Makamanda wa polisi wa mikoa nao wanashindwa kutafsiri maana ya 'central police station'?

Salange

JF-Expert Member
Jul 28, 2018
683
1,000
Ni kawaida kuwasikia watanzania wengi wakisema ' kituo cha kati' cha polisi kwa maana ya ' central police station' badala ya kusema ' kituo kikuu cha polisi'. Hata kituo kikiwa pembeni ya mji tunasema kituo cha kati! Tumezoea hivyo na kwa kweli tunadhani ndiyo usahihi wenyewe.

Kioja ni pale hata polisi wenyewe, wa kawaida na ma RPC wao, nao wamekazana tu kusema 'kituo cha kati' badala ya kituo kikuu cha polisi !! Ni makusudi au nao hawaelewi?

Kama hawaelewi, basi tuna shida. Ikiwa wenye fani wenyewe hawaelewi tafsiri sahihi ya central kwa muktadha huu, nani atatuelekeza ili upotoshwaji huu ufike mahali sasa uishe badala ya kuendelezwa mpaka kwa wajukuu na vilembwe wetu? Kwa nini tusiwe makini na weledi wa mambo ya kawaida kabisa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom