Makala kwenye magazeti ya Tanzania...mnisaidie!!

Stv Mkn

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
244
225
Ndugu zangu,mimi ni muhandishi ninaechipukia wa makala za kijamii,kisiasa na kiuchumi..Nimetayarisha makala zangu ambazo nataka zisomwe na umma kupitia magazeti yetu hapa nchini..

Ombi langu......
1) Naomba kujuzwa ni namna gani naweza kupata nafasi ya kuchapiwa makala zangu gazetini.
2) Ni mchakato gani niufuate kuweza kupewa iyo nafasi ya makala zangu.
3) Ni vitu gani nizingatie ili kuandika makala bora inayoweza kuvutia wasomaji wengi.
4) Kuna maslahi yoyote ya kifedha nayoweza kuyapata endapo makala zangu zitapata nafasi gazetini?
5) Nakalibisha pia chochote unachoweza kunishauri kuhusu ili wazo.

Asanteni!!

cc Pasco Mzee Mwanakijiji Mohamedi Mtoi Yericko Nyerere Mtambuzi Mchambuzi Manyerere Jackton na wengineo wote.
 
Last edited by a moderator:

Yericko Nyerere

Verified Member
Dec 22, 2010
16,807
2,000
Kama upo Dar njoo posta, ulizia mtu yeyote akuonyeshe klabu ya bilikanasi, ukifika mapokezi waambie unakwenda freemedia wachapishaji wa gazeti la Tanzania Daima, hapo shida zako zote zitatatuliwa bila wewe kutoa malipo bali utalipwa,

NB

Ni mwandishi na sio muhandishi,
 
Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
6,236
2,000
Duh anza kuandika makala kwanza uzirushe hapa then tujue uwezo wako ndyo tutakushauri vizuri.
 
Chen Hu

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
3,514
2,000
Kwa maandishi mafupi namna hii umeshaharibu lugha mara 2 yaani

MUHANDISHI na NAKALIBISHA.
Sasa ukiandika makala yenye aya 50 si utatuulia kiswahili chetu?
 
Dec 11, 2010
3,322
0
Ndugu zangu,mimi ni muhandishi ninaechipukia wa makala za kijamii,kisiasa na kiuchumi..Nimetayarisha makala zangu ambazo nataka zisomwe na umma kupitia magazeti yetu hapa nchini..

Ombi langu......
1) Naomba kujuzwa ni namna gani naweza kupata nafasi ya kuchapiwa makala zangu gazetini.
2) Ni mchakato gani niufuate kuweza kupewa iyo nafasi ya makala zangu.
3) Ni vitu gani nizingatie ili kuandika makala bora inayoweza kuvutia wasomaji wengi.
4) Kuna maslahi yoyote ya kifedha nayoweza kuyapata endapo makala zangu zitapata nafasi gazetini?
5) Nakalibisha pia chochote unachoweza kunishauri kuhusu ili wazo.

Asanteni!!

cc Pasco Mzee Mwanakijiji Mohamedi Mtoi Yericko Nyerere Mtambuzi Mchambuzi Manyerere Jackton na wengineo wote.

Mkuu.

Tofauti na nchi za wenzetu huku Bongo sisi huwa tunajiandikia tu, kila anaye kurupuka usingizini anataka kuanda makala itoke gazetini lakini ukweli ni kwamba lazima tuige utamaduni wa nchi za wenzetu walioendelea. Kuandika iwe kwa waledi (professionalism), Yaani ifike hatua kama ni kuhusu elimu basi makala hayo yaandikwe na mtaalamu wa elimu aliyefanya tafiti za kutosha kwenye angle anayotaka kuandikia, halika dhalikwa kwenye uchumi, afya, mazingira nk.

Linapokuja swala la kuandikia mambo ya kisiasa basi awe mtu aliyebobea kwenye chambuzi za mambo ya kisiasa na anayejua vyema situation kwenye nchi yake na mbobezi wa taaluma ya siasa. Makala za watu nilio wataja hapo juu utatamani kuzisoma kila kukicha.

Cha kufanya kabla hujafikiria kupeleka makala zako.

1. Jipime ujue wewe una uwezo wa kuandika kwenye eneo gani.

2. Hakikisha unajua kufanya angalau ka-utafiti ili ukiandika ujue una kuja na ladha gani tofauti itakayo mvutia msomaji wako.

3. Andika kwenye chombo unacho jua mlengo wake na yajue mapema maslahi utakayo pata, usije ukawa na ndoto kubwa kuwa utalipwa vizuri kumbe makala ikitoka unalipwa elfu 10 gazeti linatoka mara moja kwa juma huku ukiwa umetumia nguvu nyingi na wakati mwingine unajikuta unakopwa. Kama unataka kuandika makala ili ujikimu ki maisha anza kujitafakari upya na andika kama hobi tu.

4. Hakikisha ukiamua kuandika uamue sawasawa na ukiandika ushike kalamu yako vizuri bila kutetereka hasa unapo simamia ukweli. Mimi kuna gazeti moja nilisha wahi kutuma makala yenye utafiti wa kina juu ya serikali kumwaga damu za raia wasio kuwa na hatia toleo liliofuata haikutoka, nikapata ka ujumbe "... Makala yako ni nzuri sana lakini gazeti linaweza kufungiwa..." Waliogopa gazeti litafungiwa kwa kusema ukweli, yaani ili lisifungiwe uandike kinyume chake.

Wakatabahu
 
Daddo

JF-Expert Member
Jan 17, 2013
1,411
2,000
Kwa maandishi mafupi namna hii umeshaharibu lugha mara 2 yaani

MUHANDISHI na NAKALIBISHA.
Sasa ukiandika makala yenye aya 50 si utatuulia kiswahili chetu?

Kama nisingeona huu mchango wako basi ingenilazimu niandike hivyo.
 
Manyerere Jackton

Verified Member
Dec 11, 2012
2,425
2,000
Ndugu zangu,mimi ni muhandishi ninaechipukia wa makala za kijamii,kisiasa na kiuchumi..Nimetayarisha makala zangu ambazo nataka zisomwe na umma kupitia magazeti yetu hapa nchini..

Ombi langu......
1) Naomba kujuzwa ni namna gani naweza kupata nafasi ya kuchapiwa makala zangu gazetini.
2) Ni mchakato gani niufuate kuweza kupewa iyo nafasi ya makala zangu.
3) Ni vitu gani nizingatie ili kuandika makala bora inayoweza kuvutia wasomaji wengi.
4) Kuna maslahi yoyote ya kifedha nayoweza kuyapata endapo makala zangu zitapata nafasi gazetini?
5) Nakalibisha pia chochote unachoweza kunishauri kuhusu ili wazo.

Asanteni!!

cc Pasco Mzee Mwanakijiji Mohamedi Mtoi Yericko Nyerere Mtambuzi Mchambuzi Manyerere Jackton na wengineo wote.

Karibu sana. Njoo Mtaa wa Samora, Dar es Salaam; Jengo la Matasalamat. Ofisi za Jamhuri. Utapata majibu kwa maswali uliyouliza. karibu sana. Hii taaluma haihitaji kuwa mchoyo. Njoo upate ya kukusaidia kufikia malengo na matamanio yako.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom