Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,408
- 31,392
Ungekuwa unaitakia nchi hii amani usingeandika kuhusu vita na kupelekana UN au AU. Ni jambo la kusikitisha sana kuwa scholar kama wewe unadhani njia nzuri ya suluhu ni vita. Baada ya kuficha sana kile unachohubiri kwa siri mwenyezi mungu amekudhiri kwa kuandika mwenyewe kuhusu UN na AU kama madai hayatasikilizwa.
Nguruvi3,
Nadhani kwa hapa mimi na wewe tulipofika tumeshafahamiana pakubwa.
Mimi nimeeleza yanayowasibu Waislam kuanzia kupotoshwa kwa historia yao kwa kadri ya uwezo wangu. Tukahama huko tukaja mfumokristo nk Kwa nini nafanya jitihada hizi zote Natafuta salama ya nchi yangu Nahisi mwenzangu kama sasa umechoka na mnakasha. Nakuomba mimi na wewe tuishie hapa. Mohamed
Ni wewe umesema unakwenda mikoani kuhubiri kuhusu dhuluma lakini mwenyezi mungu ni mkubwa umetoa siri yako moyoni. Mohamed nakuhakikishia kuwa Watanzania ni waelewa na wanakuelewa wewe na wenzako mna nia gani. Nia yako si ya Sykes wala Nyerere kwa sababu wao waliongozwa na utu. Chuki ni maradhi mabaya sana na yanahitaji msaada wa SOS.
Unaposema asilimia 17 unajumisha waislam wote. Ukiulizwa shule zinazofelisha unasema si za waislam ni za BAKWATA.
Kwakuwa umepewa uongozi mafichoni na taasisi tusizozijua basi unachukua na jukumu la hukumu wanadamu wenzako.
Mtume Muhamad S.A.W hakufanya hivyo na wala halipo katika hadithi, sunna au Quran. Muombe mwenyezi mungu msamaha, uombe ukumbi huu msamaha wa kuhukumu na kushadidia vita. Huo ndio uongozi na ueledi.
Sitakaa kimya na wala sitachoka kuangalia kakundi kadogo ka watu kana taka kulivuruga taifa. Nitaendelea kutoa maoni yangu kwa kile utakachosema au kuandika na ambacho kipo nje ya maadili, usomi, ustaarabu na weledi. Mimi si miongoni mwa wale wanaosubiri wakubusu mkono wakisema 'sheikh kazi yako tunaiona'. Mohamed, Siondoki jamvini kwani kufanya hivyo ni kuwasaliti watanzania walioshi na wanaoishi kwa utangamano miaka nenda rudi.
Nawaomba wana jamvi, penye ukweli tupaseme na tupongeze bila haya wala soni
.Penye uongo, unafiki, usomi zuzu tukemee maana mtu anayetangaza nia ya vita si wa kumuangalia na kumdharau.