Makali ya mgao wa umeme: MUHIMBILI NAYO NDANI

Discoverer

Member
Jul 16, 2009
58
12
Katika hali isiyo kuwa ya kawaida, hospitali ya taifa ya Muhimbili nayo imeingia katika mgao mkubwa wa umeme tofauti na ilivyokuwa awali.
Wodi zilizo athirika zaidi ni sewa haji, kibasila, mwaisela, watoto na majokofu ya kuhifadhia ndugu walio tutangulia ambazo zote hizo hazina jenereta.
Hii inaonesha ni jinsi gani mambo yalivyo magumu!!!!!! Ukiona miili ya marehemu inavyoshushwa toka ghorofa ya juu utalia, na wagonjwa wa operation wanavyo pelekwa wodini ni hatari sana.
Ndugu zangu nini kifanyike au tuendelee kunung'unika tu??
 
Rais keshaichoka nchi huyu.. hadi hospitali zinakuwa mna mgao? inabidi aondoke kwa nguvu za wananchi .. hakuna kingine zaidi ya hapo .inabidi ajue kuwa kama hawezi wengine wana weza .. goodbye JK
 
Katika hali isiyo kuwa ya kawaida, hospitali ya taifa ya Muhimbili nayo imeingia katika mgao mkubwa wa umeme tofauti na ilivyokuwa awali.
Wodi zilizo athirika zaidi ni sewa haji, kibasila, mwaisela, watoto na majokofu ya kuhifadhia ndugu walio tutangulia ambazo zote hizo hazina jenereta.
Hii inaonesha ni jinsi gani mambo yalivyo magumu!!!!!! Ukiona miili ya marehemu inavyoshushwa toka ghorofa ya juu utalia, na wagonjwa wa operation wanavyo pelekwa wodini ni hatari sana.
Ndugu zangu nini kifanyike au tuendelee kunung'unika tu??

mkuu hii bahari nashindwa kumeza, mpaka hospitali kama kuna mtu maeneo wanayokaa vigogo hatujulisha kama hawana umeme au kama wanatumia genereta kama wanafanya hivyo basi wakati umefika kuiweka serikali yetu kwenye record za serikali kandamizi na TANZANIA itanjwa kuwa sehemu hatari kuishi dunia kutokana na matendo ya serikali yake
 
S erikali inunue majenereta kama wanashndwa kuzuia mgao maeneo nyeti kama hayo.
 
jk alishajua nchi imemshinda ck nyng ndo maana anaishi ughaibuni.wanaona aib kutangaza kwa sabab ya mapambo kibao waliyompa mwanzo
 
Unajua hawa viongozi walisha tuzarau sisi wananchi tulio wapa ajira kwahiyo wanatuongoza jinsi watakavyo wao sasatunasema basi tunahitaji nchi yetu.Ifahamike iliturudishiwe nchi yetu inabidi tufanye juhudi na nguvu kuichukua uwoga wetu hautatufikisha popote tutachekwa na vituku vyetu tunahitaji mobilazation ya nguvu ya maandamano ya kufamtu tukishinikiza Serikali yote ijiuzulu kwani imebaki kuwa watazamaji wala hawajui la kufanya kuhusu suala la umeme tutakaa mpakalini watu wanaendelea kufa mahospitalini.
 
'nimeisha waambia cna uwezo wa kugeuka wingu la mvua nikanyeshe mtela'
 
Matatizo ya tanzania nimeyakuta,na tatizo la umeme ni la ukame haya ni maneno ya rais wenu,nchi ya kipuuzi hii.
 
Kikwete afanye hivi,ahairishe safari moja ya nje hiyo fedha atakayosave anunue genereta kubwa kwa ajili ya muhimbili na balance itakayobaki iwe kwa ajili ya mafuta ya hiyo genereta mwaka mzima.
 
Jamani sehemu zote wafanye mgao wa umeme lakini sio maeneo ya hospitali kubwa kama muhimbili. Hiyo muhimbili ikiwa na umeme hali tete bila umeme je itakuwaje? Si ndio wagonjwa watakatwa ndimi badala ya kung'olewa meno mabovu?! Oh God have mercy! Sijui waTZ tukimbilie wapi?
 
Maskini nchi yangu! Wapi tunakoelekea jamani? Kwa kweli inasikitisha.
 
Vilio vya watanzania ni sawa na vile vilio ndani ya ile novel ya 'Unanswered Cries'by Osman Konteh,ni mda muafaka wa CDM kutoa tamko na kutuambia waTz tufanye nini,Dr.,Mbowe,Kabwe,Lissu,Mnyika tunaomba mtwambie tufanye nn?
 
Back
Top Bottom