Makamanda Wa Polisi Wazawadiwa Gari Na Wafanyabiashara

Mongoiwe

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
524
263
KWA mara ya kwanza katika historia ya sherehe za kuagwa kwa maofisa wa polisi nchini, makamanda wa polisi mkoa wa Mbeya na Mwanza wamezawadiwa gari kila mmoja.

Ingawa jambo hili linaweza kuonekana ni la kawaida kwa makanda hao kuzawadiwa gari, lakini katika mtazamo wa maadili ya viongozi wa umma, magari haya yanaweza kufikirika kuwa ni moja kati ya RUSHWA ambazo viongozi wetu wamezoea kupewa.

Makamanda hao ni Steven Zelothe aliyehamishiwa mkoani Mbeya toka mkoani Mwanza na anayechukua nafasi yake Jamal Rwambow aliyehamia kutoka mkoa maalum wa kipolisi wa Kinondoni Dar es salaam pamoja na kupokea zawadi hiyo ya gari pia walipokea zawadi nyingine kama kompyuta, mifugo, nguo, nafaka na vyombo mbalimbali.

Sherehe ya kumuaga kamanda Zelothe na kumkaribisha Rwambow zilifanyika katika ukumbi wa Yatch Club na kuhuduriwa na mkuu wa mkoa wa Mwanza Dr. Alex James Msekela, katibu tawala mkoa Alhaji Yahaya Mbilla viongozi wa ngazi mbalimbali za mkoa chama na serikali ikiwa ni pamoja na wafanyabiashara.

Katika sherehe hizo mara baada ya kuanza utaratibu wa utoaji zawadi, na kuzawadiwa zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kompyuta ndogo (Lap top) zilizotolewa na maofisa wa ofisi yake waliokuwa wakifanya nae kazi.

Zawadi nyingie ni pamoja na ng’ombe wawili toka ofisi ya mkuu wa mkoa, magunuia mawili ya nafaka friji dogo majiko ya ovena na vitenge na vitambaa kwa ajili ya mavazi yeye pamoja na mkewe.

Lakini zawadi iliyotia fora ilikuwa ni zawadi ilitotangazwa na mwenyekiti wa kamati ya sherehe hiyo Augustino Uromi ambaye pia ni afisa upelelezi (RCO) wa jeshi hilo mkoani Mwanza.

Akitangaza kutoa zawadi hiyo ya kamati, RCO Uromi alisema kuwa kamati yake imeamua kuwazawadia gari makamanda hao kila mmoja na kuwakabizi kadi za kuwatakia heri huku akieleza kwamba ndani yake kulikuwa na maelekezo ya magari hayo bila ya kutaja thamani ya magari hayo.

Magari hayo ni aina ya Toyota salon (Namba zake tunazo), alilozawadiwa kamanda Zelothe ndilo ambalo mkewe alikuwa akilitumia mkewe katika mizunguko mara baada ya kuwasili kutokea jijini Mbeya kwa ajili ya sherehe za kuagwa.

Kutolewa kwa zawadi hiyo kulizua minong’ono mingi huku baadhi ya wageni waalikwa kushindwa kuamini macho yao baadhi wakidhani ilikuwa ni mbwembwe za msemaji wa kamati lakini baada ya gazeti hili kufuatilia kwa kina ilithibitika kweli.

“Tumetoa kwa mapenzi yetu, tulimpenda sana kamanda, lakini tumeamua kuwapatia wote kuonyesha hatuna ubaguzi” alieleza Kitano Chacha mmoja wa wafanyabiashara ambaye alikuwa mjumbe wa kamati hiyo ya sherehe wakati alipokuwa akiongea na mwandishi wetu.

Hata hivyo kulingana na sheria ya maadili ya viongozi wa umma ya mwaka 1995, kifungu cha 12 kifungu kidogo (2), kinaeleza kuwa iwapo kiongozi wa umma atapokea zawadi yenye thamani inayozidi sh. 50,000 (kama ilivyo magari hayo) atatakiwa kutaja zawadi hiyo pamoja na thamani yake na kukabidhiwa zawadi hiyo kwa afisa mhasibu wa ofisi husika inayohisika, ambaye atatoa maagizo kwa maandishi kuhusu matumizi ya zawadi hiyo au jinsi ya kuishughulikia kwa njia nyingie yoyote.

Aidha habari kutoka ndani ya kamati hiyo zimedai kuwa zawadi hizo za magari zimetolewa na mfanyabiashara mmoja wa samaki Jijini Mwanza (jina lake limehifadhiwa kwa sasa) na kutolewa kwa kamati hiyo kwa ajili kuwakabidhi makamanda hao.
 
Gazeti lipi si utaje?Taja pia na hizo number ili tukiona haya magari tuyapige mawe kwa sababu kuna uwalakini katika utoaji wake maana Mbongo hatoi kitu bure kuna something behind the curtain.Wamefanya kazi gani kupewa hizo zawadi?Mimi ninaposhindwa kuelewa ni pale bosi ambaye kazi yake ni kukaa ofisini tu na ku issue orders anapewa zawadi without doing anything na wale maofisa wadogo ambao ndio watekelezaji wakuu wanabaki palepale wapanda daladala na wala hawapewi chochote.
 
