Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Vyanzo vya ndani toka Wizara ya Habari, Michezo na Utamaduni ambayo ndiyo inasimamia tasnia ya habari vinadokeza kuwa Serikali imechukizwa sana na makala iliyoandikwa na gazeti la Mwanahalisi toleo la 195 lenye kichwa cha habari "Akili ya Sofia haiwezi kuwaza zaidi ya ngono" ambapo makala imetumia kejeli (sarcasm) kuelezea maoni ya Waziri Simba.
Sehemu ambayo inaonekana kuwatibua kabisa ni sehemu ya mwisho ya makalah hiyo:
Maneno hayo yaliyokolezwa rangi ndiyo yanaonekana kuwatibua wakuu kiasi cha kuandika barua ya kutaka maelezo toka kwa Mwanahalisi ya kwanini wasifungiwe.
Hata hivyo hilo la kutaka maelezo ni formality tu kwani wenye nchi wameshatoa agizo kuwa Mwanahalisi lifunguwe na safari hii kwa muda mrefu zaidi ili lisiwepo kuelekea uchaguzi mkuu.
Sehemu ambayo inaonekana kuwatibua kabisa ni sehemu ya mwisho ya makalah hiyo:
Sofia kila anapomwaangalia wanawake wenzake anamwangalia kama mashine ya kumtuliza mwanaume; fikra zake kuhusu wanawake ni ngono.
Kwake, haoni nguvu nyingine yoyote ya wanawake ambayo inaweza kutumiwa kuleta mabadiliko katika jamii yetu; kwake mwanamke ni kiungo chake cha uzazi basi.
Katika dunia ya watu wanaowaza sawasawa siku Sofia alipotoa kauli ya kuwataka wanawake wawanyime waume zao unyumba, tungeona taharuki kubwa serikalini na hata bosi wake angemkemea kama si kumweka pembeni.
Lakini kwa kuwa nafasi za uwaziri zilikwisha kurahisishwa siku nyingi, bado ataendelea kutesa na kutesa, kwani ana shida gani wakati akili yake imeganda kwenye ngono na hicho ndicho kilichompa uwaziri?
Gazeti toleo na. 195