Makalla ukitaka kuisafisha Dar es salaam anzisha Operesheni " Nguvu Kazi" kama ile ya RC Mhaville

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,614
141,437
Kuwaondoa wamachinga kwa utaratibu wa sasa hakuwezi kuisafisha Dar es salaam kwa sababu machinga hawataondoka.

Ni heri upekue mafaili hapo ofisini kwako ukilipata lile la " Operesheni Nguvu Kazi" wakati wa RC John Mhaville lisome taratibu linaweza kuwa la msaada kwako.

Nawatakia Sabato yenye baraka!
 
Nguvu kazi ukiwakamata uwapeleke wapi?
Au ndiyo unaenda kuwatupa porini

Ova
 
Wanawekwa kwenye vikundi wapelekwe kulima hata bustani na matunda, wapelekwe kisarawe, kibiti,
Uko wanapopelekwa watakuwa washaandaliwa miundu mbinu!!
Au wnapelekwa porini,wanaoneshwa pori hilo
Haya anzeni maishaaa

Ova
 
Wanawekwa kwenye vikundi wapelekwe kulima hata bustani na matunda, wapelekwe kisarawe, kibiti,
Endelea kujitekenya. Hayo matunda toka Tanga yanakosa soko mpaka yanaoza. Unadhani fursa hizo katika kilimo hawajaziona. Au hawajawaona wazazi wao wamepinda migongo bila tija toka kwenye hicho kilimo unachodai. Wanakijua kifo hawahitaji kuangalia kaburi.
 
Huyu jamaa ovyo tu kama wengine wengi ..aliunda timu kufatilia wizi wa mafuta kwenye pampu za bandarini hadi leo hatujawahi kuambiwa ni nani alikuwa mwizi. Ndo maana daima ntamuenzi jpm make ishu kama hizi alimtumbua Makala na leo angeshampasua tena ili akalime maboga, hopeless Makalla.
 
Makalla ni hakuna kitu hana lolote alirudishwa ilikuwanyanyasa wamachinga hana lolote

Anerudishe ili akina ridhiwani waendelee kutolipa kodi

Makala amekuja kuifanya dar es salaam ichukiwe na ccm nadhani kuna jambo linatafutwa huko

Huwezi kuwapora vitu vyao hii sio nzuri sana
 
Uko sahihi sana Logic Mentality, katika dunia iliyostaarabika na ya wastaarabu kwenda mahala usiku watu wamelala na kuanza kuvunja ni uvamizi na uporaji. Haina tofauti na wezi wale wa kwa madiba wanaovamiaga maduka usiku na kufanya uharifu, Makalla anatakiwa kushtakiwa haraka sana iwezekanavyo.
 
Kuwaondoa wamachinga kwa utaratibu wa sasa hakuwezi kuisafisha Dar es salaam kwa sababu machinga hawataondoka.

Ni heri upekue mafaili hapo ofisini kwako ukilipata lile la " Operesheni Nguvu Kazi" wakati wa RC John Mhaville lisome taratibu linaweza kuwa la msaada kwako.

Nawatakia Sabato yenye baraka!
Bomu la MACHINGA ni CCM ililitega YENYEWE Wacha wahangaike Nao
Na HALITEGUKI kama wanavyodhani
 
Kwa sasa ni vigumu,wamachinga wanaongezeka kila kukicha.Sababu kuu ni ukosefu wa ajira rasmi, viwanda vikubwa vya kubangua korosho,viwanda vya kuchakata mazao ya pamba vilivyojengwa na Mwl.Nyerere Nyerere enzi hizo kama sio kuuzwa,na kuhujumiwa tusinge kuwa na tatizo la machinga.
 
Huyu jamaa ovyo tu kama wengine wengi ..aliunda timu kufatilia wizi wa mafuta kwenye pampu za bandarini hadi leo hatujawahi kuambiwa ni nani alikuwa mwizi. Ndo maana daima ntamuenzi jpm make ishu kama hizi alimtumbua Makala na leo angeshampasua tena ili akalime maboga, hopeless Makalla.
Eti akalime mabega
 
Kuwaondoa wamachinga kwa utaratibu wa sasa hakuwezi kuisafisha Dar es salaam kwa sababu machinga hawataondoka.

Ni heri upekue mafaili hapo ofisini kwako ukilipata lile la " Operesheni Nguvu Kazi" wakati wa RC John Mhaville lisome taratibu linaweza kuwa la msaada kwako.

Nawatakia Sabato yenye baraka!
Ni utoto kufikiri unaweza kuondoa machinga mjini. Kama kuna mtu anabisha, subirini pale Makalla atakapotoka kwenye uRC uone kama machinga hawatakuwepo. Jambo limshinde JPM halafu Makalla aliweze? Ahahahahahah!!!
 
Kuwaondoa wamachinga kwa utaratibu wa sasa hakuwezi kuisafisha Dar es salaam kwa sababu machinga hawataondoka.

Ni heri upekue mafaili hapo ofisini kwako ukilipata lile la " Operesheni Nguvu Kazi" wakati wa RC John Mhaville lisome taratibu linaweza kuwa la msaada kwako.

Nawatakia Sabato yenye baraka!
naunga mkono hoja
P
 
Back
Top Bottom