Makala fupi kuhusu Aliens na story ya mapenzi ni maua

scryberryder

New Member
Mar 17, 2019
0
4
Alien ni nani?
Alien ni Mgeni wa anga (Alien / Extraterrestrial)
Mgeni asiye wa dunia hii, au mgeni wa anga ya nje, ni kiumbe ambacho hakitoki Ardhi. Bunilizi ya kisayansi mara nyingi huwachora wageni wa anga wakiwa na umbo la binadamu au reptilia, ngozi ya kijani-kijivu na kichwa kikubwa chenye umbo la kitunguu, pamoja na viungo vinne. Asili yao kuu ya ubadilishaji ni vyombo vya anga ambavyo vinaweza kusafiri kwa kasi ya kupotosha. Pia wao hujulikana kutengeza miviringo ya mazao, kuwateka binadamu kwa kuwainua ndani ya meli yao kwa mwale wa kusafirisha na kuchunguza kwa undani mapengo ya mwili.

Mbari za wageni wa anga, kama vile wadudu wa anga, zina uwezo wa kutia mimba mwenyeji kwa yai na wakati kiini tete kimekua, mwenyeji huwa sisimizi wa anga au buibui. Katika makunda wao, hutumia “akili ya mzinga” na kupitisha kumbukumbu kwa wenyeshi wao.

Aina za Aliens
1. _Flatwoods monster_ hawa Ni warefu wanene wana vichwa venye shape ilichongoka juu Kama mkuki. Kwenye story yetu ya mapenzi ni maua kwa wale wasomaji wangu naweza nikawaambia kwamba goro ni aina hii ya Alien.
2. _Greys_ hawa wana rangi ya kijivu na urefu Wa futi 3-4, macho yao yamepanda juu kidogo alaf yamechongoka, hawana pua ila wana matundu ya pua, wana vidole 3-4 (Dole gumba wanalo), wana mdomo ila hawana maskio. Kwenye story yetu ya mapenzi ni maua aliens Wa aina hii ni mapolisi. (Kwa wale wasomaji wangu Wa story wanaelewa nadhani)
3. _Hopkinsvillegoblin_ hawa wana maumbo madogo, wana rangi ya kijani na silver na wana maskio marefu yamepanda juu. Kwenye story yetu ya mapenzi ni maua aina hii ya aliens ni walinzi Wa kasri LA mfalme qasisi (wasimaji wangu wananielewa)
4. _Little green men_ hawa wana rangi ya kijani na wana maumbo madogo na hawana maskio ila wana mapembe madogo juu ya vichwa vyao ambavyo vipo Kama vya binadamu. Kwenye story ya mapenzi ni maua hawa ni walinzi pia.
5. _Nordic/Aryan Aliens_ hawa wapo Kama binadamu ni warefu Kama binadamu, wana nywele za brown na macho ya blue. Katika jamii ya Aliens hawa ndo wanaheshimika Sana na wengi wao ni viongozi japo kuna ambao sio viongozi ni wanafanyakazi Kama wengine. Mfano katika story ya mapenzi ni maua, mfalme Qasis na familia yake ni aina hii ya aliens na viongozi wengi aliowachagua walikua katika jamii hii akiwemo waziri mkuu hamdan na familia take. Vile vile hanim japo alikua ni mfanyakazi ila alikua katika aina hii ya aliens na hii ndomana ikapelekea kupendwa na kheiran kwakua ni aina moja
6. _Reptilians_ hawa wapo miili yao ina fanana na mijusi ila wao ni warefu Kama binadamu ila wana vichwa Kama mijusi na wana nguvu sana na wanatisha. Katika story yetu ya mapenzi ni maua hawa wapo katika kikosi maalumu cha jeshi LA Emired na ndo wanahusika na ulinzi Wa mfalme na familia yake.

Makala hii imendaliwa na kuandikwa na Scryber ryder
rayhosn@yahoo.com
+255627923380
download.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom