Makala ya wiki iliyoichefua ikulu ikatishia kufunga gazeti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makala ya wiki iliyoichefua ikulu ikatishia kufunga gazeti

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mpayukaji, Mar 15, 2012.

 1. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Nilichojifunza kutoka mgomo wa madaktari


  Nkwazi Mhango
  Kanada

  INGAWA mgomo wa madaktari wa nchi nzima ni tukio lililosababisha vifo ambavyo si kazi ya Mungu bali serikali, kuna somo umetoa.

  Sijui kama watu wengi hasa waathirika wameliangalia kama mimi. Wenye akili wanasema kila tukio limtokealo binadamu mwenye akili ni darasa tosha. Hivi ndivyo ilivyokuwa kwangu binafsi kama mwana taaluma na mkereketwa, ukiachia mbali kuwa mwanaharakati wa haki za binadamu.

  Hata kama siishi Tanzania, bado nayajua masahibu na mazingira ya watu wetu. Hivyo siandiki kutokana na hasira ya kuathiriwa na mgomo wa madaktari kwa vile nilipo sina upungufu wala shida ya huduma ya madaktari, ikichukuliwa kuwa afya ni haki ya msingi ya kila mwananchi (hapa si Tanzania).

  Siandiki kujisifu bali kuchochea hasira na welewa wa ndugu zangu Watanzania. Sitaki nieleze hali ya afya hapa Canada ikoje kwa vile kila mtu anajua kuwa kuna mfumo mzuri kuliko hata jirani zetu kusini, yaani Marekani.

  Ukimwambia Mcanada kuwa afya si haki ya binadamu anaweza kukushauri ukapimwe akili. Hayo tuyaache.

  Katika mgomo uliokwisha ambao umezaa mwingine nimejifunza yafuatayo:
  Kwanza, rais wetu haambiliki wala hasikii na sijui hii inasababishwa na uwezo wake wa kuelewa au anavyojiona baada ya kuwa rais.

  Maana ukiangalia yule Kikwete tuliyeambiwa ni kipenzi cha watu na chaguo la Mungu unashangaa inakuwaje kipenzi cha watu na chaguo la Mungu anakuwa mkatili ambaye hajali hata taarifa kuwa kuna watu wamepoteza maisha kutokana na mgomo.

  Unashangaa alipopata mshipa wa hata kuweza kwenda kwenye mkutano usio na umuhimu wala ulazima huku watu anaowaita wake wakifa kutokana na uzembe wa kawaida wa wateule wake! Kama hutajizuia kuhukumu ili usije ukahukumiwa, unaweza kumuita hata majina mengine ambayo si sahihi.

  Sitaki nifikie hapo. Unashangaa ni baba au mama gani anaweza kwenda kwenye biashara wakati wale anaowaita watoto wake wakiugua na kufa kutokana na sababu anazoweza kuzuia hata kuingilia, achia mbali kuzuia.

  Hivi waliopoteza maisha wangekuwa watoto wa Kikwete hata wapendwa wake kama vile Haji Mponda na Lucy Nkya, angeweza kupata hamasa kwenda Davos huku akiacha wakiteketea kwa kitu kinachohitaji si pesa wala nini, bali tamko lake? Je, huu ni ubinafsi na upogo kiasi gani?

  Hakuna haja ya kupindisha maneno, rais wetu, sijui wao, hajali. Maana angekuwa rais wetu angetujali badala ya kujali kujilisha pepo kwenye vikao visivyo na ulazima ikilinganishwa na wapendwa wetu waliopoteza maisha, ukiachia mbali wale wanaouawa na polisi wake.

  Siachi kujiuliza si mara moja wala mbili. Hivi hawa waliopoteza maisha wangekuwa watoto wake au hata mkewe angefanya alivyofanya? Lakini atajalije wakati yeye na familia yake wanatibiwa nje kwa pesa ya walalahoi wanaouawa na serikali kwa kuwadharau na kuwanyonya wananchi?

  Nasema hivi kutokana na yaliyotokea. kwa wale waliopoteza ndugu zao serikali kwao haina maana na ni mnyonyaji wa kawaida.

  Maana walipoichagua walijua itaingilia kwenye hali kama hizi. Kutofanya hivyo kunaifanya kupoteza uhalali mbele ya macho yao hata kama wanaogopa kuifurusha kutokana na woga ujinga na hata kuishi kwa matumaini.

  Kitu kingine nilichojifunza ni kwamba Watanzania ni watu wa ajabu ambao hawana tofauti na kondoo kwa kushindwa kuwaunga mkono madaktari. Usishangae ukakuta wanawalaumu madaktari bila kuangalia upande wa pili ambao unatibiwa nje.

  Hebu jiulize. Rais anaandamana na watu 40 kwenye ziara ya kutanua huku akiacha umma unateketea. Anapata wapi hiyo pesa ya kufanya hivyo kama si kutojali?

  Cha msingi cha kuzingatia ni kwamba ni hao hao wadharauliwa na wapuuziwa wanaokatwa pesa itokanayo na kazi na jasho lao kumlipia rais na wapendwa wake kwenda kutanua wakati punda hao hao wanaomwezesha wakipukutika kama wadudu yeye asihangaike hata kutumia akili ya kawaida achia mbali elimu.

  Kitu kingine nilichojifunza japo kinatia aibu ni kwamba wateule wa rais si wa kuguswa hata wakifanya madudu kiasi gani. Rejea Mponda na Nkya na wanaodaiwa kughushi vyeti vya taaluma. Yuko wapi bwana EPA bin Kagoda? Si anaendelea kutumia mahakama zetu na za kimataifa kuvuna pesa yetu huku tukijua mchezo wote na tusichukue hatua?

  Rais yuko tayari kuwatoa kafara wananchi ili kuwalinda wateule wake ambao kwake ni kila kitu na si wapiga kura.

  Hata hivyo ana shida gani na wapiga kura wakati hana mpango wala haki ya kugombea tena? Je, huu si utapeli wa kimfumo ukiachia mbali kuwa unyama wa ajabu ambao hata simba na fisi hawawezi kuufanya?

  Kitu kingine ni kwamba Tanzania ina ombwe kubwa la uongozi kuliko ambavyo imewahi kutokea. Kiongozi wetu huyu ni ajali ya kihistoria kutokana na ukosefu wa upendo na heshima kwa wananchi, amembebesha zigo waziri mkuu kiasi cha kuonekana mbaya wakati mbaya si yeye.

  Kimsingi, kinacholisumbua taifa ni ibada za sanamu, ambapo rais anaombwa badala ya kuamrishwa kama mtumishi yeyote wa umma. Nashindwa kuendelea.

  Chanzo:Tanzania Daima Machi 14, 2012.
   
 2. M

  Mmeku Tukulu Member

  #2
  Mar 15, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimesoma kwa makini makala hii,nimetokwa na machozi kwa kuililia nchi yangu Tanzania na watu wake wanavyoteseka na kuteketea kutokana na utawala usiowajali wananchi waliowaweka madarakani. Kulia haitasaidia kitu maana hawasikii vilio vyetu,tuamke watanzania tufanye maamuzi pale tutakapopata fursa na kuuondoa utawala usiojali wananchi wake. Mungu ibariki Tanzania.
   
 3. NdasheneMbandu

  NdasheneMbandu JF-Expert Member

  #3
  Mar 15, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 940
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hakika mkweere ni janga la taifa. Sijui Dr. Slaa alijuaje alipotutahadharisha wakati wa uchaguzi!
   
 4. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #4
  Mar 15, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mod Kama inawezekana wapige ban wote wanao itetea hii serikali ya magamba
   
 5. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #5
  Mar 15, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  "Kuendelea kuichagua ccm ni maafa" Dr Slaa 2010.
   
 6. Prishaz

  Prishaz JF-Expert Member

  #6
  Mar 15, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 1,930
  Likes Received: 1,462
  Trophy Points: 280
  Hii makala imetulia sana,naamini Jakaya anajua yote hayo ila ubishi, ushost kny utendaji na ukaidi ndiyo vinafanya wananchi wazidi kuteka
   
 7. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #7
  Mar 15, 2012
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Haya maafa yalianza kwenye sekta ya elimu pale Serikali ilipoamua kupuuza madai ya walimu na sasa inasambaa kwenye sekta ya afya na kwenye usalama wa raia kwa ujumla (angalia suala la milipuko ya mabomu mbagala na gongolamboto, mauaji ya albino, polisi kuua raia hovyo pasipo sababu yoyote na mengineyo mengi). Mambo yote haya yameibuka kwenye kipindi cha utawala wa awamu ya nne ambapo kwa ujumla watanzania wamekosa pa kuegemea na pale linapotokea tatizo hakuna wa kuwatetea ama pa kukimbilia.
   
 8. Avanti

  Avanti JF-Expert Member

  #8
  Mar 15, 2012
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 1,209
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Absolutely one sided makala, inafaa kwa upande ulee!
   
 9. A

  Ahakiz Member

  #9
  Mar 15, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hawana shida jk na wateule wake hawana shida wanasambaza umasikini ikifika 2015 watanunua kura na kusonga mbele kwa hari zaidi sana na kasi zaidi sana na kusambaza umasikini sana
   
 10. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #10
  Mar 15, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,207
  Likes Received: 1,007
  Trophy Points: 280
  Rais tulie nae ana ugonjwa wa kushindwa kufanya jambo zaidi ya moja kwa wakati mmoja. Nchi kama nchi huaga ina mambo mengi ya kutolea maamuzi yanayojitokeza kwa wakati mmoja hivyo hayatashughulikiwa mpaka ile ratiba ya rais iishe kwa kufanya maamuzi ya jambo moja kwa kila siku yake na ndio maana unaona makubwa yakijitokeza nchini na rais kutoyatolea ufumbuzi bali siku zote amekuwa akijitokeza baada ya madhara na wakati mwingine yashapitwa na wakati, na kuanza kuwahutubia watanzania kuwaeleza kuwa mchawi ni fulani na wala mimi sihusiki. Mtoa makala amegusia kuwa Tz tumepata janga la kihistoria. Kimsingi kwa kuzingatia kanuni za kimaumbile inatupasa kuvumilia tu hili janga litapita. 2015 sii mbali sana lakini tukiwa na rais kama tulie nae sasa inaonekana kama ni miaka 30. Tuombe Mungu tu atupatie nguvu za kuvumilia maumivu na kwa kuwa tuliyataka wenyewe, hili tatizo linatuhusu sisi na wala sii Mungu. Uvumilivu ndio utakaotupeleka katika wakatimwingine tutakapopewa mfumo mpya wa utawala Tanzania.
  .
   
 11. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #11
  Mar 15, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Mwandishi wa Makala hii ni mtu mwenye uchungu na nchi yetu, tena ajabu anaishi nje lakini ana uchungu.

  Sisi tulio ndani na tunaoumia na mambo yote haya tupo kimya tena tunapiga makofi kushangilia hotuba feki za kuturaghai. Eti kwa sababu tunaweka itikadi za chama mbele ya masilahi na uhai wa mtu. Ni aibu kwa Wazee wa liojiita wa DSM kushangilia wakati utumbo unatamkwa, ni aibu na shamefull kwa wanaojiita wanaharakati wa kujitegemea eti kutaka kufungua kesi ya kuwashitaki madakitari waliogoma.

  Wanashindwa kuelewa kuwa muuaji ni nani kama siyo serikali iliyokosa usikivu na kuwajali wananchi wake. Aliyosema mwandishi wa makala ni sahihi kabisa haiwezekani wewe nyumbani kwa ko kuna msiba eti unaenda kwenye harusi ya rafiki yako, unaacha msiba wa mwanao ndani!!!!! PTYUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUU!!!!!!!!! KICHEFUCHEFU KABISA YAANI!!!!!!!!!!!!!!  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
 12. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #12
  Mar 15, 2012
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hatua zishaanza kuchukuliwa:
  mf. Madaktari waliosababisha vifo vya wagonjwa 300 WATASHTAKIWA KARIBUNI kwa kusababisha vifo vya wagonjwa.
   
 13. m

  mkipunguni Member

  #13
  Mar 15, 2012
  Joined: Jul 1, 2010
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kikwete ni Tatizo kuliko Malaria, CCM na wateule wake ni Cancer ya NCHI NA WATANZANIA.... INAUMA SANA tena SANA
   
 14. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #14
  Mar 15, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280


  Inabidi kuanza na Watendaji na Viongozi wa Serikali ambao waliruhusu kwa uzembe mgomo ufanyike. Kwani wangelipungukiwa nini mwilini mwao kama wangeongea na madakitari mapema kama walivyofanya mwishoni baada ya maafa. (Mfano. maongezi ya pinda na madakitari ambayo yalizuia mgomo wa kwanza; na maongezi ya JK na madakitari yaliyozima mgomo wa pili)

  Kwa nini mnakuwa kama kikosi cha Zima moto kinachosubiri nyumba iwake moto kisha wanakutaja na magari yao kuzima too late!!!!!!!

  CHUKUA TAHADHARIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII KUZUIA MAJANGA!!!!!!!!!!!!!!! YANAYOZUILIKA!!!!!!!!!! ACHA KUTAFUTA SABABU ZA KISIASA!!!!!!  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
 15. D

  DURACEF JF-Expert Member

  #15
  Mar 15, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 244
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Unamaanisha dr jk,mponda na nkya{triplets}.
   
 16. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #16
  Mar 15, 2012
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  nitalisema tena hili, nimewahi kulisema kabla. Kikwete hajali yanayowatokea watanzania kwa kuwa ktk uchaguzi uliopita watanzania hawakumchagua. Alirudishwa madarakani na hao wateule wake kwenye taasis za usalama. ndio maana kwake Kikwete ni bora kuwajali na kuwalinda hao wasaidizi wake kuliko kuwajali watanzania ambao hawakumpigia kura anyway. mbona hili liko wazi kabisa kimazingira...
   
 17. Mlamoto

  Mlamoto JF-Expert Member

  #17
  Mar 15, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 347
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Uzalendo ndo huu. Kutetea nchi pasipo uoga! Naungana na Mchangiaji mmoja wa hapo juu, atakayepinga Hii Mada apigwe ban.
   
 18. M

  Msengapavi JF-Expert Member

  #18
  Mar 15, 2012
  Joined: Oct 23, 2008
  Messages: 4,807
  Likes Received: 2,751
  Trophy Points: 280
  Yes, Makala ni one sided but very true expression on the Zimwi litujualo na linalotumaliza. Wewe Avanti unaweza kuandika makala uonyeshe the other side. big up Mpayukaji
   
 19. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #19
  Mar 15, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Tumia fact kuutetea upande unao hisi unaonewa.
   
 20. kakakuona40

  kakakuona40 JF-Expert Member

  #20
  Mar 15, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 300
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nafili ulipaswa kusema MOD tafadhali wapige ban wote wanaotoa maoni kinyume na sera za JF
   
Loading...