Makala ya Mwanahalisi kuhusu SS, kusababisha kufungiwa tena...

Nikiwa kama kiswahili ni lugha yangu ya mwanzo.Naona hio sio statement, bali ni suali.Hivyo wako on the good side...keep up the good work guys...:A S tongue:
 
Uenda ikawa kuna ukweli ndani yake!!!

Akili ya Sofia haiwezi kuwaza zaidi ya ngono!

picture-6.jpg

Na Mbasha Asenga - Imechapwa 30 June 2010

Tuseme Ukweli

simba_195.jpg

KUNA dhana iliyojengwa kwamba watu wenye fikra nyepesi hujadili watu; wenye fikra za kati hujadili matukio na wale wenye fikra pevu hujadili dhana au tuseme mawazo.
Ingawa ni ukweli kwamba nadharia hii hutoa changamoto katika jamii ili watu wajielekeze kujadili mambo ya maana na si kubobea katika umbeya, ni vigumu pia kufungwa katika misimamo hii hasa tunapotazama ofisi za umma na waliozikalia.
Hakuna ubishi kuhusu nafasi ya waziri katika serikali kwamba ni kubwa, nzito na nyeti katika kuendesha si nchi tu, bali pia katika kushughulikia matatizo ya wananchi.
Kwa kawaida mtu anayebebeshwa jukumu la uwaziri katika jamii kama yetu, anatarajiwa awe ni mtu ambaye ana upeo, anayetambua dhamana aliyopewa ina maana gani kwa taifa lake?
Ndiyo maana hata “wanaposaga” fedha za walipa kodi, inakuwa si shida sana kwa sababu wanatarajiwa kusaidia kutatua kero za jamii.
Nafasi za uwaziri katika nchi zote duniani ni chache lakini nyeti, ndiyo maana wenye wajibu wa kuteua watu wa kushika nafasi hizo hutakiwa kujaa hekima na busara ili uteuzi utakaofanywa kwa kweli uonekane ukijielekeza kuisadia jamii kukabiliana na changamoto za maisha.
Unapozungumzia uwaziri kwa taifa kama hili, kinadharia unazungumzia mtu aliyepewa dhamana ya ofisi ya umma akiwa na mlolongo wa changamoto.
Kwanza, kuwa mstari wa mbele katika kusaka mwarobaini wa umasikini wa watu wetu; kuwa mbunifu wa kutumia rasilimali za taifa ili kuleta mabadiliko ya maana katika maisha ya wananchi kwa ujumla wake.
Uwaziri kwa maneno mengine unatakiwa uelekezwe kwa mtu ambaye atatambua kwamba cheo alichopewa ni mzigo; ni kutumika, ni kutumwa na kukosa usingizi.
Kama hiyo ni sehemu ya sifa ya mtu anayestahili kukabidhiwa nafasi ya uwaziri; basi hapana shaka kwamba wengi wa mawaziri wetu hawastahili katu kukalia nafasi walizopewa.
Hawastahili kwa sababu wamekosa sifa hizo kutokana na matendo yao kila uchao; ni watu wasiosumbuliwa na umasikini wa watu wetu.
Lakini zaidi sana ni watu wasiokuwa na fahamu kama wao ni mawaziri na kwamba wanatarajiwa walau waonyeshe mfano wa nini kifanyike ili kutokomeza umasikini wetu.
Bahati mbaya wengi wamebakia kuwa watazamaji. Hawana mbinu wala mikakati.
Kwa kawaida uwaziri ni dhamana, na kwa maana hiyo ni vigumu kuutengenisha uwaziri na utu wake, vimeshikamana kwa kuwa ni kwa muunganisho wa utu na uwaziri (cheo) ndipo maana ya nafasi hiyo inaonekana kwa jamii.
Yupo Waziri wa Ofisi ya Rais Utawala Bora, Sofia Simba, huyu pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT-CCM), ni waziri ambaye amepewa dhamana nzito, ‘utawala bora’.
Katika malengo makuu ya Mpango wa serikali wa Kupunguza Umasikini nchini (Mkukuta) suala la utawala bora ni miongoni mwa malengo makuu matatu yaliyoanishwa.
Mengine ni kuwaongezea watu kipato na kuwapatia maisha bora. Kwa maana hiyo, suala la utawala bora ni jambo linalopewa umuhimu wa kipekee ili kung’oa umasikini nchini.
Kwa hiyo, Sofia si waziri mwepesi kwa maana ya majukumu ya utawala bora; ni waziri ambaye katika hali yoyote ile kuzungumzia habari ya mapambano dhidi ya rushwa nchini angepaswa aonekane akiwa mstari wa mbele kwa sababu hilo ni eneo lake la kujidai.
Ukizungumzia habari ya demokrasia; hapo kungekuwa ni nyumbani wake; lakini pia ukizungumzia habari ya kudhibiti watumishi wanaojihusisha na vitendo vya ukiukaji wa maadili na sheria za utumishi, hapo pia ungemwona. Lakini wapi!
Pamoja na majukumu yote haya, Sofia ni mweupe kama ubongo wa kichanga cha leo. Hana lolote katika fikra zake kinachokaribia kumfanyakutambua majukumu yake.
Ni waziri ambaye kwa utumishi wake wa miaka takribani mitano sasa kwanza kama Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto na sasa Utawala Bora, ni vigumu kusema kwa yakini anafanya nini serikalini kama si kusubiri mshahara na marupurupu mengine ya uwaziri tu.
Hivi karibuni kwa kuthibitisha kiwango cha ufinyu wa fikra zake, aliwaambia wanawake wa CCM kwamba kama waume wao wanasaidia vyama vya upinzani, basi njia ya kuwakomesha ni kuwanyima tendo la ndoa.
Eti tendo la ndoa kwake ndicho kitu anachokiona cha maana na muhimu kutumika kama silaha! Sofia! Sofia!
Naogopa kumtaja Mama huyu kama ni mkware au vipi, yaani pamoja na nafasi zake zote alizoshikilia – waziri, mwenyekiti wa UWT, mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya chama chake, uwezo wake wa kifikiri hauvuki hisia na matamanio ya ngono!
Huyu ni kiongozi anayejinasibu kuwa anaweza kuwaunganisha wanawake na kuwaelekeza kwenye ukombozi wa kweli.
Ni mwanamke ambaye alitarajiwa kuwa nguzo ya wanawake wa CCM katika kuwaunganisha na kuwaelekeza kwenye njia inayofaa katika mapambano dhidi ya umaskini.
Ni mwanamke ambaye kwa macho ya wengi, angejua vilivyo njia bora zaidi za kupita ili wanawake wa taifa hili wajikomboe dhidi ya madhila ya umasikini wa kipato.
Alitakiwa kufahamu kwamba madhira haya yanachangiwa pamoja na mambo mengine, mfumo dume unaokataa kutambua nafasi za wanawake katika milki ya mali katika jamii.
Sofia kila anapomwaangalia wanawake wenzake anamwangalia kama mashine ya kumtuliza mwanaume; fikra zake kuhusu wanawake ni ngono.
Kwake, haoni nguvu nyingine yoyote ya wanawake ambayo inaweza kutumiwa kuleta mabadiliko katika jamii yetu; kwake mwanamke ni kiungo chake cha uzazi basi.
Katika dunia ya watu wanaowaza sawasawa siku Sofia alipotoa kauli ya kuwataka wanawake wawanyime waume zao unyumba, tungeona taharuki kubwa serikalini na hata bosi wake angemkemea kama si kumweka pembeni.
Lakini kwa kuwa nafasi za uwaziri zilikwisha kurahisishwa siku nyingi, bado ataendelea kutesa na kutesa, kwani ana shida gani wakati akili yake imeganda kwenye ngono na hicho ndicho kilichompa uwaziri?
Gazeti toleo na. 195
 
