Makala: CCM IMECHOKA INATUCHOSHA NA MIMI NA WEWE NA SISI, IPUMZISHWE

Karibuni masijala

JF-Expert Member
Sep 13, 2012
409
135
Kuna kila sababu sasa ya kukipumzisha. Kimechoka na kinatuchosha tena Kimezeeka na kukiendekeza ni kufanya mzaha na Taifa hili. Kwani katika uzee wake kimekuwa legelege na hakina mikakati, iwe ni ya kukinusuru au kuinusuru nchi hii na matatizo yake. Kinajiendea kwa mazoea na sasa kuna dalili zote kinachapa mwendo kuelekea kaburi lake la kisiasa.

Kwa sasa hivi kimesambaratika mapande mapande. Mapande mengine yakishikiliwa na nguvu ya dola kwani bila vyombo vya mabavu haiwezi kufika hata kesho. Kwani kinabebwa ili kifanye siasa, lakini hakibebwi kutatua matatizo yetu ya kweli ya Taifa letu. Hivyo tunahitaji chama mbadala na ninaweza kusema hata kama ni kujaribu kingine wacha tujaribu tu. Liwalo na Liwe.

Hatuwezi kuendelea na watu wale wale waliotuangusha miaka nenda rudi, kimeshindwa kujipanga kujana mikakati ya kuikwamua nchi tunachokiona ni mikakati binafsi ya kuchukua madaraka. Na sasa mambo hayendi.

Nikupe nafasi nawe kuchangia kama nawe umechoshwa na chama hiki au hujachoshwa maana kuna wachache wananufaika nao ni huru kuchangia kwa hoja ili nasi tuwaelewe. Makala
 
Mwenyekiti wa hilo chama lao yuko busy kutuma salamu za rambirambi atajenga chama na nchi saa ngapi.
 
hili alilijua mapema au baada y kukatwa jina ujumbe wa nec
 
Ningekaa kimya kama mchosho wake usingeadhiri ambao sio wanachama au Taifa umekuwa too much ukanichosha mimi na hata wewe kuchoka kidole nalo neno unachoshwaje na chama vidole heri ungesema mkono ndio nimeutumia kwani nimeandika kwakutumia vidole au mkono.

Naaomba hoja wewe ambaye hakijakuchosha kama Wazee wa Africa mashariki mafao, Ahadi za kigoma kuwa kama Dubai, maisha bora kwa kila mtanzania, kilimo kwanza, Uchaguzi huru kwenye hata Jumuiya zake na mwishoa Vua gamba wanachama hawana hamu kusikia waliyoaminishwa na hata Watanzania
kwa alieandika hii makala, kama kweli unahamu ya kupumzisha kitu, basi ungevipumzisha vidole vyako badala ya kuvichosha kwa kuandika upuuzi.
 
Kuna kila sababu sasa ya kukipumzisha. Kimechoka na kinatuchosha tena Kimezeeka na kukiendekeza ni kufanya mzaha na Taifa hili. Kwani katika uzee wake kimekuwa legelege na hakina mikakati, iwe ni ya kukinusuru au kuinusuru nchi hii na matatizo yake. Kinajiendea kwa mazoea na sasa kuna dalili zote kinachapa mwendo kuelekea kaburi lake la kisiasa. Kwa sasa hivi kimesambaratika mapande mapande. Mapande mengine yakishikiliwa na nguvu ya dola kwani bila vyombo vya mabavu haiwezi kufika hata kesho. Kwani kinabebwa ili kifanye siasa, lakini hakibebwi kutatua matatizo yetu ya kweli ya Taifa letu. Hivyo tunahitaji chama mbadala na ninaweza kusema hata kama ni kujaribu kingine wacha tujaribu tu. Liwalo na Liwe. Hatuwezi kuendelea na watu wale wale waliotuangusha miaka nenda rudi, kimeshindwa kujipanga kujana mikakati ya kuikwamua nchi tunachokiona ni mikakati binafsi ya kuchukua madaraka. Na sasa mambo hayendi. Nikupe nafasi nawe kuchangia kama nawe umechoshwa na chama hiki au hujachoshwa maana kuna wachache wananufaika nao ni huru kuchangia kwa hoja ili nasi tuwaelewe. Makala
Hata CDM kuna mvurugano wa hali ya juu,huko pia kuna kambi 3 na zinapigana vijembe humu JF. sasa kama hivi vyama viwili vimechemsha basi nani ashike nchi? Mimi naona bora wapewe Mods wa JF waongoze hii nchi.
 
Inawezekana CCM ikawa imechoka lkn sikubaliani na hili kwa asilimia mia mmoja, nachoweza kusema CCM inachoshwa na uongozi dhaifu wa baadhi ya viongozi wake ktk kusimamia utekelezaji wa ilani.

Kuna viongozi wachache bado wanafanya vizuri sana, ukimuangalia Mwakyembe, Magufuli, Tibaijuka, waziri wa nishati utaona bado ccm ina majembe mengi.

Kiukweli mkiti wa chama ambaye pia ni rais ndiye anasababisha chama kionekane kimechoka. Bado siamini kama chadema wanauweza wa kuongoza nchi, ila nakubali kazi yake ni nzuri kukipa changamoto chama tawala
 
Mkuu kiukwel tunahitaji chama chenye vision na mission yenye viongozi makini wenye kusimamia maslahi ya wana wa nchi na si vingine! Bila shaka ni CDM hata JK analifahamu hilo
 
Back
Top Bottom