makalio ya mke wa mtu

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
KIJANA mmoja amejikuta akiburuzwa kituo cha polisi bila kutegemea baada ya kumshika makalio mke wa mtu katika utani waliokuwa wakiendesha kati yao.
Kijana huyo ambaye aliyetambulika kwa jina moja l Jose [24] alikutwa na dhoruba hILO jana huko maeneo ya Kigogo Mburahati majira ya jioni.

Wakati Nifahamishe.com ilipokuwa ikipita maeneo hayo ilikuta umati wa watu ukiwa umemzonga mume wa dada aliyeshikwa makalio kwa kuhamaki na kumpiga mtuhumiwa na kumpa kichapo mkewe kutokana na kumkuta akiendesha utani huo.

Imedaiwa kijana huyo alikuwa akitaniana mara kwa mara na dada aliyefahamika kwa jina la Salama [28] bila ya mume huyo kutambua.

Jana mume wa Salama wakati akirudi nyumbani alimkuta mkewe na mwanaume huyo wakitania kama kawaida yao na ghafla aliona mkewe akishikwa makalioni na mwanaume huyo.

Mume wa Salama alimvamia kijana huyo na kuanza kumpa kichapo cha nguvu na kuwafanya wakazi wa maeneo hayo kuingilia kati kunusuru maisha ya kijana huyo.

Wakazi hao walijaribu kumwambia mume wa Salama kuwa mkewe na kijana huyo walikuwa wakitaniana.
 
Mke wa mtu unaruhusu nyeti zako kuchezewa barabarani!!!! Kweli ndoa haziheshimiwi siku hizi.
 
Ndugu zangu katika jf, kila stage ya maisha unayoifikia ina sifa na haiba yake. ukiwa msichana (miss) kuna namna na mazingira ambayo unatakiwa uwe. kama wewe ni mke au mume wa mtu lazima ujuwe siyo tu ujiangalie wewe tu lazima ujuwe kuwa umebeba jina la mtu nyuma yako, ukiona watu wanamshika mkeo usikimbilie kumlaumu aliyemshika pia uangalie upande mwingine wa shilingi, je aliyeshikwa anatabia zipi, mwendowake, mavaziyake, anaongozana na watu wa tabia zipi!.
nirahisi kulinda vituvyako visiibiwe kuliko kumlinda mbwa asiibe.
 
Back
Top Bottom