Wewe binafsi umetoa mchango gani kwa the Kubenea's of this world kuwafanya "watu kama SS na CCM wasiweze kuchukua ushindi kirahisi kwa sababu ya technical knockout za kirahisi"??
Una-substantiate vipi kuwa Kubenea asingeandika alichokiandika basi akina SS & co hawatapata ushindi wa kirahisi?
It only goes on prove my point kuwa kumbe mchango wa kina Kubenea (clean or dirt) unahitajika kuliko kunyamaza kama wewe na mimi tunafanya! Huu ukondoo na logic nyingi za wasomi make me really sick..

Mchango wa kwanza ni darasa la uandishi hapa, you don't write what you can't prove / bak up.

Sikusema kwamba Kubenea asingeandika alichoandika kina SS hawatapata ushindi wa kirahisi, nimesema kina Kubenea wakiandika kwa style hii kama ma simpleton watawapa SS na wenzake TKO on a silver platter, these two are totally different, now don't get it twisted.

Huwezi kusema mchango wa kina Kubenea clean or dirt unahitajika, huwezi kumuapproach mtu mwenye status quo, incumbency, bunge, tume ya uchaguzi, civil service, wafanyabiashara, dola, jeshi, executive na hata sehemu kubwa ya mahakama, huwezi kui approach administration hii iliyopo madarakani huku ukiwa na loopholes za kupigwa TKO, hutakiwi kumpa chance CCM na SS, unatakiwa kuja na case cleaner than a tablecloth ili kusudi hata yeye mwenyewe pamoja na kuwa na vyote alivyo navyo nilivyovitaja hapo juu, kama anataka kuku time afanye kazi ya ziada, na akikutime awe anakuonea tu, na akikuonea grassroot organizations tutapiga kelele zote zinazotakiwa.

Lakini leo Mwanahalisi umeingia mtegoni, umevuka mpaka, umesema kitu ambacho so far huna ushahidi, hata kama ni kweli, it is not about what the truth is, it is about what you can prove the truth is.Kwa hiyo watu wenye akili wanaweza kuona Mwanahalisi wamekuwa overzealous na hawako makini. Kama nilivyosema hapo juu, struggle inahitaji vichwa na Mwanahalisi kama wanashindwa mitego midogo midogo tu na kujitia vitanzi wao wenyewe kwa kuwa overzealous bila kuweza ku back up maneno yao wenyewe, basi watakuwa hawatufai katika vita dhidi ya status quo bongo.

Mpinzani halisi ni yule anayeweza kuona hata mapungufu katika upinzani.Sio kwa sababu Mwanahalisi ni gazeti linalojulikana kwa upinzani tu basi tuliunge mkono religiously. Sio kwa sababu CHADEMA ni chama cha upinzani basi tukiunge mkono religiously.

Waki boogie step wanasemwa kama kawa, na hizi habari za kutoa shutuma nzito, hata kama ziko disguised kama swali, bila kutoa backing evidence ziko juvenile.

Watoe ushahidi au waombe msamaha, vinginevyo hapa kuna a genuine defamation case ambayo huyu SS anaweza kushinda hata kama madai ya Mwanahalisi largely yana ukweli.
 
Mimi ningeishangaa serikali kama isingechukuwa hatua yoyote baada ya kuisoma makala hiyo kwa mara ya kwanza, hiyo sentensi ya mwisho si kejeli tu bali ni kashafa kwa mwanamke yeyote si mama Simba tu, na hatua zaidi ya kufungiwa kwa MwanaHalisi zingepaswa kuchukuliwa. Nawashangaa mnaowatetea MwanaHalisi kwa ukiukwaji wa wazi wa maadili ya uandishi na aibu kwa fani nzima ya habari.

Mhariri asingekosa lugha ya kueleweka zaidi ya hiyo na badala yake kachukuliwa na hisia za mwandishi wake (ambaye pengine ni mwanamke). Mimi sipingi harakati za vyombo vya habari kukemea ukiukwaji wa maadili ya uongozi lakini na wao wanapaswa kufanyakazi kwa sheria za nchi na maadili ya kazi zao zinavyoongoza.
 
Vyanzo vya ndani toka Wizara ya Habari, Michezo na Utamaduni ambayo ndiyo inasimamia tasnia ya habari vinadokeza kuwa Serikali imechukizwa sana na makala iliyoandikwa na gazeti la Mwanahalisi toleo la 195 lenye kichwa cha habari "Akili ya Sofia haiwezi kuwaza zaidi ya ngono" ambapo makala imetumia kejeli (sarcasm) kuelezea maoni ya Waziri Simba.

Sehemu ambayo inaonekana kuwatibua kabisa ni sehemu ya mwisho ya makalah hiyo:

Maneno hayo yaliyokolezwa rangi ndiyo yanaonekana kuwatibua wakuu kiasi cha kuandika barua ya kutaka maelezo toka kwa Mwanahalisi ya kwanini wasifungiwe.

