Makahaba Waenda Mahakamani Baada ya Kugundulika Wana Ukimwi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makahaba Waenda Mahakamani Baada ya Kugundulika Wana Ukimwi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Nov 15, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 15, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"][/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #e1e1e1"]
  [TD] [​IMG][/TD]
  [TD] Monday, November 14, 2011 8:35 AM
  Makahaba 14 wa nchini Malawi ambao walikamatwa na polisi na kulazimishwa kupimwa ukimwi na kugundulika wote wameathirika na ugonjwa huo, wameenda mahakamani kuishtaki serikali kwa kukiuka haki zao za msingi za kutokulazimishwa kupima ugonjwa huo.[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"] Makahaba 14 wa nchini Malawi ambao walikamatwa mitaani wakiiuza miili yao na kulazimishwa kupimwa kama wameathirika na ugonjwa hatari wa HIV, baada ya kugundulika wote wameathirika na matokeo yao kuwekwa hadharani, makahaba hao wameamua kwenda mahakamani kuishtaki serikali.

  Makahaba hao walikamatwa na polisi kwenye mji wa Lilongwe mnamo mwaka 2009 na walifikishwa mahakamani ambako matokeo yao yalianikwa wazi mbele ya hakimu na watu waliohudhuria kesi hiyo ambapo walishtakiwa kwa makosa ya kuiuza miili yao huku wakijua fika kuwa wameathirika.

  Waliachiwa huru baada ya kupigwa faini ya kwacha 1200 ambazo ni sawa na Tsh. 12,000.

  Awali madai yao hayakuruhusiwa kufikishwa mahakamani lakini baada ya miaka miwili kupita huku wakipewa tafu na mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini Malawi na yale ya kimataifa, wanawake hao wameenda mahakamani wakiishtaki serikali kwa kuvunja haki zao za msingi za kuwa na hiari ya kukubali kupimwa HIV au la.

  Makahaba hao walisema kuwa kinyume cha sheria walipimwa kinguvu kama wameathirika na pia matokeo yao yalitangazwa wazi na hivyo kukiuka haki zao za msingi na utu wao kutothaminiwa.

  Kesi hiyo imepangwa kuanzwa kusikilizwa disemba 14 mwaka huu.

  Takwimu zilizotolewa zimeonyesha kuwa asilimia kati ya asilimia 70 hadi 80 ya makahaba nchini Malawi ni waathirika wa HIV.

  Asilimia 13 ya raia wa Malawi wapatao milioni 13 ni waathirika wa virusi vya HIV vinavyosababisha ukimwi.

  Malawi ni mojawapo ya nchini zenye kiwango kikubwa cha waathirika wa HIV duniani, kila mwaka watu 90,000 huambukizwa ugonjwa huo wengi wao wakiwa ni vijana wenye umri mdogo na wanawake.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  Chanzo: Makahaba Waenda Mahakamani Baada ya Kugundulika Wana Ukimwi
   
 2. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #2
  Nov 15, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Way to go Makahaba

  Sio kwa sababu tu ni makahaba basi haki zao za msingi zikiukwe. Wawashitaki na ikiwezekana walipwe fidia
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  Nov 15, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Nawaunga mkono hao makahaba.

  Mambo gani hayo ya kulazimishwa kupima Ukimwi!
   
 4. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #4
  Nov 15, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  This is definitely going to shake em' up..... Sad.
   
Loading...