Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,407
- 31,391
Ningependa tujadili mambo yenye tija kwa taifa, lakini tuhuma za kumwekea maneno mdomoni Mohamed ni nzito na ninapaswa kuzithibitisha au kuomba radhi. Ikifika hapo nachukua njia ya kuthibitisha neno 'vita' na analogy yake kama ninavyomnukuu Sheikh Mohamed Said Salum Samtungo:Mkuu,Huna haja ya kumwekea maneno mdomoni Mzee Muhamed Said,watu wote tumesoma na hatujaona neno vita sasa wewe haya umeyatoa wapi!?
Au wewe unalihitaji hilo liwe mtaji wa kisiasa au kwengineko?ili ionekane kwamba MS amechochea vurugu?
Ninacho kumbuka yeye kusema "nyinyi na sisi kukutana mezani,nyinyi kule,sisi huku kati wapatanishi" sasa hayo ya vita yanatoka wapi?
Kwanza anaanza kwa kuthibitisha kuwa nitakayoyaonyesha ni yake
Mohamed anaanza kujenga mazingira ya mfarakano katika jamii kwa maneno haya yenye kuonyesha vita kwa lugha ya unrestMohamed Said;2695214]WC, Hayo umesema wewe na mdomo haumkatai bwana wake
Kwamba uvunjaji wa mabucha ni kutokana na umasikini wa Kigoma, Lindi Tabora na Mtwara. Hapa hakuna ukweli bali kuunga unga hadithi ili kuleta maana aliyokusudia. Tuendelee kulitafuta neno vitaMohamed Said;2697795] Catholics form Most areas which are underdeveloped in Tanzania mainland are areas with Muslim majority like Kigoma,Tabora, Kilwa, Mtwara, Lindi etc. These areas are now re-examining themselvesand are gradually turning into local factions of radical Muslim politicsreminiscence of the era of nationalist politics of the 1950s. This could be asource of civil unrest in the very near future. Signs of this have begun toshow in the recurrent violent conflicts between Muslims and the government. Tanzaniahas experienced the Buzuruga Muslim-SungusunguConflict (1983), Pork Riots (1993) and Mwembechai Upheaval (1998)
Anatoa ujumbe ambao hauna neno vita lakini unaelekea huko tunavyosoma hapaMohamed Said;2697723]Mkandara,Allah anawaasa Waislam "wasidhulumu na wasikubali kudhulumiwa."
Bado neno vita halijatokea, lakini maneno yenye uelekeo huo yanaanza, tuendelee kulitafuta neno vitaMohamed Said;2717867]Mwanakijiji, serikali haijakubali kuwa tuna tatizo. Hadi watakapokiri na kutaka ushauri kipi kifanyike hapo ndipo tutazungumza . Kwa sasa tujikite katika kuisihi serikali iamke tuiepushe nchi yetu na vurugu.
Baada ya kuwaonya waislam wasikubali kudhulum au kudhulimiwa sasa anatamka neno vita kwa mdomo wake.Ameshajenga mazingira akatamka neno vita na akaweka na kulihusisha na imani kuwa, ni dhambi kukimbia vita ili kuwatia ushajaa watu wake. Lakini anahitimisha kauli yake ya vita kwa maneno haya ambayo kinyume na uandishi wake ameaua makusudi kuya 'bold' kutia msisitizo wa hamasa yake juu ya vitaMohamed Said;2725399]MM,Wako wanaokimbia humu ukumbini lakini mimi sijapata na Insha Allah Mungu asinijalie kukimbia vita,Hilo ni moja katika makosa makubwa sana katika Uislam
Mohamed Said;2716291]Ndugu zangu haya yote yaliyo humu ukumbini kuhusu dhulma dhidi ya Waislamu siku moja yatakuwa ndiyo ushahidi wetu ama tuko African Union (AU) au United Nations (UN)endapo kama baadhi ya watu wanavypenda kusema, tutakuwa "ignored" maana yake sisi hatuwezi kukubali hali hii iendelee daima. Serikali zote duniani zinajua hatari yake.
Hili si jambo la mchezo kama wanavyofikiri. Waislam tulianza mbali kwanza ilikuwa kuwaelimisha Waislam kujua hatari inayowakabili maana Sheikh Malik (Mungu amrehemu) alikuwa akisema kwanza waelimisheni Waislam kuhusu dhulma vinginevyo mkianza kuidai haki bila ya Waislam wenyewe kujua dhulma hao mnaowadaia watakupigeni vita.
Subirini zitakuja nchi hii kamisheni kuja kuchunguza ukweli. Siku hizi hawasubiri mpaka vita ianze kama Rwanda ndiyo waje.
Kuwa leo tunamkabili dhalim waziwazi kwetu ni ushindi mkubwa sana.Mohamed
Hadi hapo si kweli kuwa hajasema neno vita kama anavyodai. Kalisema direct na indirect. Huu ni ushahidi kuwa huwa simuwekei maneno mdomoni bali na nukuu maneno yake mwenyewe.
Huyu ni mjuzi sana wa uandishi , inahitaji umsome katika mistari na kila neno kumuelewa.
Mimi Nguruvi3 nasema kwa dhati kuwa Mohamed Said ameandika neno vita kwa maneno yake mwenyewe mara kadhaa na kutamka maneno yanayohusiana na vita mara kadhaa. Anayepinga ushahidi nilioweka hapo juu, atoe maoni yake ya kukanusha hoja zangu nami nitamuomba Moderator wa JF anichukulie hatua zinazolingana na 'kumwekea maneno', vinginevyo Mohamed aliyekanusha na Sandamatuta aliyenituhumu waniombe radhi kwa ukurasa wa mbele wa maneno yao!
Kuendelea kupuuza kauli hatari kama hizi ni kuupuza umma wa Watanzania. Tukemee bila haya kungali mapema kabisa.
Nguruvi3