Makahaba Kuvaa Vizibao Vya Njano Ili Waonekane Vizuri

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,385
Makahaba Kuvaa Vizibao Vya Njano Ili Waonekane Vizuri
5069678.jpg

Makahaba wakiwinda wanaume nchini HispaniaThursday, October 28, 2010 1:23 AM
Makahaba wa nchini Hispania wanaowinda wanaume pembeni ya barabara wameanza kuvaa vizibao vya njano vinavyoakisi mwanga ili waweze kuonekana vizuri.Ili kuepuka faini ya euro 40, makahaba katika mji wa Els Alamus kaskazini mwa Hispania wameanza kufuata masharti ya serikali ya kuvaa vizibao vya njano vinavyoakisi mwanga.

Meya wa mji huo aliamuru makahaba wote wanaosimama pembeni ya barabara kuwinda wanaume wavae vizibao hivyo ili kuwafanya waonekane vizuri na hivyo kuepusha kutokea kwa ajali.

Taarifa ya meya wa mji huo ilisema kuwa baadhi ya makahaba wameanza kuvaa vizibao hivyo baada ya polisi kuanza kuwatoza faini ya euro 40 makahaba wanaosimama pembeni ya barabara kuu kuwinda wateja.

Nchini Hispania kuna jumla ya wanawake laki tatu wanaofanya biashara ya ukahaba. Mwanamke anaruhusiwa kisheria kufanya ukahaba nchini Hispania ingawa kujinufaisha kwa kuwatafutia makahaba wateja ni kinyume cha sheria.

Ni jambo la kawaida katika miji mbalimbali nchini Hispania kuwaona wanawake wanaovaa nguo fupi sana wakiwa wamesimama pembeni ya barabara wakitafuta wanaume.

Utafiti uliofanywa hivi karibuni nchini Hispania ulionyesha kuwa mwanaume mmoja kati ya wanne nchini Hispania ameishawahi kununua penzi toka kwa kahaba.
chanzo:nifahamishe
 
Na huku kwetu wavae nyekundu ili kurahisisha kuona hatari mbele yako.
 
Maendeleo, hawa ndio wenzetu wanaokubali sex workers have the rights and should have the labour card and pay tax!
 
uku kwetu wavae shanga za kijani ....zinaakis mwanga!!!!
mwee hatar yan mpk serikali pia inasimamia show izi?mungu wangu hatarrrrrrrrrrrrrrrrrr!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom