MAKALA: Mambo muhimu ya kuzingatia kuhusu kodi kwa mtu anayeanza biashara

Afrolink-Tz Consult Ltd

JF-Expert Member
Feb 25, 2018
420
939
MUHIMU: UPDATE
MABADILIKO YA VIWANGO VYA KODI NA MENGINEYO KUANZIA MWAKA WA FEDHA 2019/2020

Katika makala hii ya kodi, sehemu ya pili kuna mabadiliko ya viwango vya kodi ambavyo vimerekebishwa ukilinganisha na mara ya kwanza ya uwasilishaji wa mada. Vlvl uandaaji wa hesabu za mizania kwa mtu binafsi kun a mabadiliko pia. Pitia kwa faida yako na jamii pia

MAKALA: SEHEMU YA KWANZA
Habari zenu wanajukwaa
1. Utangulizi
makala hii inahusu masuala ya kodi kwa wanaoanza biashara lakini vilevile itagusa sheria na biashara kwa ujumla wake. lengo ni kuzidi kuelimishana kwa wasiofahamu na vilevile kukumbushana kwa wenye ufahamu na kuongezeana elimu kwa michango mbalimbali itakayoletwa kutoka kwa wanajukwaa.
2. Biashara na aina zake
Biashara ni kununua na kuuza, kuzalisha mali na kuuza, utaalmu, wito na makubaliano ya kipekee yenye nia ya kupata faida kwa kifupi ili nisiwachoshe.
kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya mwaka 2003 ya kuendeleza wajasiriamali wadogo, wa kati na wakubwa, biashara zimegawanyika katika makundi manne:
1. Biashara ndogo sana
Ina idadi ya waajiriwa kuanzia mmoja hadi wanne, na Mtaji wake ni kuanzia Sh 1 hadi 5mil

2. Biashara ndogo
Ina idadi ya waajiriwa 5 hadi 49, na mtaji wake ni kuanzia mil5 hadi mil 200

3. Biashara za kati
Ina idadi ya waajiriwa 50 hadi 99 na mtaji ni kati ya mil 200 hadi mil 800

4. Biashara Kubwa
Ina idadi ya waajiriwa zaidi ya 100 na mtaji zaidi ya mil 800.

Vingezo vingine vinavyotumika na Mamlaka ya Mapato kuweka madaraja ya walipa kodi ni kulingana na kiasi cha mauzo kwa mwaka au kiasi cha kodi kinacholipwa kwa mwaka

3. SHERIA ZA KODI
Shera hizi zinamgusa anaeanza biashara:
1. Sheria ya kodi ya mapato ya mwaka 2004
2. sheria ya kodi ya Ongezeko la thmani (VAT) ya mwaka 2014 kwa anefuzu kusajiliwa
3. Sheria ya ushuru wa stempu ya mwaka 1972
4. sheria ya usimamizi wa kodi ya mwaka 2015
Sheria hizi zinasimamiwa na Mamlaka ya Mapato (TRA) kupitia kodi za ndani

A: Sheria ya Kodi ya Mapato
Kodi ya mapato hutozwa kwa mtu ambaye mapto yake yanatokana na vyanzo mbalimbali km vilivyoainishwa ktk sheria kama vile
a) Biashara yoyote na kwa muda wowote inapofanyika
b) Ajira yoyote afanyayo mtu
c) Uwekezaji ktk rasilimali. Mfano nyumba, ardhi na hisa
d) Vyanzo vinginevyo vya mapato vya kutozwa kodi ya zuio "Final Withholding Tax. Mf: Kodi ya malipo ya pango, malipo ya gawio kutoka ktk kampuni kwa Mtz, Riba itokanayo na benki na malipo kutokana na maliasili (mrahaba)

B: Mapato yatokanayo na biashara
kwa mujibu wa sheria ya kodi ya mapato ya mwaka 2004 ikarejewa mwaka 2006, Mapato yanayotozwa kodi kutokana na biashara ni Faida au Ziada itokanayo na biashara kwa mwaka wa mapato. Mapato hayo ni pamoja na:
1. Faida kutokana na mauzo ya bidhaa au huduma za biashara
2. Malipo anayolipwa mfanyabiashara kwa masharti ya kufanya au kutofanya biashara kulingana na makubaliano ya upande wa pili
3. Zawadi au Takrima anazolipwa mfanyabiashara kutokana na shughuli zake za biashara
4. Kiasi cha mapatoyanayohusiana na biashara ambayo vinginevo yangekuwa mapato ya uwekezaji ktk rasilimali kwa mtu anayefanya biashara ya kupangisha nyumba`

Inaendelea.......
B: Taratibu za kufuatwa na mtu anaeanza biashara kupata namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN) pamoja na malipo ya kodi na mengineyo:

Mtu anaeanza biashara atatakiwa kuomba TIN kutoka TRA ambapo vielelezo hv vitahitajika
1. Fomu za maombi ya TIN kwa mtu binafsi (zinatolewa TRA)
2. Barua ya utambulisho wa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa (hutolewa na TRA)
3. Mkataba wa pango kwa aliepanga eneo la biashara au kielelzo cha umiliki wa eneo la biashara kama hati, ofa au karatasi za malipo ya kodi ya majengo
4. Kopi ya kitambulisho cha Taifa, Leseni ya udreva, paspoti ya kusafiria au kitambulisho cha kupigia kura
5. Picha ndogo ya paspoti saizi

Mhusika utaulizwa juu ya biashara yako "business assessment". baada ya hapo utaambiwa kiasi cha kodi utakayostahili kulipa kutokana na mauzo ya biashara unayofanya au unayotarajia kuifanya. baada ya maelezo haya taratibu nyingine zitaendele na hatimaye utapata TIN.
Kwa leo naomba tuishie hapa sehemu ya kwanza kutokana na majukumu. Tutaendelea sehemu ya pili
 
Habari zenu wanajukwaa
1. Utangulizi
makala hii inahusu masuala ya kodi kwa wanaoanza biashara lakini vilevile itagusa sheria na biashara kwa ujumla wake. lengo ni kuzidi kuelimishana kwa wasiofahamu na vilevile kukumbushana kwa wenye ufahamu na kuongezeana elimu kwa michango mbalimbali itakayoletwa kutoka kwa wanajukwaa.
2. Biashara na aina zake
Biashara ni kununua na kuuza, kuzalisha mali na kuuza, utaalmu, wito na makubaliano ya kipekee yenye nia ya kupata faida kwa kifupi ili nisiwachoshe.
kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya mwaka 2003 ya kuendeleza wajasiriamali wadogo, wa kati na wakubwa, biashara zimegawanyika katika makundi manne:
1. Biashara ndogo sana
Ina idadi ya waajiriwa kuanzia mmoja hadi wanne, na Mtaji wake ni kuanzia Sh 1 hadi 5mil

2. Biashara ndogo
Ina idadi ya waajiriwa 5 hadi 49, na mtaji wake ni kuanzia mil5 hadi mil 200

3. Biashara za kati
Ina idadi ya waajiriwa 50 hadi 99 na mtaji ni kati ya mil 200 hadi mil 800

4. Biashara Kubwa
Ina idadi ya waajiriwa zaidi ya 100 na mtaji zaidi ya mil 800.

Vingezo vingine vinavyotumika na Mamlaka ya Mapato kuweka madaraja ya walipa kodi ni kulingana na kiasi cha mauzo kwa mwaka au kiasi cha kodi kinacholipwa kwa mwaka

3. SHERIA ZA KODI
Shera hizi zinamgusa anaeanza biashara:
1. Sheria ya kodi ya mapato ya mwaka 2004
2. sheria ya kodi ya Ongezeko la thmani (VAT) ya mwaka 2014 kwa anefuzu kusajiliwa
3. Sheria ya ushuru wa stempu ya mwaka 1972
4. sheria ya usimamizi wa kodi ya mwaka 2015
Sheria hizi zinasimamiwa na Mamlaka ya Mapato (TRA) kupitia kodi za ndani

A: Sheria ya Kodi ya Mapato
Kodi ya mapato hutozwa kwa mtu ambaye mapto yake yanatokana na vyanzo mbalimbali km vilivyoainishwa ktk sheria kama vile
a) Biashara yoyote na kwa muda wowote inapofanyika
b) Ajira yoyote afanyayo mtu
c) Uwekezaji ktk rasilimali. Mfano nyumba, ardhi na hisa
d) Vyanzo vinginevyo vya mapato vya kutozwa kodi ya zuio "Final Withholding Tax. Mf: Kodi ya malipo ya pango, malipo ya gawio kutoka ktk kampuni kwa Mtz, Riba itokanayo na benki na malipo kutokana na maliasili (mrahaba)

B: Mapato yatokanayo na biashara
kwa mujibu wa sheria ya kodi ya mapato ya mwaka 2004 ikarejewa mwaka 2006, Mapato yanayotozwa kodi kutokana na biashara ni Faida au Ziada itokanayo na biashara kwa mwaka wa mapato. Mapato hayo ni pamoja na:
1. Faida kutokana na mauzo ya bidhaa au huduma za biashara
2. Malipo anayolipwa mfanyabiashara kwa masharti ya kufanya au kutofanya biashara kulingana na makubaliano ya upande wa pili
3. Zawadi au Takrima anazolipwa mfanyabiashara kutokana na shughuli zake za biashara
4. Kiasi cha mapatoyanayohusiana na biashara ambayo vinginevo yangekuwa mapato ya uwekezaji ktk rasilimali kwa mtu anayefanya biashara ya kupangisha nyumba`
Itaendelea.........
Itaendelea lini?
 
Inaendelea.....
MAKALA: SEHEMU YA PILI
Habari za leo
Tuendelee na makala yetu juu ya ulipaji kodi kwa mtu anaeanza kufanya biashara. Katika sehemu ya kwanza tumeangalia mambo mbalimbali kama sheria za kodi, mgawanyiko wa makundi ya biashara, namna ya kuomba TIN na vielelezo vinavyotakiwa ktk kuomba TIN kutoka TRA. Makala ya leo tutaangazia masuala mbalimbali kama ifuatavyo:

1. VIWANGO VYA KODI YA MAPATO
Kodi hii hulipwa kutokana na mapato ya biashara na vinatofautiana kulingana na pato la mtu. Kwa mujibu wa sheria ya kodi ya mapato jedwali na. 1 viwango vya kodi vimegawanyika ktk makundi matatu ambayo ni:
kundi la kwanza
Viwango vinavyowahusu wafanyabiashara wadogo wenye mauzo ghafi kuanzia mil 4 hayazidi mil 100 kwa mwaka. Hawa hutozwa kodi kutegemeana na mauzo yao ya mwaka.

Kundi la pili
Viwango vywa wafanyabiashara binafsi ambao mauzo ghafi kwa mwaka ni zaidi ya mil 100. Hawa hutozwa kwa kutegemea faida inayokokotolewa kulingana na kumbukumbu za biashara na hesabu za mizania

Kundi la tatu
Inahusisha makampuni, mashirika, vilabu, ushirika na taasisi zingine na kiwango cha kodi ni 30% ya faida iliyopatikana kwa mwaka

2. UTARATIBU WA KULIPA KODI
Ulipaji wa kodi ya mapato itokanayo na makisio "provison tax" hufanyika kwa awamu nne ambazo ni
Awamu ya kwanza
Kuanzia tarehe 1 Januari hadi 31 Machi

Awamu ya pili
Kuanzia tarehe 1 Aprili hadi 30 Juni

Awamu ya tatu
Kuanzia tarehe 1 Julai hadi 30 Septemba

Awamu ya nne
Kuanzia tarehe 1 Oktoba hadi 31 Disemba

Kuchelewa kulipa awamu yyt kati ya hizo penati yake ni Sh 225,000 kwa kila mwezi unaoongezeka toka awamu husika ipite

3. VIWANGO VYA KODI KWA WAFANYABIASHARA WADOGO WAKAZI
Kwa kuzingatia kifingu cha 35 cha Sheria ya usimamizi wa kodi (utunzaji wa kumbukumbu) kodi zimegawanyika kama ifuatavyo:
(Note: Mauzo ni kwa mwaka, Tsh)
1. Mauzo yasiyozidi mil 4
Hakuna kodi kwa asietunza na anaetunza kumbukumbu

2. Mauzo kati ya mil 4 hayazidi mil 7.0
a) Kwa asiyetunza kumbukumbu kodi atalipa sh 100,000
b) Kwa anaetunza kumbukumbu kodi atalipa 3% ya mauzo yanayozidi mil 4

3. Mauzo kati ya mil 7.0 hayazidi mil 11.0
a) Kwa asiyetunza kumbukumbu analipa sh 250,000
b) Kwa anaetunza kumbukumbu atalipa sh 90,000+3.0% ya mauzo yanayozidi mil 7.0

4. Mauzo kati ya mil 11.0 na hayazid mil 14
a) Kwa asiyetunza kumbukumbu atalipa sh 450,000
b) Kwa anayetunza kumbukumbu atalipa sh 230,000+ 4.0% ya mauzo yanayozidi mil 11.0

5. Mauzo zaidi ya mil 14 hayazid mil 100
a) Kwa asiyetunza kumbukumbu atalipa sh 450,000
b) Kwa anaetunza kumbukumbu kodi atalipa sh 450,000+ 3.5% ya mauzo yanayozidi mil 14

ZINGATIA KUWA:
1. Endapo mauzo ghafi kwa mwaka yatazidi mil 100 ni LAZIMA KUTENGENEZA HESABU ZA MIZANIA kulingana na biaahara
2. Mlipakodi ambaye mauzo ghafi kwa mwaka yanazidi mil 14 ANATAKIWA KUTUMIA MASHINE ZA KIELEKTRONIKI ZA KODI (EFD)
3. Mlipakodi mwenye mauzo chini ya mil 14 anatakiwa kutoa risiti ya kuandikwa kwa mkono zenye nakala zikionyesha TIN, Jina la Muuzaji, Jina la mnunuzi, aina ya bidhaa na thamani yake.
Hii ni kwa mujibu wa kifingu na. 36 (3&4) cha sheria ya usimamizi wa kodi

KOSA LA KUTOKUTOA RISITI YA KODI YA ELEKTRONIKI (EFD)
1. Kulipa faini kati ya mil 3 hado 4.5 au kifungo cha miaka mitatu jela
2. Kutozwa faini ambayo itakuwa mara mbili ya kodi iliyokwepwa
3. Kushindwa kudai risiti na hukutoa taarifa adhabu yake ni kati ya sh 30,000 hadi mil 1.5
Hivyo tujitahidi ukiuza TOA RISITI na UKINUNUA DAI RISITI.

ULIPAJI WA KODI YA MAKISIO NA MENGINEYO
Baada ya kupata bili yako ya kulipa kodi ya makadirio/makisio una muda wa siku 90 wa kujipanga kuilipa sehemu (robo ya jumla ya kodi yote). Hivyo basi
1. Utaomba Certificate of Tax Clearance ambayo itakufaa ktk kuombea leseni au vibali kwaujibu wa mahitaji yako.
2. Ili kuipata hii itakulazimu kulipa baadhi ya kodi km kodi ya zuio "withholding tax" ambayo ni 10% ya thamani ya kodi ya pango uliyolipa.
3. Utaulipia mkataba wako ushuru wa stempu ambao ni 1%
Ikumbukwe kama mkataba umechelewa kuasilishwa nje ya mwezi ule uliosainiwa, basi kuna adhabu. (Hili tutaangalia mbele)
Tutaendeleaaa...
 
Wasanii, mawakili, advisors, nk wanaotumia their knowledge or skills wanalipaje kodi?
Japo hili lipo mbele ya somo lkn ntajibu kwa ufupi.
1. Hawa watu wa kada zenye utaalam wanalipa kodi kama biashara yoyote nyingine. Wanawasilisha makisio ya kulipa kodi "provision tax" mwanzo wa mwaka

2. Vlvl katika masuala ya kodi, zile kazi za utaalamu km washauri, wakili nk kwa sheria ya kodi ya ongezeko la thamani inawalazimu kusajili VAT, watakuwa wanawasilisha mahesabu yao ya VAT kabla au kila tarehe 20 ya kila mwezi. Hii ni lazima sio mpk mauzo yawe mpaka mil 100 kama biashara nyinginezo
 
Kuna kitu inaitwa Withholding Tax (WHT)
hawa watu wanaangukia hii category
Japo makala mbele nitajibu
Withholding tax ni kodi ya zuio kwa mnufaikaji ambayo anatakiwa kulipa kwa 10% ndani ya muda toka kusainiwa kwa mkataba (case study ya mpangaji na mpangishaji)

Kodi hii wanalipa pia kama na kama tu wamepanga eneo la kuendeshea shughuli zao. Kodi hii inatakiwa mpangishaji alipe TRA kutoka ktk malipo ya mkataba wa pango kwa muda wa mpangaji aliopanga. Ss wapangishaji wengi (wamiliki wa nyumba/maeneo ya biashara) huwa wanazingua kuilipa ndiyo maana ukienda unalipa wewe kwa niaba yake. Inapaswa UMKATE Kile kiasi ulichomlipia TRA ktk kodi au gharama zozote ambazo atakwambia kulipia, muhimu mpe risiti yake ya malipo
 
Japo makala mbele nitajibu
Withholsing tax ni kodi ya zuio kwa mnufaikaji ambayo anatakiwa kulipa kwa 10% ndani ya muda toka kusainiwa kwa mkataba (case study ya mpangaji na mpangishaji)

Kodi hii wanalipa pia kama na kama tu wamepanga eneo la kuendeshea shughuli zao. Kodi hii inatakiwa mpangishaji alipe TRA kutoka ktk malipo ya mkataba wa pango kwa muda wa mpangaji aliopanga. Ss wapangishaji wengi (wamiliki wa nyumba/maeneo ya biashara) huwa wanazingua kuilipa ndiyo maana ukienda unalipa wewe kwa niaba yake. Inapaswa UMKATE Kile kiasi ulichomlipia TRA ktk kodi au gharama zozote ambazo atakwambia kulipia, muhimu mpe risiti yake ya malipo
Good! Nmekupata 100%, thank you
 
Back
Top Bottom