Makamanda wa CHADEMA watikisa Mji wa Moshi

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
SIASA






chademaarusha.jpg

Katibu wa Chadema Mkoa wa Kagera, Conchesta Rwamlaza, ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu kupitia chama hicho, akihutubia wakazi wa Bukoba, mkutano uliofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa jana. Picha na Mpiga Picha Wetu



Na Daniel Mjema

Posted Jumatatu,Novemba26 2012 saa 8:31 AM


KWA UFUPI


"Maisha wakati wa Rais Ali Hassan Mwinyi (1985-1995) na Benjamin Mkapa (1995-2005), yalikuwa mazuri kuliko ya Rais wa sasa Jakaya Kikwete, hakuna sababu ya kuendelea na CCM,"alisema.






MAKAMANDA wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutoka Jiji la Arusha, juzi walitikisa mji wa Moshi huku wakitaka wananchi kujiandaa kuchukua nchi kwa njia ya kura 2015.
Katika mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Aslam Gereji, Kata ya Mawenzi, makamanda hao pia walitaka wananchi kuishinikiza Serikali, ili irejeshe mabilioni ya shilingi yaliyofichwa Uswisi.


Chiristopher Mbajo anayetarajiwa kugombea Ubunge Same Magharibi mwaka 2015, alihoji uhalali wa vyombo vya dola vya Tanzania, kuwabebesha wananchi jukumu la vigogo walioficha fedha Uswisi.

"Jukumu la kumchunguza mwananchi wa kawaida au kiongozi ni la vyombo vya dola lakini leo Zitto (Kabwe-Mbunge Kigoma Kaskazini) anatakiwa eti apeleke majina hii ni aibu,"alisema Mbajo.
Wakili wa Jijini Arusha, James Lyatuu alisema ugumu wa maisha unaowakabili Watanzania hivi sasa kuliko awamu zote za Serikali ya CCM zilizotangulia, ndio silaha ya kuking'oa chama hicho katika uchaguzi wa mwaka 2015.


"Maisha wakati wa Rais Ali Hassan Mwinyi (1985-1995) na Benjamin Mkapa (1995-2005), yalikuwa mazuri kuliko ya Rais wa sasa Jakaya Kikwete, hakuna sababu ya kuendelea na CCM,"alisema.
Wakili huyo aliwataka wakazi wa Moshi, kusimama imara kudai haki yao ya kikatiba ya maisha bora na wale watakaopata misukosuko kwa kutetea haki yao, yuko tayari kuwatetea bure mahakamani.
Katibu Mwenezi wa Chadema katika Kata ya Sekei jijini Arusha, Bahati David alisema CCM ni wepesi kama pamba na kwamba chama hicho kijiandae kuwa chama cha upinzani katika uchaguzi mkuu wa 2015.


Kwa upande wake,Diwani wa Viti Maalumu katika Manispaa ya Moshi, Hawa Mushi (Chadema), aliitaka CCM kujiandaa kukabidhi madaraka kwa Chadema kwa amani ifikapo mwaka 2015.
Diwani huyo ambaye ndiye aliyeandaa mkutano huo wa hadhara, alisema mafanikio ambayo Chadema Moshi imeyapata katika kipindi kifupi ni kielelezo cha umakini katika kusimamia maslahi ya umma.


Mwenyekiti wa zamani wa Umoja wa Vijana wa CCM (Uvccm) Wilaya ya Simanjiro, Frank Ole Lelesho, alisema uendeshaji bora wa mji wa Moshi ni kielelezo cha umakini wa viongozi wa Chadema.

Kwa mujibu wa Ole Lelesho, wapo watoto waliozaliwa katika wilaya ya Simanjiro hadi wakamaliza kidato cha nne lakini hawajawahi kuona lami lakini mji wa Moshi una lami hadi pembezoni.

 
Vizuri sana kwa VIJANA tungoje tuone wa Umoja wa VIJANA wa CCM; Wasigawe T-SHIRTS; KHANG; KOFIA Pesa za MAFUTA ya MALORI n.k
 
Hongereni sana pia jengeni chama vijijin bado uwezakano wakuendelea kushika dola kwa ccm ni mkubwa nawatakia kazi njema
 
Chadema wanatakiwa kuongeza bidii maana siyo majimbo mengi yaliyo na msimamo thabiti kama jimbo la Moshi.
Lile ni jimbo lililoelimika kisiasa. Wasilizembee na pia wasisahau kazi ngumu waliyonayo mbele yao ya kuwaelimisha na kuwaamsha wananchi kwenye majimbo mengine mengi sana nchini.
 
MOshi imeiva ila inahitaji watu wakufuatilia na kuwatia moyo makamanda hasa vijijini kwani wote wamekata tamaa na stystem mbovu iliyopo
KAZI NZURI HONGERENI MSIBWETEKE
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom