Elections 2010 Makala Ya HabariLeo: Vita ya CCM,Chadema, vyombo vya habari isipotoshe umma

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,285
24,155
NIMEFUATILIA kwa karibu mwenendo wa kampeni za uchaguzi mkuu wa rais, bunge na madiwani nchini, utakaofanyika Oktoba 31, mwaka huu.
Licha ya kusimamiwa na sheria, kanuni,

utaratibu, bado kuna kasoro nyingi zinazoonekana waziwazi katika kampeni zetu. Nimebaini mambo si sawa! Wananchi tunapaswa kuwa makini kwa wakati huu wa uchaguzi ili tusije kuburuzwa na baadhi ya wagombea.

Kasoro ninazozizungumzia, zimegawanyika katika sehemu kuu mbili. Sehemu ya kwanza ni mwenendo wa wagombea kupitia vyama mbalimbali; na sehemu ya Pili, kuna udhaifu mkubwa kwa baadhi ya vyombo vya habari ; na mwandishi mmoja mmoja katika kuandika habari za
uchaguzi.

Nikianza na suala la wagombea, kumekuwapo na mivutano ya hapa na pale baina ya wagombea na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ;na tusipotafakari na kuelezana ukweli, inaweza kubabaisha wapiga kura.

Kwa upande wa wagombea, ingawa nilikuwa sitaki kutaja wagombea na vyama vyao ili nisitumbukie katika mtego wa kampeni chafu, nitawataja ili niwasaidie wale ambao hawakusikia juu ya mgogoro ili wapate kujua kilichojiri.

Ukweli ni kwamba inawezekana kwamba mgombea mmoja, akashindwa kukabiliana na mwingine aliyejiandaa vyema kuingia katika kampeni ; au kwa upande wa sera za chama chake, hivyo akajikuta akitumia visingizio mbalimbali ili ionekane kana kwamba anakwamishwa, kutokana na kutokuwapo na mazingira sawa ya kiushindani.

Tunaposikia kwamba Chadema imemwekea pingamizi mgombea urais wa CCM , Jakaya Kikwete, halafu Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, akatoa uamuzi juu ya pingamizi hilo, halafu Chadema ikadai kwamba uamuzi huo umekiuka sheria, hapo kuna tatizo!

Tatizo ninaloliona hapa ni kwamba inapofikia taasisi inayosimamia vyama vya siasa, inashindwa kuaminiwa na viongozi wa chama hicho, ujue kutakuwapo na visingizio hadi mwisho!

Nasema hivyo kwa sababu iwapo chama hicho, kitaendelea kukosa imani, na baadaye kikashindwa katika uchaguzi huu, basi kitakuwa na kisingizio kwamba uchaguzi haukuwa huru na wa haki. Hilo halikwepeki, kwani dalili zimeshaanza kuonekana. Tukumbuke methali isemayo kuwa “Pafukapo moshi, ujue kuna moto.”

Ninachofahamu mimi ni kwamba masuala ya kisheria, lazima yatekelezwe kisheria. Ni jambo la ajabu kumsikia Mwanasheria mkongwe wa chama hicho, Mabere Marando, akitamka kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa kakiuka sheria, lakini wakati huo huo anasema kwamba wananchi ndio watakaotoa hukumu.

Mwanasheria huyo anataka tuamini kwamba hajui mahala pa kwenda iwapo Tendwa asipotenda haki? Hiyo ni aibu kubwa, kwani ingawa mwanasheria husika anaweza kuwa gwiji wa kuchambua masuala ya kisheria, akitoa kauli hiyo inaonekana wazi kwamba anafahamu fika kuwa kuna jambo linalombana.

Inawezekana hata yeye, akawa ametafuta vifungu vya sheria ili kutoa hoja ya kisheria, lakini vilevile ya kisiasa. Kwa hali ya kawaida, wananchi ni rahisi kuchanganyikiwa, kwani si rahisi kujua nani mkweli au muongo.

Hiyo inatokana na ukweli, kwamba Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, inafanya kazi zake kwa mujibu wa sheria ; na Marando ni mwanasheria, hivyo wananchi wamwamini nani kati ya hao wawili?

Naamini na kushawishika kwamba Msajili wa Vyama vya Siasa, anafanya kazi zake kwa mujibu wa sheria, hivyo siamini kwamba uamuzi wa kutupilia mbali pingamizi la Chadema, kuwa ulikuwa wa kisiasa.

Jambo jingine kuhusu wagombea, ni kitendo cha kuhusisha masuala binafsi ya wagombea, kama sehemu ya propaganda kwa baadhi ya vyama vya siasa. Baada ya kufuatilia kwa makini suala la Dk. Willibrod Slaa, kuandaliwa mashtaka ya kuoa mke wa mtu na kudaiwa fidia,
nimebaini kwamba limeanza kupoteza mwelekeo wa wapiga kura.

Badala ya wananchi kusikiliza sera na ahadi za wagombea, sasa suala hilo ndio gumzo mitaani. Mengi yanasemwa kuhusu sakata hilo. Wapo wanaodai kwamba mgombea huyo, ametengenezewa kesi ili kumchafua mbele ya jamii hatimaye asiweze kutimiza ndoto yake ya kuingia Ikulu.

Kwa maana hiyo basi, suala hilo linaweza kumwongezea au kumpunguzia umaarufu kwa kipindi hiki. Tunapojadili suala hili kwa makini, tunapaswa kujiuliza kwamba lina maslahi ya taifa au la?

Ingawa ni muhimu kujua maadili ya kiongozi anayegombea urais, tunataka kusikia chama chake, kina sera gani ; na si kubadili mwelekeo na kuanza kujitetea kwa wananchi, juu ya tuhuma zinazomkabili.

Aidha, nimekuwa nikisikia vyama hivyo, vikipondana kwa hoja za msingi, lakini nyepesi, kutokana na ukweli kwamba lengo lake si kutoa mwelekeo wa mustakabali wa nchi, bali ni kutengeneza hali fulani kuchochea umma, kwa maana ya kupandikiza chuki kati ya wagombea na wagombea au wagombea na wananchi.

Ingawa huu ndio wakati mwafaka wa propaganda, hiyo si sahihi. Kwa kumalizia, vyombo vya habari vifanye kazi yake, kwa kuzingatia maadili na kanuni tulizokubaliana katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu, badala ya kuwa mashabiki na washambuliaji wa vyama na wagombea.

Imeandikwa na Neophitius Kyaruzi; Tarehe: 13th September 2010 @ 22:00 Imesomwa na watu: 4; Jumla ya maoni: 0
Source:

HabariLeo | Vita ya CCM,Chadema, vyombo vya habari isipotoshe umma
 
Tunaposikia kwamba Chadema imemwekea pingamizi mgombea urais wa CCM , Jakaya Kikwete, halafu Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, akatoa uamuzi juu ya pingamizi hilo, halafu Chadema ikadai kwamba uamuzi huo umekiuka sheria, hapo kuna tatizo!

Tatizo ninaloliona hapa ni kwamba inapofikia taasisi inayosimamia vyama vya siasa, inashindwa kuaminiwa na viongozi wa chama hicho, ujue kutakuwapo na visingizio hadi mwisho!

Nasema hivyo kwa sababu iwapo chama hicho, kitaendelea kukosa imani, na baadaye kikashindwa katika uchaguzi huu, basi kitakuwa na kisingizio kwamba uchaguzi haukuwa huru na wa haki. Hilo halikwepeki, kwani dalili zimeshaanza kuonekana. Tukumbuke methali isemayo kuwa "Pafukapo moshi, ujue kuna moto."
Nafikiri huyu sliyeandika habari hii anatafuta excuse ili hapo CCM itakaposhinda kwa kuiba kura, ionekane kwamba CHADEMA ni wa hivyo hivyo. Kwanza huyu mwandishi yeye ni mwanasheria? Kama siyo mwanasheria anawezaje kubishia mambo asiyoyajua? Hivi wewe siyo daktari, unawezaje kukataa matibabu ambayo daktari amekuandikia? Nafikiri kauli hii haina mshiko. Kama marando alipotoka kwanini CCM au Tendwa hakukanusha kauli yake.

Jambo jingine kuhusu wagombea, ni kitendo cha kuhusisha masuala binafsi ya wagombea, kama sehemu ya propaganda kwa baadhi ya vyama vya siasa. Baada ya kufuatilia kwa makini suala la Dk. Willibrod Slaa, kuandaliwa mashtaka ya kuoa mke wa mtu na kudaiwa fidia,
nimebaini kwamba limeanza kupoteza mwelekeo wa wapiga kura.

Badala ya wananchi kusikiliza sera na ahadi za wagombea, sasa suala hilo ndio gumzo mitaani. Mengi yanasemwa kuhusu sakata hilo. Wapo wanaodai kwamba mgombea huyo, ametengenezewa kesi ili kumchafua mbele ya jamii hatimaye asiweze kutimiza ndoto yake ya kuingia Ikulu.

Kwa maana hiyo basi, suala hilo linaweza kumwongezea au kumpunguzia umaarufu kwa kipindi hiki. Tunapojadili suala hili kwa makini, tunapaswa kujiuliza kwamba lina maslahi ya taifa au la?

