na si ACT chama alichokiasisi kwa kushirikiana na Zitto Kabwe. Hivyo Uanaharakati ndio nguzo kuu ya siasa za CDM. Mwingine kwa utani anamuuliza Lowasa. "Inawezekana vipi mwanamke umempata ukiwa Bar umkataze asiende huko?"

Wengine wanasema kuwa Lowasa hana mamlaka ya kutoa kauli kama hiyo kwa vile yeye ni mwanachama tu na mjumbe wa Kamati Kuu. Kwamba, CHADEMA haijawahi kukaa kikao na kutathmini hali yake na kutoa hitimisho kuwa imegraduate kutoka uanaharakati na kuwa chama cha siasa. Wanasema kuwa hayo ni mawazo yao. Kwamba CHADEMA kina utaratibu wake wa kutoa kauli. Wanashangaa kumuona Lowasa akijipa cheo cha Mwenyekiti, Msemaji na mwenye chama vyeo ambavyo si vyake.

Mwingine alisikika akisema kuwa kama CHADEMA kilikuwa ni chama cha kiharakati kwa siku zote, wamewezaje kupata wabunge, madiwani na kuongoza halmashauri kadhaa? Ina maana wao si wanasiasa bali ni wanaharakati?

Mwingine amesikika pia akisema kuwa Lowasa anahatarisha usalama wa chama chao. Kwamba kauli hiyo inahalalisha vitendo vya jeshi la polisi kuwazuia, kuwakamata na kuwafungulia mashtaka makamanda. Kwamba, "kama CHADEMA tulikuwa tunafanya uanaharakati na si siasa, basi jeshi la polisi lilikuwa na lipo sahihi kutukamata na inapaswa sasa CHADEMA tuliombe radhi jeshi hilo na taifa kwa ujumla kwa usumbufu, uharibifu na hata vifo vilivyotokea wakati wa uanaharakati wetu". Alisikika kamanda mmoja.

Mwingine alisikika akiuliza, je Lowasa ametumwa na nani kutamka hayo? Au haridhishwi na matamko ya makamanda kuwa wataenda Dodoma kwenda kuzuia mkutano wa CCM?

Kamanda mwingine anamuona Lowasa ni mkurupukaji na kwamba anajiona kuwa yeye tu yupo sahihi na wengine wafuate maneno yake. Alihoji. Hivi si huyu huyu tu Lowasa aliyesema kuwa ameporwa ushindi? Si huyu huyu tu Lowasa aliyesema kuwa hatakubali matokeo mpaka anaingia kaburini?

Mwingine amemtaka Mbowe na CHADEMA kwa ujumla kumdhibiti Lowasa kwani asipodhibitiwa sasa, atasumbua sana wakati wa uchaguzi wa chama hicho mwaka 2018.

Wadau, hizi ni baadhi ya kauli zilizotolewa na makamanda kwa nyakati tofauti. Majina yao nayafahamu ila siwezi kuyadisclose humu kwa kulinda hadhi ya JF na kuwalindia heshima zao vinginevyo moto utawaka zaidi kwani waliosema ni makamanda wazito na wenye vyeo vikubwa chamani.
 
Hakuna anayehangaika na huo mzoga wenu. Nawahurumia sana.
......,,,,,,,,,,, Mwingine amemtaka Mbowe na CHADEMA
kwa ujumla kumdhibiti Lowasa kwani
asipodhibitiwa sasa, atasumbua sana
wakati wa uchaguzi wa chama hicho
mwaka 2018......,thubutu!!!! kuna mwanachadema aweza kumthibiti lowassa!!!?????CCM wenyewe na Mwalimu Nyerere alikuwa anawatoa majasho!!!!
 
tunajua umesomea propaganda ya disinformation.piga kazi upate siku lakini hutafanikiwa malengo yako. hatudanganyiki!!!
 
Back
Top Bottom