• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Makadirio ya uchumi wa dunia 2020 kuwa madogo huku uchumi wa China ukitarajiwa kuporomoka

miss zomboko

miss zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Messages
2,606
Points
2,000
miss zomboko

miss zomboko

JF-Expert Member
Joined May 18, 2014
2,606 2,000
Benki ya Dunia imesema ukuaji wa uchumi wa dunia kwa mwaka huu unakadiriwa kufikia asilimia 2.5, ikilinganishwa na asilimia 2.4 ya mwaka jana, licha ya kuendelea kuwepo kwa hatari ya kushuka.

Ripoti mpya kuhusu mustakbali wa uchumi wa dunia inayotolewa kila baada ya nusu mwaka na Benki ya Dunia, inasema ongezeko hilo linaweza kuwa kubwa zaidi kama hatua za kisera zinazochukuliwa hivi karibuni, haswa zile ambazo zimepunguza mvutano wa kibiashara, zitaendelea kupunguza sintofahamu ya sera.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, ukuaji katika masoko yanayoibuka na nchi zinazoendelea unatarajiwa kufikia asilimia 4.1 mwaka 2020 kutoka asilimia 3.5 ya mwaka 2019, huku ukuaji katika nchi zilizoendelea ukikadiriwa kushuka hadi kufikia asilimia 1.4 kwa mwaka huu ikilinganishwa na asilimia 1.6 ya mwaka jana.

Uchumi wa China unakadiriwa kukua kwa asilimia 5.9 mwaka huu, ukipungua kutoka asilimia 6.1 ya mwaka 2019.
 
Mgumu04

Mgumu04

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2011
Messages
1,689
Points
2,000
Mgumu04

Mgumu04

JF-Expert Member
Joined Jul 15, 2011
1,689 2,000
Hii ripoti imekaa kibeberu sana mbona hawajasema kuhusu kukua kwa kasi uchumi wetu?

Sent from my TECNO WX3 using Tapatalk
 

Forum statistics

Threads 1,406,209
Members 532,237
Posts 34,508,800
Top