Makamanda wa CDM waunguruma saizi Maji ya Chai - Kijiji cha Kitefu

Mzee wa Rula

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
8,171
3,346
Katika kuhakikisha wanautumia muda uliobakia ipasavyo, makamanda wa CDM wakiongozwa na Vicent Nyerere, Mchungaji Msigwa na madiwani baadhi kutoka Moshi saizi wapo kijiji cha Kitefu - Maji ya Chai kuwasihi wananchi siku ya Jumapili tarehe 01.04 hawafanyi makosa zaidi ya kumchagua Joshua Nassari.

Picha zitawekwa baadae wakuu, hivyo mvute subira.
 
Pamoja sana mkuu.Tupe Live bila chenga
 
PICHA HIZI HAPA

jamani

564324_320322561365066_100001619734978_888709_301333869_n.jpg

Nimetapika ugali wangu wa mchana
 
Updates:
1.0 Mjumbe mmoja wa CCM kwa moja la Peter ambaye ni mwakilishi wa katika vikao vya kata katika wilaya na mkoa amerudisha kadi na kuchukua ya CDM.
2.0 Msigwa;
Mchungaji Msigwa amewaasa wananchi wasidanganye kuwa kuchagua upinzani eti ni kutochagua maendeleo. Ameponda hilo kwa kutoa mifano ya Moshi ambapo kila sehemu ni lami, Karatu karibu kata zoe zina shule ya msingi na saizi mkakati ni sekondari, maji Karatu mabomba yanakaribia kupasuka maana yapo ya kutosha, Iringa ndiyo usiseme JK mwenyewe kaenda juzi kuzindua mradi wa mabilioni ya fedha.

Hivyo amewataka kutosita kumchagua kijana shupavu, mjasiri na mwenye kuweza kujenga hoja bila woga na ikaeleweka.

3.0 Vicent Nyerere.

Yeye amekumbusha wananchi kuwa katika kila kitu wanachotumia kina kodi, hivyo ni jukumu lao kuhakikisha wananchagua kijana mahiri akasimamie kodi zao maana amefananisha CCM na mapanya hivyo yanahitaji Mapaka ya kulinda ufujaji wa fedha ambazo zinatokana na kodi ambayo kila kukicha wanalipa.

Paka hilo ni Joshua Nassari na siyo mwingine, hivyo wampe kura za ndiyo maana hata hapana nayo ni kura.

Aidha Nyerere amewaambia CCM baada ya miaka kumi itakuwa haipo maana wale ambao wanaisuport ni wazee, hivyo wasijihangashe kupiga kura kwa chama ambacho kimefika ukomo wake.

Kwa ujumla mkutano ulikuwa umehudhuriawa na watu wa marika yote na wazee, akina mama ambao ni nguzo kuu ya CCM. Na wao kwa kauli moja hasa wazee na kina mama wameazimia safari hii hawadanganyiki.
Mkutano umekwisha tayari.

Saizi Nassari ndiyo anaongea, kifupi anaongelea masuala mazito kabisa. Ameanza na suala la ardhi ya wameru ambayo ni kama imegaiwa bure kwa hao walowezi ambao tayari wameshaanza kutetewa na CCM kupitia waziri wa ardhi ambaye yupo Arumeru.

Hakuishia hapo akasema anasema anashangaa kwa nini mpaka leo hii Kitefu haina maji lakini Monduli yapo na maji yanatoka Meru? Anawauliza wanaArumeru kama ni sawa hiyo? Wanajibu si sawa kabisa.

jamani ndo hizo picha au zimechakachuliwa?

Kama kawaida dhambi ya kuchakachua ukishaianza hauiachi, hiyo ilikuwa Igunga mkuu lakini ili kuchafua hali ya hewa jamaa kaamua kuiweka makusudi.

Ni kama Mwigulu alivyozooea kuchakachua wake za makada wenzake lakini huku jasho linamtoka labda aende mitaa fulaani hapa kwetu.
 
Nipe update leo nipo Ngarenanyuki naona Professor Kahigi na Mama yetu Rose kamili Anatelemsha Nondo za kufa mtu,kweli CHADEMA balaa

Vipi huko Ngarenanyuki hali ikoje mkuu? Huku kama ulivyojulishwa picha baadae lakini ni funiko bovu kabisa. Jamaa wanatema cheche balaa.
 
Saizi Nassari ndiyo anaongea, kifupi anaongelea masuala mazito kabisa. Ameanza na suala la ardhi ya wameru ambayo ni kama imegaiwa bure kwa hao walowezi ambao tayari wameshaanza kutetewa na CCM kupitia waziri wa ardhi ambaye yupo Arumeru.

Hakuishia hapo akasema anasema anashangaa kwa nini mpaka leo hii Kitefu haina maji lakini Monduli yapo na maji yanatoka Meru? Anawauliza wanaArumeru kama ni sawa hiyo? Wanajibu si sawa kabisa.
haya ndiyo maneno ya maana mtu wangu,
japo nipo mbali, najihisi kama nipo eneo la tukio,
endeleeni kutujuza, tupo pamoja wakuu,
 
Kweli nimeamini pilau za ccm za miaka hamsini na kila baada ya miaka mitano au chaguzi ndogozinapojitokeza hazina kazi tena kwa watz....
Naamini watatumia uhuru wao baada ya miaka 50 ya uhuru.
 
Kweli nimeamini pilau za ccm za miaka hamsini na kila baada ya miaka mitano au chaguzi ndogozinapojitokeza hazina kazi tena kwa watz....Naamini watatumia uhuru wao baada ya miaka 50 ya uhuru.[/QUOTETatizo ni kwamba ccm hawaheshimu tena uhuru wa watanzania wako tayari watu wafe lakini wao watawale halafu waseme wapinzani ndio wenye fujo. Lakini wakumbuke kuwa mjinga akielewa mwerevu yu mashakani. Itafikia hatua watanzania watakataa kupiga kura kwa siri bali kumchagua wampendae kwa kunyoosha mikono
 
Tatizo ni kuwa ccm hawaheshimu tena maoni wala uhuru wa watu hasa baada ya kuona wameshindwa kutatua kero za wananchi baada ya miaka 50 ya uhuru. Lakini wakumbuke kuwa mjinga akierevuka mjanja yu mashakani. Watanzania wa leo co wale w 1977. Wasishangae siku moja watz wanakataa kumchagua mtu kwa kura ya siri bali wakaamua kunyoosha mikono ili uwe ndo uchaguzi kw mgombea wanayemtaka. Ikishindikana hapo nguvu ya umma yaweza kutumika.

Kweli nimeamini pilau za ccm za miaka hamsini na kila baada ya miaka mitano au chaguzi ndogozinapojitokeza hazina kazi tena kwa watz....Naamini watatumia uhuru wao baada ya miaka 50 ya uhuru.
 
Mkuu!!!!!

Bila shaka hawa mafisadi hatima yao imetimia.Hila na njama yao hakika tunao mifukoni mwetu.

Pamoja Mkuu wangu!!!!!!!!!!!!!!!
 
Updates:
1.0 Mjumbe mmoja wa CCM kwa moja la Peter ambaye ni mwakilishi wa katika vikao vya kata katika wilaya na mkoa amerudisha kadi na kuchukua ya CDM.
2.0 Msigwa;
Mchungaji Msigwa amewaasa wananchi wasidanganye kuwa kuchagua upinzani eti ni kutochagua maendeleo. Ameponda hilo kwa kutoa mifano ya Moshi ambapo kila sehemu ni lami,
Karatu karibu kata zoe zina shule ya msingi na saizi mkakati ni sekondari, maji Karatu mabomba yanakaribia kupasuka maana yapo ya kutosha, Iringa ndiyo usiseme JK mwenyewe kaenda juzi kuzindua mradi wa mabilioni ya fedha.

Hivyo amewataka kutosita kumchagua kijana shupavu, mjasiri na mwenye kuweza kujenga hoja bila woga na ikaeleweka.

3.0 Vicent Nyerere.

Yeye amekumbusha wananchi kuwa katika kila kitu wanachotumia kina kodi, hivyo ni jukumu lao kuhakikisha wananchagua kijana mahiri akasimamie kodi zao maana amefananisha CCM na mapanya hivyo yanahitaji Mapaka ya kulinda ufujaji wa fedha ambazo zinatokana na kodi ambayo kila kukicha wanalipa.

Paka hilo ni Joshua Nassari na siyo mwingine, hivyo wampe kura za ndiyo maana hata hapana nayo ni kura.

Aidha Nyerere amewaambia CCM baada ya miaka kumi itakuwa haipo maana wale ambao wanaisuport ni wazee, hivyo wasijihangashe kupiga kura kwa chama ambacho kimefika ukomo wake.

Kwa ujumla mkutano ulikuwa umehudhuriawa na watu wa marika yote na wazee, akina mama ambao ni nguzo kuu ya CCM. Na wao kwa kauli moja hasa wazee na kina mama wameazimia safari hii hawadanganyiki.
Mkutano umekwisha tayari.

Saizi Nassari ndiyo anaongea, kifupi anaongelea masuala mazito kabisa. Ameanza na suala la ardhi ya wameru ambayo ni kama imegaiwa bure kwa hao walowezi ambao tayari wameshaanza kutetewa na CCM kupitia waziri wa ardhi ambaye yupo Arumeru.

Hakuishia hapo akasema anasema anashangaa kwa nini mpaka leo hii Kitefu haina maji lakini Monduli yapo na maji yanatoka Meru? Anawauliza wanaArumeru kama ni sawa hiyo? Wanajibu si sawa kabisa.

Sahihisho kwenye Bold.
Karatu imekuwa upinzani tokea mfumo wa vyama vingi
Karatu kila kijiji na vitongoji kuna shule za msingi
Karatu kila Kata kuna shule za secondary
Karatu sasahivi wanajenga chuo kikuu cha karatu. haya si maneno yangu kishabiki, bali ndiyo ukweli uliopo karatu

Ukichagua CHADEMA umechagua MAENDELEO
 
Back
Top Bottom