KWA mara ya kwanza katika historia ya sherehe za kuagwa kwa maofisa wa polisi nchini, makamanda wa polisi mkoa wa Mbeya na Mwanza wamezawadiwa gari kila mmoja.

Ingawa jambo hili linaweza kuonekana ni la kawaida kwa makanda hao kuzawadiwa gari, lakini katika mtazamo wa maadili ya viongozi wa umma, magari haya yanaweza kufikirika kuwa ni moja kati ya RUSHWA ambazo viongozi wetu wamezoea kupewa.

Makamanda hao ni Steven Zelothe aliyehamishiwa mkoani Mbeya toka mkoani Mwanza na anayechukua nafasi yake Jamal Rwambow aliyehamia kutoka mkoa maalum wa kipolisi wa Kinondoni Dar es salaam pamoja na kupokea zawadi hiyo ya gari pia walipokea zawadi nyingine kama kompyuta, mifugo, nguo, nafaka na vyombo mbalimbali.

Sherehe ya kumuaga kamanda Zelothe na kumkaribisha Rwambow zilifanyika katika ukumbi wa Yatch Club na kuhuduriwa na mkuu wa mkoa wa Mwanza Dr. Alex James Msekela, katibu tawala mkoa Alhaji Yahaya Mbilla viongozi wa ngazi mbalimbali za mkoa chama na serikali ikiwa ni pamoja na wafanyabiashara.

Katika sherehe hizo mara baada ya kuanza utaratibu wa utoaji zawadi, na kuzawadiwa zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kompyuta ndogo (Lap top) zilizotolewa na maofisa wa ofisi yake waliokuwa wakifanya nae kazi.

Zawadi nyingie ni pamoja na ng’ombe wawili toka ofisi ya mkuu wa mkoa, magunuia mawili ya nafaka friji dogo majiko ya ovena na vitenge na vitambaa kwa ajili ya mavazi yeye pamoja na mkewe.

Lakini zawadi iliyotia fora ilikuwa ni zawadi ilitotangazwa na mwenyekiti wa kamati ya sherehe hiyo Augustino Uromi ambaye pia ni afisa upelelezi (RCO) wa jeshi hilo mkoani Mwanza.

Akitangaza kutoa zawadi hiyo ya kamati, RCO Uromi alisema kuwa kamati yake imeamua kuwazawadia gari makamanda hao kila mmoja na kuwakabizi kadi za kuwatakia heri huku akieleza kwamba ndani yake kulikuwa na maelekezo ya magari hayo bila ya kutaja thamani ya magari hayo.

Magari hayo ni aina ya Toyota salon (Namba zake tunazo), alilozawadiwa kamanda Zelothe ndilo ambalo mkewe alikuwa akilitumia mkewe katika mizunguko mara baada ya kuwasili kutokea jijini Mbeya kwa ajili ya sherehe za kuagwa.

Kutolewa kwa zawadi hiyo kulizua minong’ono mingi huku baadhi ya wageni waalikwa kushindwa kuamini macho yao baadhi wakidhani ilikuwa ni mbwembwe za msemaji wa kamati lakini baada ya gazeti hili kufuatilia kwa kina ilithibitika kweli.

“Tumetoa kwa mapenzi yetu, tulimpenda sana kamanda, lakini tumeamua kuwapatia wote kuonyesha hatuna ubaguzi” alieleza Kitano Chacha mmoja wa wafanyabiashara ambaye alikuwa mjumbe wa kamati hiyo ya sherehe wakati alipokuwa akiongea na mwandishi wetu.

Hata hivyo kulingana na sheria ya maadili ya viongozi wa umma ya mwaka 1995, kifungu cha 12 kifungu kidogo (2), kinaeleza kuwa iwapo kiongozi wa umma atapokea zawadi yenye thamani inayozidi sh. 50,000 (kama ilivyo magari hayo) atatakiwa kutaja zawadi hiyo pamoja na thamani yake na kukabidhiwa zawadi hiyo kwa afisa mhasibu wa ofisi husika inayohisika, ambaye atatoa maagizo kwa maandishi kuhusu matumizi ya zawadi hiyo au jinsi ya kuishughulikia kwa njia nyingie yoyote.

Aidha habari kutoka ndani ya kamati hiyo zimedai kuwa zawadi hizo za magari zimetolewa na mfanyabiashara mmoja wa samaki Jijini Mwanza (jina lake limehifadhiwa kwa sasa) na kutolewa kwa kamati hiyo kwa ajili kuwakabidhi makamanda hao.
..

Toyota salon??????? Corola, Corona, Mark II, Chaser, Caldina, Cresta, Vista??????????????? weka na namba zake za usajiri wa hayo magari hapa...
 
Maswali ni mengi ya kumuuliaza na hata haonekani kuyajibu.
 
Back
Top Bottom