Makala inayofichua nafasi ya Israel katika vita dhidi ya Yemen kurushwa hewani

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,990
17,877
Makala inayofichua nafasi ya Israel katika vita dhidi ya Yemen kurushwa hewani

Msemaji wa Vikosi vya Yemen amesema makala tarishi ya kufichua nafsi ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika vita dhidi ya Yemen vilivyoanza tokea Machi 25 mwaka 2015 itarushwa karibuni hivi.

Brigedia Jenerali Yahya Saree amesema hayo katika ujumbe aliotuma kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter na kuongeza kuwa, filamu hiyo ya matukio ya kweli yenye anuani isemayo "Jasusi wa Israel nchini Yemen" itarushwa hewani ndani ya siku chache zijazo.

Amebainisha kuwa, mbali na kuonesha mkono wa utawala haramu wa Israel katika vita hivyo, lakini makala hiyo pia itafichua uovu na njama nyingine za siri za Tel Aviv katika mgogoro wa Yemen.

Filamu hiyo ya matukio halisi inakuja katika hali ambayo, duru za habari zilifichua hivi karibuni kuwa, utawala khabithi wa Israel unashirikiana na Umoja wa Falme za Kiarabu kwa ajili ya kuunda kituo cha kijasusi katika visiwa vya Yemen.

Harakati ya Ansarullah ya Yemen imekuwa ikisisitiza kuwa, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu ziliishambulia Yemen katika fremu ya kutekeleza njama za Marekani na Utawala wa Kizayuni wa Israel katika eneo la Asia Magharibi (Mashariki ya Kati).

Mwezi Machi 2015, Saudi Arabia ikiungwa mkono na Marekani, Imarati na nchi zingine kadhaa iliivamia kijeshi Yemen na kuiwekea mzingiro nchi hiyo wa nchi kavu, baharini na angani ambao unaendelea hadi sasa.
 
Yemen nao wanalialia kwa nani awasikilize wafuasi wa Ayatollah ni Magaidi.. so wacha nchi jirani zijilinde ni haki yao...
 
Back
Top Bottom