Makahaba 40,000 Kwenda Afrika Kusini Wakati wa Kombe la Dunia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makahaba 40,000 Kwenda Afrika Kusini Wakati wa Kombe la Dunia

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by MziziMkavu, Mar 8, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Monday, March 08, 2010 12:15 AM
  Makahaba wapatao 40,000 toka nchi mbalimbali duniani wanatarajiwa kuingia nchini Afrika Kusini wakati wa kombe la dunia litakalofanyika nchini humo baadae mwaka huu. Wanawake wapatao 40,000 wanatarajiwa kuingia nchini Afrika Kusini kufanya kazi ya ukahaba wakati wa mwezi mmoja wa kombe la dunia ambalo litafanyika baadae mwaka huu nchini humo.

  Afrika Kusini inaongeza ulinzi kwenye mipaka yake ili kuzuia wimbi hilo la makahaba ambao wengi wao wanatarajiwa kutoka nchi za ulaya mashariki.

  Zaidi ya watu 450,000 toka nchi mbali mbali duniani wanatarajiwa kuingia nchini Afrika Kusini kwaajili ya kombe la dunia.

  Akiongea katika kikao na umoja wa mataifa kuhusiana na vita dhidi ya madawa ya kulevya na uhalifu nchini humo, David Bayever, ambaye ni makamu mwenyekiti wa mamlaka ya kupambana na madawa ya kulevya nchini Afrika Kusini alisema kuwa maafisa wa Afrika Kusini wanahofia wimbi kubwa la wanawake wanaotarajiwa kuingia nchini humo kwaajili ya biashara ya ukahaba.

  "Tumepewa taarifa na waandaaji wa kombe la dunia kuwa wamepata taarifa kuwa wanawake 40,000 wameajiriwa kuja kufanya ukahaba wakati wa kombe la dunia", alisema.

  "Hali inatisha sana kutokana na kwamba asilimia 16 ya idadi ya watu wana maambukizi ya virusi vya ukimwi", alisema.

  Bayever alisema kuwa wamehakikishiwa na idara ya uhamiaji kuwa ulinzi utaongezwa kwenye mipaka na ukaguzi wa pasport utaimarishwa.
   
 2. T

  Tall JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Du, hiyo kazi kweli kweli.
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  Mar 8, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Siyo hivyo tu... tahadhari imetolewa kwa watoto wakike wawe extra careful kipindi hiki maana kuna kutekwa nyara na kuingizwa kwenye utumwa wa ngono..kisa world cup!
   
 4. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #4
  Mar 8, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Watawadhibiti vipi endapo watakuwa na passport, na obvious watakuwa nazo kwa kuzingatia kwamba wanatoka ulaya mashariki ambako ni mbali kutoka SA ni lazima watafuata sheria zote za uhamiaji lakini ndio wakisha tia timu kazi moja!!
   
Loading...