Hata hivyo hilo la kutaka maelezo ni formality tu kwani wenye nchi wameshatoa agizo kuwa Mwanahalisi lifunguwe na safari hii kwa muda mrefu zaidi ili lisiwepo kuelekea uchaguzi mkuu.
jamani tuache uongo hii article jamani si tu inamtukana SS bali pia ina makosa makubwa haswa kwenye masuala ya gender discrimination and oppression! Hiyo article imemuanika mwanamke vibaya katika jamii na sidhani kama kuna mwanamke yeyote dunia hii atafurahia lugha hiyo itumike kwake! siamini macho yangu kama Mwanahalisi linaweza kuandika makala yenye kubagua jinsia namna hiyo katika karne hii ilhali hata hao wahariri wana mama zao na wake zao na watoto zao! Jamani huko ni kuvuka mpaka! tuwe fair!!! Kuna haja ya waandishi wetu kupewa somo la gender awareness la sivyo mama zetu watatukanwa kila siku bila kufahamu uchungu wanaousikia wanawake woote
 
What if what the are saying is true( which seems to be), and what if they can back up their statements, and what if it is misinterpetation of those who when they read between the lines it is bed, thighs and miniskirts which comes to their minds? Au kuna mtu ameguswa na contents? Hata kama gazeti likisema "she slept her way to the cabinet" not good enough kuwa libel and slander case.
 
Hivi kuna mtu ana clue kuhusu miongozo ya baraza la habari / mahakama inasemaje? Kwamba kipi kina warrant gazeti kufungiwa na kipi ni swala la fidia tu?

anything and nothing, at the sole discretion of the Minister. Once, he/she has acted on kufungia gazeti.. you can not appeal it anywhere, not even in a court of law.
 
Mwanakijiji, Nyani Ngabu, Junius, Kiranga na wengineo mliotoa michango kuhusu makala inayosemekana ya libel dhidi ya Waziri SS. Mbona hamtii maanani mchango wa Zak Malang (Reply No 21 hapo juu) kwamba ni bora suala hili lingeachiwa tu kati ya SS na Mwanahalisi? Kwa nini serikali iingilie?

Serikali hii imezoe sana kuingilia masuala ya libel na mengine yanayohusu individuals:

1. Hao hao Sofia Simba na Mkuchika (kama mawaziri) waliingilia kati na kumkemea, kumtisha Reginald Mengi alipowatangaza hadharani wale mafisadi papa. Haikuwahusu kabisa, kwani ilichotakiwa ni waliokashifiwa na Mengi ni kwenda Mahakamani -- kama walivyofanya baadhi yao baadaye.

2. DCI Manumba alituma makachero wa polisi kupekua ofisi za Mwanahalisi kutafuta nyaraka (statement za mteja) za benki ya NBC zilizosemekana zimevujishwa na mfanyakazi mmoja wa benki hiyo. Polisi haikuwa na haki kufanya upekuzi huo kwa individual kutokana na shinikizo kutoka taasisi binafsi (such as NBC), unless kama nyaraka hizo zingekuwa ni za serikali. Hilo lilikuwa ni kosa kwa upande wa serikali -- na kitu sahihi kilikuwa ni kwa Mteja wa NBC kuishitaki benki yake kwa kuvujisha statement zake kwa gazeti -- hatua ambayo mteja huyo (Chenge) kisha chukua.

Hivyo inafaa sana kuishinikiza serikali isiwe inaingilia masuala ya libel between individuals, kwani kuna mahakama zimewekwa kwa kazi hiyo.
 
However you spin this, serious accusation kwamba either ngono au akili yake kuwa kwenye ngono ndicho kilichompa uwaziri. Both are salacious accusations.Now they have to prove either or face a legitimate disciplinary action.
Kiranga, ile sentensi ya mwisho, ni direct defamation kwa SS na defamation by innuendo kwa JK, kama SS ameupata uwaziri kwa shughuli hiyo, inamaanisha, aliyempa huo uwaziri ndiye benefishary wa huduma iliyotolewa kumpatia uwaziri.

Ila Kiranga, kwenye presidential appointment powers, hakuna terms of reference wala criterial for such appointments, na SS anaonekana kama anavyoonekana, empty upstairs, hivyo inaruhusiwa to think aloud kuwa merits zilizompa uwaziri ni matumizi mazuri tuu ya alichonacho, hapa hata mimi nakiri udhaifu binafsi nikiangaliwa na yale macho tuu, track record ya muungwana huko nyuma inajulikana, hivyo that could be the posibility.

