Makahaba Wanaaminika Zaidi nchini China Kuliko Wanasiasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makahaba Wanaaminika Zaidi nchini China Kuliko Wanasiasa

Discussion in 'International Forum' started by Bikra, Aug 6, 2009.

 1. Bikra

  Bikra Senior Member

  #1
  Aug 6, 2009
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 103
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Wananchi wa jamhuri ya China wana imani zaidi na makahaba wa nchini humo kuliko wanasiasa na maafisa wa serikali, kwa mujibu matokeo ya utafiti uliofanywa hivi karibuni nchini humo.
  Matokeo ya utafiti uliofanywa nchini China ukishirikisha zaidi ya raia 3000 wa China, yameonyesha kwamba makahaba nchini humo wanaaminika zaidi kuliko watu wanavyowaamini wanasiasa, maafisa wa serikali na wanasayansi.

  Watu 3,376 nchini China walishiriki kwenye utafiti huo na walionyesha kuwa na imani zaidi na makahaba kuliko wanasiasa na wanasayansi.

  Makahaba walishika nafasi ya tatu wakiwa nyuma ya viongozi wa dini na wakulima, jarida la Insight China lilitoa ripoti ya utafiti huo kwenye tovuti yake.

  "Matokeo ya utafiti huu yanashangaza na yanahuzunisha" lilisema gazeti la China Daily kuhusiana na ripoti ya utafiti huo uliofanyika mwezi juni na julai.

  "Makahaba nao kuhesabika watu wanaoheshimika zaidi ya wanasiasa na wanasayansi ni jambo lisilo la kawaida" lilisema gazeti hilo.

  Wanajeshi na wanafunzi nao walikuwa chini ya makahaba katika orodha iliyotolewa ya watu wanaoheshimika.

  "Kwa kuangalia maskendo yanayotokea kila wakati yakiwahusisha viongozi wa serikali, si ajabu matokeo ya utafiti kuonyesha hali hii" lilisema gazeti la China Daily.
   
 2. G

  Gashle Senior Member

  #2
  Aug 7, 2009
  Joined: Mar 30, 2007
  Messages: 116
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Bora hata huko Uchina ambapo tumesikia mara kwa mara wanasiasa wakikamatwa wanakula rushwa wanahukumiwa vifo...maskini Tanzania, ni aibu hata kuuliza kama wanasiasa wa Tanzania wanaaminika ama la! Utamu unakujua pale wanazuoni nao wanapoona academic hailipi na kuamua kujitosa kwenye siasa, njia ya mkato na ya kilaghai ya ku make it!

  Mungu ibariki Africa, Mungu ibariki Tanzania
   
Loading...