Ingawa ni muhimu kujua maadili ya kiongozi anayegombea urais, tunataka kusikia chama chake, kina sera gani ; na si kubadili mwelekeo na kuanza kujitetea kwa wananchi, juu ya tuhuma zinazomkabili.
Nashangaa kama makala hii imeandikwa kwenye gazeti la habari leo. Hivi kuna gazeti lililoandika habari za kuoa kwa Slaa kama habari leo? Nafikiri hata magazeti ya UDAKU yale ya Shigongo hayakuandika habari za kuoa kwa Slaa kama lilivyoandika gazeti hili. Ninashangaa kama hii leo gazeti hilo hilo linaweza kuchapisha makala ya kuwaasa wengine kuacha kufanya ambayo gazeti hili limekuwa pioneer wa kuyafanya hayo?
 
habari leo wasubiri kimbunga ockoba, watajutaaaaa kuwa wandishi wa habari makanjanja.
 
NIMEFUATILIA kwa karibu mwenendo wa kampeni za uchaguzi mkuu wa rais, bunge na madiwani nchini, utakaofanyika Oktoba 31, mwaka huu.
Licha ya kusimamiwa na sheria, kanuni,

utaratibu, bado kuna kasoro nyingi zinazoonekana waziwazi katika kampeni zetu. Nimebaini mambo si sawa! Wananchi tunapaswa kuwa makini kwa wakati huu wa uchaguzi ili tusije kuburuzwa na baadhi ya wagombea.

Kasoro ninazozizungumzia, zimegawanyika katika sehemu kuu mbili. Sehemu ya kwanza ni mwenendo wa wagombea kupitia vyama mbalimbali; na sehemu ya Pili, kuna udhaifu mkubwa kwa baadhi ya vyombo vya habari ; na mwandishi mmoja mmoja katika kuandika habari za
uchaguzi.

Nikianza na suala la wagombea, kumekuwapo na mivutano ya hapa na pale baina ya wagombea na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ;na tusipotafakari na kuelezana ukweli, inaweza kubabaisha wapiga kura.

Kwa upande wa wagombea, ingawa nilikuwa sitaki kutaja wagombea na vyama vyao ili nisitumbukie katika mtego wa kampeni chafu, nitawataja ili niwasaidie wale ambao hawakusikia juu ya mgogoro ili wapate kujua kilichojiri.

Ukweli ni kwamba inawezekana kwamba mgombea mmoja, akashindwa kukabiliana na mwingine aliyejiandaa vyema kuingia katika kampeni ; au kwa upande wa sera za chama chake, hivyo akajikuta akitumia visingizio mbalimbali ili ionekane kana kwamba anakwamishwa, kutokana na kutokuwapo na mazingira sawa ya kiushindani.

Tunaposikia kwamba Chadema imemwekea pingamizi mgombea urais wa CCM , Jakaya Kikwete, halafu Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, akatoa uamuzi juu ya pingamizi hilo, halafu Chadema ikadai kwamba uamuzi huo umekiuka sheria, hapo kuna tatizo!

Tatizo ninaloliona hapa ni kwamba inapofikia taasisi inayosimamia vyama vya siasa, inashindwa kuaminiwa na viongozi wa chama hicho, ujue kutakuwapo na visingizio hadi mwisho!

Nasema hivyo kwa sababu iwapo chama hicho, kitaendelea kukosa imani, na baadaye kikashindwa katika uchaguzi huu, basi kitakuwa na kisingizio kwamba uchaguzi haukuwa huru na wa haki. Hilo halikwepeki, kwani dalili zimeshaanza kuonekana. Tukumbuke methali isemayo kuwa "Pafukapo moshi, ujue kuna moto."

Ninachofahamu mimi ni kwamba masuala ya kisheria, lazima yatekelezwe kisheria. Ni jambo la ajabu kumsikia Mwanasheria mkongwe wa chama hicho, Mabere Marando, akitamka kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa kakiuka sheria, lakini wakati huo huo anasema kwamba wananchi ndio watakaotoa hukumu.

Mwanasheria huyo anataka tuamini kwamba hajui mahala pa kwenda iwapo Tendwa asipotenda haki? Hiyo ni aibu kubwa, kwani ingawa mwanasheria husika anaweza kuwa gwiji wa kuchambua masuala ya kisheria, akitoa kauli hiyo inaonekana wazi kwamba anafahamu fika kuwa kuna jambo linalombana.

Inawezekana hata yeye, akawa ametafuta vifungu vya sheria ili kutoa hoja ya kisheria, lakini vilevile ya kisiasa. Kwa hali ya kawaida, wananchi ni rahisi kuchanganyikiwa, kwani si rahisi kujua nani mkweli au muongo.

Hiyo inatokana na ukweli, kwamba Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, inafanya kazi zake kwa mujibu wa sheria ; na Marando ni mwanasheria, hivyo wananchi wamwamini nani kati ya hao wawili?