Mwanahalisi wamefanya kosa kumention direct names.
 
.............................................................
Huwezi kusema mchango wa kina Kubenea clean or dirt unahitajika, huwezi kumuapproach mtu mwenye status quo, incumbency, bunge, tume ya uchaguzi, civil service, wafanyabiashara, dola, jeshi, executive na hata sehemu kubwa ya mahakama, huwezi kui approach administration hii iliyopo madarakani huku ukiwa na loopholes za kupigwa TKO, hutakiwi kumpa chance CCM na SS, unatakiwa kuja na case cleaner than a tablecloth ili kusudi hata yeye mwenyewe pamoja na kuwa na vyote alivyo navyo nilivyovitaja hapo juu, kama anataka kuku time afanye kazi ya ziada, na akikutime awe anakuonea tu, na akikuonea grassroot organizations tutapiga kelele zote zinazotakiwa.

Lakini leo Mwanahalisi umeingia mtegoni, umevuka mpaka, umesema kitu ambacho so far huna ushahidi, hata kama ni kweli, it is not about what the truth is, it is about what you can prove the truth is.Kwa hiyo watu wenye akili wanaweza kuona Mwanahalisi wamekuwa overzealous na hawako makini. Kama nilivyosema hapo juu, struggle inahitaji vichwa na Mwanahalisi kama wanashindwa mitego midogo midogo tu na kujitia vitanzi wao wenyewe kwa kuwa overzealous bila kuweza ku back up maneno yao wenyewe, basi watakuwa hawatufai katika vita dhidi ya status quo bongo.
Kaka/dada yangu kwa hayo uliyoyasema hapo juu - you are already preaching to converts ambao unfortunately wanahisi wamefika peponi hivyo they have turned a deaf ear. How long has this dragged on now - 18 years??!! Akina NCCR, CHADEMA, CUF, etc wame-achieve nini all this time kwa kutumia hayo unayotu-lecture nayo hapo juu?? Kushika mtutu kupambana na status quo siyo practical kwa mazingira ya sasa lakini tuache ukondoo. Hivi hii sheria iliyopo unategemea ita-work in Kubenea's favour kweli hata kama atakuwa proved beyond reasonable doubt kuwa yuko right? EPA iko wapi? Richmond iko wapi? Meremeta? Wezi wa kuku tu mtaani wanapata kipondo gani in comparison?? Hizo institutions ulizozi-list kwenye red hapo juu zimefanya kitu gani all this while? Gimme a break. Guys, we must be practical - no silver platter stuff here. Sacrifices, sacrifices & sacrifices - this is what crusaders like Kubenea are doing...na sisi wasomi tuambukizwe hili and let's consign theories kwenye serious issues where they belong - trashbin! Extremely disppointed by wasomi (count me in) of this society.
 
Wanachotakiwa kuonyesha hapo si kwamba SS kazungumzia mambo ya ngono, bali kwamba kapata uwaziri ka mambo ya ngono. That is gonna be hard.

Kama ana credentials zinazostahiki kuwa waziri kuliko wengine kutoka katika kundi la waliokuwa na uwezo wa kuteuliwa(wabunge wa CCM kutoka mkoa wake au eneo lake la uchaguzi), kama uteuzi wake ulizingatia vigezo vya kitaaluma beyond doubts, then i do not see how wanaweza kujustfy maneno yao.
 
Mwanakijiji, Nyani Ngabu, Junius, Kiranga na wengineo mliotoa michango kuhusu makala inayosemekana ya libel dhidi ya Waziri SS. Mbona hamtii maanani mchango wa Zak Malang (Reply No 21 hapo juu) kwamba ni bora suala hili lingeachiwa tu kati ya SS na Mwanahalisi? Kwa nini serikali iingilie?

Serikali hii imezoe sana kuingilia masuala ya libel na mengine yanayohusu individuals:

1. Hao hao Sofia Simba na Mkuchika (kama mawaziri) waliingilia kati na kumkemea, kumtisha Reginald Mengi alipowatangaza hadharani wale mafisadi papa. Haikuwahusu kabisa, kwani ilichotakiwa ni waliokashifiwa na Mengi ni kwenda Mahakamani -- kama walivyofanya baadhi yao baadaye.

2. DCI Manumba alituma makachero wa polisi kupekua ofisi za Mwanahalisi kutafuta nyaraka (statement za mteja) za benki ya NBC zilizosemekana zimevujishwa na mfanyakazi mmoja wa benki hiyo. Polisi haikuwa na haki kufanya upekuzi huo kwa individual kutokana na shinikizo kutoka taasisi binafsi (such as NBC), unless kama nyaraka hizo zingekuwa ni za serikali. Hilo lilikuwa ni kosa kwa upande wa serikali -- na kitu sahihi kilikuwa ni kwa Mteja wa NBC kuishitaki benki yake kwa kuvujisha statement zake kwa gazeti -- hatua ambayo mteja huyo (Chenge) kisha chukua.

Hivyo inafaa sana kuishinikiza serikali isiwe inaingilia masuala ya libel between individuals, kwani kuna mahakama zimewekwa kwa kazi hiyo.

Na si hayo tu, kuna uwezekano mkubwa wa serikali (kwa maana ya Mkuchika) kumharibia SS kesi yake anayotarajia kufungua dhidi ya Mwanahalisi. Hebu fikiria Mkuchika akilifungia gazeti -- mawakili wa Mwanahalisi hawatasita kutaja mahakamani kwamba serikali imekwisha pre-judge uamuzi wa kesi hii kwa hivyo hakutapatikana uamuzi wa haki. Maana Mkuchika atatoa tafsiri yake binafsi ya "uchochezi" chini ya Sheria ya Magazeti ya 1976. Ni vyema serikali ikawaacha SS na Mwanahalisi waminyane mahakamani na serikali isiingilie.

Pia kunaweza kuwekwa precedent -- jee mimi nikiashifiwa na gazeti Mkuchika atalifungia? Kwani SS si individual tu mbele ya masuala ya libel yanayoandikwa na magazeti, au mawaziri wa JK wako above this?
 
hawa walishakosa kazi hata siwashangai akili zao zinatakiwa kukua na kushugulikia matatizo ya nchi hii wanachanganywa na nn mbona habari yenyewe inaeleweka

Tatizo kubwa hiyo makala iliandikwa kwa jazba?????????? wakasahau itasomwa na watu wengi wenye mtizamo tofauti na tafsiri zikwa tofauti pia. Ndio tatizo la wengi wa waandishi wetu
 
Serikali hii inajiingiza katika mambo mengine kwa kukurupuka. Itakuwaje kama Mwanahalisi itadhibitisha kuwa kuliwahi kuwa na mahusiano ya kingono kati ya mkulu na SS? hito haiwezi kuwa sababu ya kuhalalisha sentesi hiyo inayobishaniwa?
 
Some of the preceding sentiments just make me feel sick, bitter.
Mimi nasema hats off to Kubenea & co - at least they can dare. Wewe (sisi) je, can you (we)?
Ninyi (sisi) m(tu)naojiita wasomi ndiyo useless ingredients katika recipe ya kuleta mabadiliko ya kweli. Watu kama kina SS wanaropoka wapendavyo kwa vile ninyi (sisi) "wasomi" m(tu)mewaruhusu wafanye hivyo. Article ya kina Kubenea is an outcome of sheer frustration baada ya kuona watu ("wasomi") wanaotegemewa kuiweka sawa jamii kwa ku-challenge status quo wanaishia kulalama kutokea kwenye mablanketi (eg hapa JF) badala ya to come out openly na kusema "no" to this rubbish. So, as far as am concerned, screw the law if that's what it takes to turn things around. Mandela mwenyewe alikuwa branded "terrorist" na serikali ya makaburu (na pengine kwa sheria zao walikuwa right), akaponda mawe "Segerea" hatimaye akawa political icon of the planet! Ninyi wasomi mnataka kuniambia nini hapa?? Kama hujafanya chochote openly kama alivyofanya Kubenea, shut the hell up and instead anza kutafuta namna ya kutoa legal advice kwa crusader Kubenea. This society needs 100 Kubenea's - what a massive take-off that would be!

