Makala: Hatuwezi kumaliza rushwa bila kulinda mashahidi

wanzagitalewa

Senior Member
Jan 25, 2018
128
84
DRokuhPXkAEjXN4.jpg
Mahakama ya Rufaa nchini

TAKUKURU imetajawa na hofu kubwa kutokana na idadi ya kesi inazopoteza mahakamani dhidi ya watuhumiwa wa rushwa. Sababu kubwa wanayotoa ni kwamba, mashahidi wanahofia kusema ukweli wanaposimamishwa mbele ya mahakama kwa ajili ya kutoa ushahidi.

Kuhusika katika tukio la rushwa kunaweza kukusababishia msongo wa mawazo, na kukuacha wewe bila kujua nini cha kufanya mbeleni. Na haishangazi kuona kwamba, hofu juu usalama wa mtu unasababisha mashahidi kuogopa kutoa ushahidi.

Watu wanahofia kuwa, watu hawa wenye uwezo mkubwa wa kifedha watawafanya nini endapo watatoa ushahidi kuwa walihusika katika vitendo vya rushwa.

Watu wanaojihusisha na vitendo vya rushwa hushirikiana katika kuhakikisha kwamba maslahi yao yanafanikiwa. Kutokana na ushirikiano huo wanaoujenga, unapelekea wangine waliopo nje ya mahakama kuwazuia mashahidi wanaotaka kwenda kutoa ushahidi.

Tufahamu kwamba, TAKUKURU hawaweza kumfungulia mtu mashtaka ya rushwa, ila pale tu wanapokuwa na ushahidi wa kutosha kwamba mtu huyo ametenda kosa. Changamoto kubwa katika mahakama ni kwamba tuhuma za rushwa zinatakiwa kuthibitishwa kiuhakika (beyond reasonable doubt). Mashahidi wafahamu kuwa wanafanya kitu kilicho sahihi kwa kuonyesha namna watu hawa wanajihusisha na vitendo vya rushwa.

Rais, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mahakama wanafahamu kuhusu njama hizi zinazofanywa na watuhumiwa wa rushwa. Kwa pamoja wanataka kuhakikisha kwamba, mashahidi wanakuwa na uhakika na usalama wa maisha yao wanapotoa taarifa kuhusu makosa haya. Hii ni hatua ambayo lazima ichukuliwe ili kuweza kushinda vita hii dhidi ya rushwa.

Katika Makala iliyopita tulijadili mbinu zinazotumiwa na watuhumiwa wa rushwa katika kuchelewesha utendekaji wa haki, kwa kukuza mambo yanayohusiana na afya zao kila mara wakifika mahakamani. Watu hawa wanatumia utajiri na uwezo walionao kushindana na mahakama.

Sethi, Rugemalira na Manji, niwataje tu wachache, wana uwezo wa kutishia mashahidi lakini hawana uwezo wa kuitishia dola, hasa pale ambapo dola itaamua kuhakikisha usalama wa mashahidi wanaotoa taarifa au ushahidi dhidi ya vitendo vya rushwa.

Serikali imeipa TAKUKURU mamlaka na uwezo unahotajika kuhakikisha inashinda vita dhidi ya rushwa. Kuwalinda mashahidi na waathirika wa rushwa, lazima liwe miongoni mwa masuala wanayoyachukulia kwa uzito mkubwa. Kuendesha kesi za rushwa, ni lazima uwe na mashahidi wa kweli mbalimbali na wenye uwezo wakujieleza.

Sina tone la shaka kwa namna TAKUKURU wanavyoshughulika na kesi za rushwa na uhujumu uchumi, lakini ni lazima wapige hatua ya ziada na kutoa usaidizi kwa wale wote wanaofanikisha shughuli zao.

Kila mmoja kwatika jamii ana nafasi ya kufanya kuhakikisha rushwa inatokomezwa kwa manufaa mapana ya taifa. Inatakiwa kuwa utamaduni wetu kuzungumza punde tu tunapooona kuna kosa linafanyika sehemu.

Botswana na Rwanda zimefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kupunguza rushwa. Nchi hizi zimefikia hatua hiyo ya kuridhisha kutokana na ulinzi uliowekwa kwa watu. Watuhumiwa wa rushwa wanafahamu kabisa kwamba, jamii haiwezi kuwaacha endapo watafikishwa mahakamani, hivyo wengi hujiepusha na vitendo vya rushwa.

Rushwa huinyima jamii haki yake, na endapo jamii itaendelea kukaa kimya kwenye makossa haya, ni kwamba watakuwa wakiendelea kunyonywa na wachache wenye uwezo.

Ombi langu kwa Rais, fanya lolote liwezekano kuwalinda wote wanaojitokeza kutoa ushahidi dhidi ya watuhumiwa wa rushwa, kwani watu hawa ndio wataweza kulikomboa taifa dhidi ya rushwa.

Shani Kimweri

Chuo Cha Usimamizi wa Mahakama Lushoto
 
Classic material right there!

Na serikali ilivyo ya kiduwanzi haifati kitu hii kamwe!Tumelogwaaaa!
 
Back
Top Bottom