Pre GE2025 Makalla: CHADEMA wanataka kuingiza Ebola Tanzania ili wazuie uchaguzi!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Precious Diamond

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
611
1,428
wakuu,

hata kama ni ndio kuchafuana ili washinde uchaguzi this is too much. Makalla anatakiwa kuchuliwa hatua mara moja, hapa anaongelea usalama wa nchi, kurusha tuhuma nzito kama hizi kwa CHADEMA bila ushahidi ni hatari.

Hili si jambo la kuchekewa kwa vyombo vya usalama wala msajili wa vyama vya siasa.

=====

Makalla akiwa mkoani Simiyu asema CHADEMA wanakusanya hela za tonetone ili walete Ebola na Mpox na kuweza kuzuia uchaguzi!

=====
Maoni ya Wadau kutokana kauli ya Makala

That is CPA (T), ndiyo wenye kuweka mipango ya maendeleo ya nchi. Mpaka sasa usalama hawajamwita kwa ajili ya mahojiano ili wahusika watiwe vunguni.

Wenye nia njema na nchi ni muda sasa wa kufungua kesi mahakamani ili Mh. Amos Makala alete ushahidi ili kuzia uwezekana wa kuwaangamiza waTanzania.
===
Huyu MTU ni ama CHADEMA imfikishe kwenye Sheria.

Au Dola iwakamate hao viongozi wanaoratibu Hilo.
===
Kwamba yeye anafanya kazi sana, kuliko Usalama wa Taifa mpaka amejua mipango ya CDM? Ilitakiwa mpaka muda huu awe amewekwa sehemu anahojiwa na kutoa ushahidi wa alichokisema.
===
Hicho alichosema anapaswa kuhojiwa atoe ushahidi, sio jambo dogo la kupuuzwa linaweza kutishia USALAMA WA TAIFA.
====
Kesho utasikia kateuliwa Balozi.
===
CHADEMA msipoenda mahakamani tutajua na nyie ni CCM B.
===
Ina maana kuanzia June huko watalii wasije Tanzania maana kutakuwa na Ebola na M-pox. Kauli hii kutolewa na Katibu Mwenezi wa chama tawala siyo jambo jepesi; na sijui kama anaelewa madhara yake.

Ukatibu Mwenezi wamrudishe tu Makonda. Pamoja na ishu zake zingine; anafaa sana kwa heka heka na amsha amsha hasa wakati huu wa uchaguzi. Makalla hana charisma, hawezi kujenga hoja na siyo mwongeaji mzuri. Inashangaza sana!
===
Kama uchaguzi ni kwa mujibu wa Katiba na Sheria hapo ndio rahisi kuuzuia maana wanaopinga kwa hoja ambayo mwamuzi ni mahakama.

Ni wapi wanauza Virusi vya Ebola na MPox wakati wakijua ni kosa kuzalisha na kuuza kwa nia ya kudhuru? Binadamu gani mwenye akili timamu anaenda kununua virusi (biological weapon) kwa nia ya kuua ndugu zake?

Je, huu sio ugaidi?

Kwanini huyo Makalla asishitakiwe, maana uongo ukikaliwa kimya wananchi watadhani kilichosemwa ni kweli?!

Walichojibu Chadema: Pre GE2025 - John Heche: Awa Mbogo kuhusu Makalla kudai CHADEMA italeta Mpox na Ebola, 'Ni mjinga na mhujumu uchumi' ataka Habari Leo wafunguliwe kesi
 
That is CPA (T), ndiyo wenye kuweka mipango ya maendeleo ya nchi. Mpaka sasa usalama hawajamwita kwa ajili ya mahojiano ili wahusika watiwe vunguni.

Wenye nia njema na nchi ni muda sasa wa kufungua kesi mahakamani ili Mh. Amos Makala alete ushahidi ili kuzia uwezekana wa kuwaangamiza waTanzania.
 
wakuu,

hata kama ni ndio kuchafuana ili washinde uchaguzi this is too much. Makalla anatakiwa kuchuliwa hatua mara moja, hapa anaongelea usalama wa nchi, kurusha tuhuma nzito kama hizi kwa CHADEMA bila ushahidi ni hatari.

Hili si jambo la kuchekewa kwa vyombo vya usalama wala msajili wa vyama vya siasa.

=====

Makalla asema CHADEMA wanakusanya hela za tonetone ili walete Ebola na Mpox na kuweza kuzuia uchaguzi!

View attachment 3279769
Dah this is too much sasa
 
Back
Top Bottom