Naamini na kushawishika kwamba Msajili wa Vyama vya Siasa, anafanya kazi zake kwa mujibu wa sheria, hivyo siamini kwamba uamuzi wa kutupilia mbali pingamizi la Chadema, kuwa ulikuwa wa kisiasa.

Jambo jingine kuhusu wagombea, ni kitendo cha kuhusisha masuala binafsi ya wagombea, kama sehemu ya propaganda kwa baadhi ya vyama vya siasa. Baada ya kufuatilia kwa makini suala la Dk. Willibrod Slaa, kuandaliwa mashtaka ya kuoa mke wa mtu na kudaiwa fidia,
nimebaini kwamba limeanza kupoteza mwelekeo wa wapiga kura.

Badala ya wananchi kusikiliza sera na ahadi za wagombea, sasa suala hilo ndio gumzo mitaani. Mengi yanasemwa kuhusu sakata hilo. Wapo wanaodai kwamba mgombea huyo, ametengenezewa kesi ili kumchafua mbele ya jamii hatimaye asiweze kutimiza ndoto yake ya kuingia Ikulu.

Kwa maana hiyo basi, suala hilo linaweza kumwongezea au kumpunguzia umaarufu kwa kipindi hiki. Tunapojadili suala hili kwa makini, tunapaswa kujiuliza kwamba lina maslahi ya taifa au la?

Ingawa ni muhimu kujua maadili ya kiongozi anayegombea urais, tunataka kusikia chama chake, kina sera gani ; na si kubadili mwelekeo na kuanza kujitetea kwa wananchi, juu ya tuhuma zinazomkabili.

Aidha, nimekuwa nikisikia vyama hivyo, vikipondana kwa hoja za msingi, lakini nyepesi, kutokana na ukweli kwamba lengo lake si kutoa mwelekeo wa mustakabali wa nchi, bali ni kutengeneza hali fulani kuchochea umma, kwa maana ya kupandikiza chuki kati ya wagombea na wagombea au wagombea na wananchi.

Ingawa huu ndio wakati mwafaka wa propaganda, hiyo si sahihi. Kwa kumalizia, vyombo vya habari vifanye kazi yake, kwa kuzingatia maadili na kanuni tulizokubaliana katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu, badala ya kuwa mashabiki na washambuliaji wa vyama na wagombea.

Imeandikwa na Neophitius Kyaruzi; Tarehe: 13th September 2010
Source: habarileo

kabla ya kujadili makala hii unayojaribu kujisafisha na kigazeti chenu, kwanza mnapashwa kuwaomba radhi watanzania kwa kukiuka maadili ya uandishi wa habari kwa kiwango kikubwa. Tena kwa kutumia kodi zetu kupandikiza chuki miongoni mwa watanzania na mmekuwa gazeti la umbea, uzandiki, la kihuni na udaku.
P****** kabisa nyie habari leo!!
 
aliyeleta hii thread amenipotezea Appetite kabisa , mi niliisha acha kusoma hiki kijalida pamoja na vijigazeti vya rostam. Ni heri kusoma uhuru kuliko hili
 
Nashangaa kama makala hii imeandikwa kwenye gazeti la habari leo. Hivi kuna gazeti lililoandika habari za kuoa kwa Slaa kama habari leo? Nafikiri hata magazeti ya UDAKU yale ya Shigongo hayakuandika habari za kuoa kwa Slaa kama lilivyoandika gazeti hili. Ninashangaa kama hii leo gazeti hilo hilo linaweza kuchapisha makala ya kuwaasa wengine kuacha kufanya ambayo gazeti hili limekuwa pioneer wa kuyafanya hayo?

Wala usishangae ndugu yangu. Wanawaasa wengine kuacha kuandika kwa sababu wanajua kama yakiandikwa mambo binafsi ya ngono ya wagombea wengine wote basi mgombea wa Chadema ataonekana ni msafi.
 
habari leo wasubiri kimbunga ockoba, watajutaaaaa kuwa wandishi wa habari makanjanja.

Bagamoyo! Tamaa zenu ndiyo zinawafanya mjijengee ukuta kati ya Watanzania wenzenu na nyie, mnakiuka maadili ya kazi zenu, mnaandika/mnatenda bila kufikiri jambo. Hamfanani na watanzania walio na shida za maisha, wanaoishi chini ya dola moja kwa siku, wanaokula mlo mmoja kwa siku. Mnataka short cut za maisha kwa kuiga. Hivi mtu ukiamua kuandika ukweli wenye kujenga jamii utakufa? I hate HabariLeo nowdays kwa sababu ya unprofessional/misconduct of your professional ethics.
 
Back
Top Bottom