Big up!!!!!!!!!!!
 
jamani tuache uongo hii article jamani si tu inamtukana SS bali pia ina makosa makubwa haswa kwenye masuala ya gender discrimination and oppression! Hiyo article imemuanika mwanamke vibaya katika jamii na sidhani kama kuna mwanamke yeyote dunia hii atafurahia lugha hiyo itumike kwake! siamini macho yangu kama Mwanahalisi linaweza kuandika makala yenye kubagua jinsia namna hiyo katika karne hii ilhali hata hao wahariri wana mama zao na wake zao na watoto zao! Jamani huko ni kuvuka mpaka! tuwe fair!!! Kuna haja ya waandishi wetu kupewa somo la gender awareness la sivyo mama zetu watatukanwa kila siku bila kufahamu uchungu wanaousikia wanawake woote

Ndugu yangu mwanahalisi wanasakamwa kwa sababu SS ni kiongozi wa serikali na sio kwa sababu mwanamke katukanwa.
Kama kuhusu kutukana wanawake ingechukuliwa hatua nadhani wanaume wachache wangepona...jela zingejaa na sijui wengine wangewekwa wapi? Makonda wa daladala karibu wote wangehamia segerea maanake kosa lolote wafanyiwalo wao hubeza.....'weee mama tu....kila kosa njiani adhabu yake ni kutukana wanawake....ukifika kariakoo tusi linalohusu nyeti za kike liko mdomon mwa watu......mpaka mtu unashangaa hivi hawa wametokea wapi? hii dharau kwa wanawake walioteseka na mimba zao na kuwazaa kwa uchungu na saa nyingine kuwalea bila msaada wa baba zao INATOKA WAPI?
Maofisini mwanaume akionyesha udhaifu basi wenzie watamrifaa kama 'mwanamke' na mwanamke akionyesha ufanisi basi nae atafananishwa na mwanaume...jike dume bwana.
Unajua wanaume hawajui kuwa child rearing and pregnant ni experience ambayo kama unaifahamu vema either kwa kui experience au kwa kuifuatilia kwa makini ni process inayoonyesha kuwa mwanamke si mtu wa kudharauliwa
Anyway wanawake wamezoea kusakwa kwa kila jambo ndani ya mfumodume uliopo na kwa sababu wamewazaa wenyewe hao wanaowatukana basi may be wanawasamehe tu
.....anyway ss amewaboa wamemtukana lakini nimezoea kusikia kila uteuzi ni ngono ..sasa sijui hawa wanoteua wana uwezo gani wa kuwapitia....mawaziri woote wakike, wakuu wa wilaya (maana hawa ndio wanasakamwa zaidi). Ila mwanaume akiteuliwa bila shaka inaonekana ana SIFA ZA UONGOZI, AU RAFIKI WA MTEUA
Anyway bwana dunia itapita na mambo yake yoooote
mix with yours
 
Some of the preceding sentiments just make me feel sick, bitter.
Mimi nasema hats off to Kubenea & co - at least they can dare. Wewe (sisi) je, can you (we)?
Ninyi (sisi) m(tu)naojiita wasomi ndiyo useless ingredients katika recipe ya kuleta mabadiliko ya kweli. Watu kama kina SS wanaropoka wapendavyo kwa vile ninyi (sisi) "wasomi" m(tu)mewaruhusu wafanye hivyo. Article ya kina Kubenea is an outcome of sheer frustration baada ya kuona watu ("wasomi") wanaotegemewa kuiweka sawa jamii kwa ku-challenge status quo wanaishia kulalama kutokea kwenye mablanketi (eg hapa JF) badala ya to come out openly na kusema "no" to this rubbish. So, as far as am concerned, screw the law if that's what it takes to turn things around. Mandela mwenyewe alikuwa branded "terrorist" na serikali ya makaburu (na pengine kwa sheria zao walikuwa right), akaponda mawe "Segerea" hatimaye akawa political icon of the planet! Ninyi wasomi mnataka kuniambia nini hapa?? Kama hujafanya chochote openly kama alivyofanya Kubenea, shut the hell up and instead anza kutafuta namna ya kutoa legal advice kwa crusader Kubenea. This society needs 100 Kubenea's - what a massive take-off that would be!
Spot on M-mbabe!
Nchi hii ilipofikia inahitaji radical thinkers and implementers sio watu moderate kama wengi wanavyofikiri. Akina Kikwete wanafanya kila wanalolitaka kwenye nchi hii kwa sababu they know what kind of a society it is, society ya wafuata sheria mbovu. Pata maradicles 100 tu nchi hii katika kila sector hawa wezi hawawezi kutunyanyasa wapendavyo!! Big up MwanaHalisi.
 
Back
Top Bottom