Makala ya Jenerali Ulimwengu Kumkumbuka Prof. Chachage Setty Chachage

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,442
113,452
Wanabodi,
Hii ni makala iliitumwa kwangu na ndugu yangu Aboubakar Liongo kuhusu "Collective Imbecilization ya Profesa Chachage"

FEB 16, 2017 by JENERALI ULIMWENGU in MAKALA

HAYATI Chachage Seithy Chachage alikuwa ndugu yangu katika maana ya undugu ambayo inatambulika kwa wale waliowahi kuonja ukaribu wa kiroho na kimaadili nje kabisa na nasaba ya watu kuzaliwa ndani ya kaya moja au kutoka kabila moja, taifa moja au dini moja.

Chachage alikuwa mdogo wangu kiumri, na kwa hiyo nilikuwa nimemtangulia kwenda shule. Lakini pia alikuwa mwalimu wangu, na kwake nilijifunza mengi. Siyo tu alinifundisha (katika kiwango cha uzamili) Sosholojia wakati nikijaribu kutafuta maarifa katika nyanja mpya tofauti na kile nilichokuwa nimekisoma awali (Sheria), lakini katika mambo mengine mengi yasiyokuwa na uhusiano wa moja kwa moja na darasa rasmi.

Katika miaka ya 1990 Chachage alikuwa mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akifundisha Sosholojia, na alikuwa na ushawishi mkubwa kwa wanafunzi wake kutokana na jinsi alivyoweza kutanua fikra zake na kuzipeleka mbali zaidi ya yale yaliyoandikwa na wasomi wa kale, huku akichungua mazingira yake na kujitathmini yeye na jamii yake.

Kwa maana hii, Chachage alikuwa ana sifa za kweli za kuitwa msomi, akijipambanua na wale wanaojisingizia “usomi” kwa sababu tu wamekusanya vyeti vingi kutokana na kukariri mawazo ya wenzao waliokufa karne kadhaa zilizopita. Isitoshe, kwa “wasomi” wa aina hii, hata hayo mawazo ya wenzao hawakuyasoma bali wamefanya mbiu za kujipatia vyeti wasivyovifanyia kazi, hata ile ya kunakili peke yake.

Chachage alikuwa mwalimu aliyewafikirisha wale waliomzunguka kiasi kwamba watawala wanaoogopa kile wasichokijua au kukielewa wakamuona kama ni tishio kwa utawala wao. Ni namna gani fikra za mtu mdogo kama Chachage angeweza kuwatisha watawala wakubwa wenye kila aina ya uweza wa kujidumisha madarakani, sijaweza kuelewa lakini ukweli ni kwamba waliwaona watu kama Chachage (hakuwa peke yake) kama watu wasiostahili kuendelea kuwafundisha watoto wa Tanzania.

Uamuzi ukafanyika katika ngazi za juu za serikali za kuwaondosha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UD) na kuwapeleka katika taasisi nyingine mbalimbali ambazo hazikuwa na hadhi ya UD. Wengi walikubali, bila shaka kwa sababu waliiogopa serikali na pia walihofu kupoteza ajira na mlo, na wakaenda huko walikoambiwa waende. Chachage alikataa.

Mantiki ya Chachage ilikuwa wazi kabisa: “Mimi niliamua mwenyewe kujiunga na UD kama mhadhiri. Nigetaka kwenda katika asasi nyingine si ningeomba mwenyewe?” Mkuu mmoja wa ngazi ya juu kabisa alijaribu kila aina za ushawishi alimradi Chachage akubali kuondoka UD, lakini ndugu yangu huyo aligoma. Hatimaye akamwambia mkuu huyo kwamba yeye, Chachage, kama kuna mahali atakofundisha patakuwa ni UD, la sivyo aachiwe akafanye kazi nyingine jijini Dar es Salaam kama mtafiti.

Mkuu huyo hakupendezwa na wazo la Chachage kama mtafiti huria jijini Dar es Salaam kwa kuwa ingekuwa ni kumpa “mkorofi” huyo uwanja mpana zaidi wa kueneza fikra zake. Hatimaye, mkuu huyo akachoshwa na malumbano na kijana huyu, akakubali yaishe. Chachage akabaki UD, na siku anafariki alikuwa katikati ya kazi za chuo hicho. Wenzake walikwisha kusombwa na kupelekwa huko watawala walikowataka waende.

Huyo ndiye Chachage ninayetaka kumtambulisha kama msomi wa kweli, aliyejua nini anataka kufanya na kujua kwamba si lazima tukubali kila tunachoambiwa na watawala, ambao wanaweza kuwa na masilahi yasiyofanana na yetu wala ya jamii yetu.

Alisimama kidete kwa kile alichokiamini, na akajiweka katika uwezekano wa kukosa ajira ya serikali, lakini hakujali kwa sababu alijua kwamba kazi si lazima itokane na serikali peke yake kama mtu kweli anayo nia ya kufanya kazi. Muhimu, usiwe na uvivu wa kufikiria nyanja mbalimbali unamoweza kutoa mchango, na mchango wako ukawa wa manufaa na ukaheshimika.

Alikuwa mcheshi pia, mtu mwenye bashasha na mwenye furaha. Nakumbuka mwaka 2005, wakati wa kampeni za urais na ubunge, CCM walikuwa wameteua kaulimbiu ya kampeni, “ARI MPYA, NGUVU MPYA, KASI MPYA,” na kauli mpya hiyo ikawavutia watu kwa mamia ya maelfu kila mahali.

Chachage aliiangalia kaulimbiu hiyo, akaitathmini pamoja na wale waliokuwa wakiifanyia kampeni, mwisho akaniambia, “Unajua, hii kaulimbiu imebeba utabiri mkubwa. Sikuelewa anachotaka kusema mwalimu wangu, lakini akaniambia, “Angalia jinsi maneno yalivyopangiliwa, halafu soma silabi ya kwanza ya kila msitari” Nilipofuatilia nikasoma:

A RI MPYA

NGU VU MPYA

KA SI MPYA

Kwa kuchukua silabi ya kwanza ya kila msitari nikasoma: “ANGUKA”. Niliporudi kumwangalia nikakuta anacheka kile kicheko chake ambacho wengi walikuwa wanakitambua kama ishara ya utundu wa kisomi wa Profesa Chachage.

Siwezi kujua ni nini kilichokuwa kimemfanya aone kwamba katika hamasa yote ya mwaka 2005 kulikuwa na anguko lililokuwa linatuvizia, lakini hatimaye tulilishuhudia anguko hilo kubwa, si tu kwa wale waliobuni kaulimbiu hiyo bali na kwa hao walionufaika kutokana na hadaa ya ujumbe uliobebwa na kaulimbiu hiyo.

Dhima kuu ya yeyote anayestahili kuitwa “msomi” ni kuufanya ubongo wake ufanye kazi, wakati wote uzunguke na kubaini kile kinachoendelea, utafute, uchambue, upime, upambanue, usaili, uzue, uainishe, utanzue na utohoe. Hiyo ndiyo shughuli ya ubongo wa binadamu; shughuli ya ubongo wa mbuzi ni kuliwa.

“Msomi” ninayemweleza hapa, narudia, si yule mwenye vyeti vya kujaza viroba kadhaa, bali ni yule anayeisumbua akili yake ili ifanye kazi. Kwa bahati mbaya Kiswahili hakijapata neno mwafaka la kueleza maana ya neno la Kiingereza “intellectual”, ambalo linaweza kumweleza mtu asiye na vyeti vya chuoni lakini ana akili inayofanya kazi.

Chachage Seithy Chachage alikuwa na hivyo vyeti, lakini pia alikuwa na akili iliyofanya kazi. Alitutoka akiwa mchanga kiumri, na wakati ule nilihisi kwamba ubongo wake ulikuwa unachanua zaidi na kuvinjari nyanda pana zaidi. Hatuna namna ya kujua ni nini angeweza kufanya kama angeishi miaka mingine 20, lakini nahisi yangekuwa mambo makubwa.

Katika mambo mengi nitakayoyakumbuka kutoka kwa Chachage ni jitihada zake za kukataa kile alichokiita “Collective Imbecilization”. Huwa nawashauri wanaosikiliza wasianze kutafua “Imbecilization” katika kamusi ya Kiingereza kwa kuwa hilo ni neno alilotengeneza Chachage mwenyewe.

Nilivyoelewa mimi ni kule kuwapumbaza watu mamilioni kwa mpigo. Ni kama vile ingewezekana kuwakusanya watu milioni 50, ukawaweka ndani ya holi moja kubwa la ukubwa huo, ukafunga madirisha na milango, kisha ukawanyunyizia dawa ya uzuzu, ubwege na ufala, ikawakolea sawasawa kabla hujawaachia waende duniani waendelee na shughuli zao. Hiyo ndiyo Chachage aliita “collective imbecilization”.

Kadri nilivyoieleza hapo juu, ni dhahiri kwamba hiyo haiwezekani katika mazingira ya kawaida. Isipokuwa inawezekana watu wakapumbazwa kwa pamoja, wakafanywa mazuzu kwa pamoja, wakageuzwa mabwege kwa pamoja, hata kama hawajioni ndani ya ukumbi huo kabambe na wala hawasikii harufu ya dawa ya ajabu wanayopuliziwa.

Napenda kuonyesha, kupitia makala chache zitakazofuatia hii, ni jinsi gani mifumo yetu mbalimbali inaweza kutumika, na imetumika hasa, kujaribu kutufanya sote tuwe mazuzu kama ambavyo alieleza vizuri Chachage alipokuwa akizungumzia “collective imbecilization”.

Nitajaribu kuonyesha ni kwa jinsi gani juhudi zinafanywa ili tukubali kuacha kutumia bongo zetu na badala yake tutumie bongo za kuazima za hao wanaodhani kwamba jinsi wanavyofikiri wao ndivyo kila mmoja wetu anatakiwa afikiri, na asiyefikiri kama wao anakuwa ni punguani.

Nia yangu ni kuwatahadharisha wasomaji wa safu hii dhidi ya jaribio lo lote linalokusudia kutufanya tuache kufikiri. Tayari juhudi hizo zimekwisha kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kutufanya kuwa “mabwana-ndiyo” (yes-men), watu wa kumezeshwa maneno, dhana, fikra na imani zisizokuwa na maana, nasi tukazikubali bila kusaili lolote.

Aidha nitaelekeza ni kwa nini nadhani kwamba taifa la “mabwana-ndiyo haliwezi kupiga hatua yoyote ya maendeleo hata kama lingesimikwa katika machimbo ya lulu na almasi.

Tuwe pamoja
 
hivi neno ni hali au ali...??..
ina maana chachage alishindwa kutofautisha hapo usahihi ni upi..??..au ndio ilikuwa ktk kile akipendacho kiwe..???
 
Jenerali at his best! Tunazisubiri makala zako kwa hamu sana, taifa liko njia panda!
 
Pascal Mayalla,
Shukrani kwa kuleta bandiko murua la wiki. Jenerali siku zote waraka wake hukufanya uweze kutambua kinachotokea katika jamii yetu kwa kutumia ufafanuzi wenye kueleweka.
 
Nimependa neno moja tu collective imbecilization yaani kuwafungia watu katika holi kubwa na kuwajaza uzuzu,upuuzi na ufala
 
Uandishi wa namna hii ndio huwa unanisisimua ike mbaya.
 
Ulimwengu na yeye si alikua katika kundi lililofungiwa katika chumba alafu baade akawa zuzu, kupitia vyombo vyake vya habari alipiga sana kampeni, baada ya uchaguzi alizawadiwa Uenyekiti wa baraza la Michezo Taifa, ghafla ikaja skendo ya Uraia

Baada ya hapo ndio akaanza kutumia akili yake kufikiri na kufukiria
 
Maeneo kama haya ndio utaona utofauti wa jenerali Ulimwengu na waandishi wengine. Huyu mzee ni mwanafalsafa,makala zake zinafikirisha sana
Hazina ya taifa yule bwana, sijui kwa nini tumeshindwa kujijengea utamaduni kama taifa kutumia raslimali watu kama hawa! Maono mapana, nguvu ya hoja na kichwa kilichotulia pasi na mihemuko?! Njozi za vi-wonder tutazifikia kweli bila watu kama hawa?!
 
Back
Top Bottom