Makamanda wakati mzuri wa kudai ahadi za CCM ni 2020

kipara kipya

JF-Expert Member
May 2, 2016
14,076
15,922
Inachekesha baada ya makamanda kukosa cha kuongea sasa wamehamia kudai ahadi za CCM zilizoahidiwa na Magufuli.
Wamekwenda mbali sasa wanasheherekea eti benki iliokua imeahidi kuikopesha serikali imejitoa.

Makamanda mbona mapema miradi ni mingi ni matumaini ipo itakayokamilika ndani ya miaka mitano ya mwanzo na kuna itakayomaliziwa awamu ya pili na kama haitokamilika Rais ajaye kwa tiketi ya CCM ataikamilisha,makamanda mbona mna hofu na ndio kwanza miaka miwili au mlimuhujumu lowassa kwa kumpa kura kwa siri magufuli baada ya zile push up.

Makamanda mambo mazuri hayataki haraka kiwanja cha ndege chato,shirika la ndege,barabara za juu,mradi mkubwa wa umeme,reli ya kisasa,tatizo la maji kitila mkumbo analishughulikia kama si kufanya historia,umeme kila kaya vijijini,elimu bure,afya na mengi mengineyo

Swali muhimu kwenu makamanda na mwenye ubavu wa kusimama na magufuli!
 
Back
Top Bottom