Makada wa CCM waliozomewa mpaka hivi sasa

ebaeban

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
2,205
2,689
Wafuatao ni makada wa CCM ambao wameonja joto ya jiwe ya kuzomewa na wanainchi katika mikutano ya hadhara wanayoiitisha kufikia leo saa nane mchana ni hawa hapa


  1. Mh. Chacha Maliam Nyang`wine - Mbunge wa Tarime alizomewa akatupiwa na masale ya CCM na gari likapigwa wakavunja vioo akakimbia mkutano
  2. Mh. Steven Wassira -Mbunge na waziri alizomewa kwao bunda mkutano ukaisha akatukana na matusi, aliwatukana wapiga kura wake.
  3. Mh Ole Medeye mbunge na waziri alizomewa kata ya daraja mbili hadi lengo aliloendea pale yaani kumfanyia kampeni diwani wa CCM halikutimia.
  4. Mh Hawa GHASIA -Mbunge na waziri alizomewa kwao mtwara kwenye uwanja wa sokoni pale anapouzia kahawa Hassani akachanganyikiwa hadi akasema wapiga kura wangu wa Mtwara vivjijini wananielewa
  5. Mh. Aggrey Mwanri naye hivyo hivyo
  6. Mh. Abraham Kinana naye hivyo hivyo hadi haamini macho yake
  7. Mh. Nape Nnawiye huyu ndio aliyezomewa mala nyingi kuliko wote anahamaki mpaka anatukana matusi
  8. Mh Jakaya Kikwete Chunya msafara wake ulitupiwa mawe
  9. Mh. Mama Salima kikwete -first lady huko mbeya alizomewa na ARUSHA wakati anamfanyia kampeni Batrida Buriani alizomewa akabidi afanye mikutano ya ndani
My take kwanini watu wanawazomea viongozi wetu? Mbona wakina Wilbrod Slaa. Mnyika, Mdee hawazomewi?
 
The answer is simple,tumewachoka!Am sure 2015 kuna baadhi ya mikoa magamba hawata amini
Kama MARA,ARUSHA,MWANZA,MBEYA,KILIMANJARO,DSM,IRINGA,SHY!!
 
Waendelee kuzomewa mpaka kwenye masanduku ya kura! Hawatufai! Ni wasaliti wa uzalendo!! Puuuuuuu ccm!
 
Makada wa CCM hawazomewi na watu wastaarabu baliwatu walioandaliwa kwa kumezeshwa viroba (Pombe kali), ili wapoteze viwango vyautu na utashi wao, hali inayowawezesha kuvamia vikao vya CCM na kupiga mayowekunakopunguza utulivu na masikilizano. Hapa nchini siku hizi, kumezuka utamaduni mpya wa vijana wadogowaliopotoka kimaadili kuwazomea viongozi ambao kiumri wako sawa na wazaziwao au hata kuwazaidi. Hizo ndizo Siasa za baadhi ya wapinzani ambaohawana hoja mbadala za kuwasilisha mbele ya umma bali kuivuruga CCM, Chama chenye SERAdhahiri na ILANI inayotekelezwa kwa kulenga mahitaji halisi ya umma kupitia Serikaliza Mitaa. Wapinzani hawawezi kuwasilisha mipango yao ya maendeleo bali lao ni kutoaporojo za kukichonganisha CCM na Umma. Hawana jipya. Generali Ulimwengu kama Mtanzania mzalendo, alikuwana nia njema katika kuasisi mitandao ya kijamii. Kwa uzalendo wake aliamuakuweka mfumo wa kimawasiliano ili WaTanzania wenzake wapate fursa yakubadilishana mawazo ili kuboreshana kifikra. Mchango wake sasa umewamiwa nawatu ambao wanachukulia ubunifu huo kama fursa ya kutukanana na kukashifiana nakupotosha kila jambo kama kwamba wanapo pengine pa kuhamia wakipachafua palipopao. Watumiaji wengine wa mitandao ya kijamii hawajitofautishi na bomba ambalokwa asili yake halichagui kati ya kupitisha maji-taka au maji safi! Hawachujihabari na ikiwa wamebahatika kuzifahamu chembechembe za ukweli wanakosauungwana wa kuisawazisha habari ili kuiweka katika mwanga bora ili watu waijuekweli iliyo kweli. Kumbukeni kwamba watoto wa Tanzania wanasoma hayomnayoyaandika na hivyo mnawapa uridhi mchafu nao hubaki kwenye giza tatanishi wakidhanikwamba hayo yasemwayo ni kweli na hivyo kubakia katika wingu la dhana potofu!! Siouungwana mtu kushupalia jambo asilolijua kwa ushabiki tu na kwa kuwa kalionakwenye mtandao na kujiweka katika nafasi kama kwamba analifahamu lisemwalo!Wapo watu wanajiofanya wanajua wasichokijua kumbe hawajui wajuacho! Ikumbukwe kwamba Waziri Professor Maghembe alikuwana ziara maalum ya kitaifa kuzindua Miradi ya ya maji katika Vijiji 10 kwenyekila Halmashauri nchini. Uzinduzi huu ulifanyikia KITAIFA katika kijiji cha Endagilleambapo maji yatatosheleza kwa 246%. Hili lilikuwa tukio la shukrani kwa Mungukwa ufanisi huo wa kupatikana kwa maji yatakayotumika kwa binadamu na mifugoyao. Maji hayo yataboresha kipato katika ngazi ya kaya, kwa watu kuanzishabustani na hivyo kuuza mazao yao. Kwa mantiki hiyo, mzunguko wa fedha kijijiniutaboreka. Sasa, katika mazingira hayo, ni binadamu gani mtimilifuambaye anaweza kukosa moyo wa shukrani kwa Mungu hadi kumzomea Kiongozialiyekuja kuwaondolea adha ya muda mrefu ya ukosefu wa maji? Kazi ya kipaumbele(aliyoijia) Professor kaifanya kwenye kata ya jirani (Mamire) na baada ya hapo akaombwakufika kwenye Kata ya Gallapo, ambayo, wala haikuwa kwenye ratiba ya shughulizake za siku! Kutokana na tabia yake ya upendo, upole, utu na uungwana, alikubaliombi la viongozi na kuchepusha ratiba na muda wake ili apate fursa ya kuwaonawana Gallapo wanaokabiliwa na adha ya upungufu wa maji kwa muda mrefu. Alikubali! Kwa watu wanaomjua Mungu, wananchi haowalipata "Bahati ya Mtende" Waziri Maghembe hakuzomewa na wananchi wa Gallapo.Waziri huyo alitoa maelekezo ya njia za utatuzi wa kero ya upungufu wa maji-akiwaWaziri mwenye dhamana. Aliahidi KISIMA kipya cha MAJI ambacho kitakamilika kablaya mwisho wa Mwaka wa Fedha, mradi wa maji uliopo uboreshwe na masualayanayolalamikiwa na wananchi ambayo Mkuu wa Mkoa aliyatolea maagizo namaelekezo yatekelezwe haraka sana. Je, huyo ndiye kiongozi wa kuzomewa? Ukweli wa hali halisi ni kwamba Vijana waliandaliwakufanya vurugu kwa kuwa Zito Kabwe amepanga kufanya ziara yake Gallapo. Walichobainini kwamba hawatakuwa na hoja yenye mashiko kwa kuwa Serikali imeshapataufumbuzi wa tatizo lililokuwa likiwakabili wanaGallapo. Sasa, hoja na agendainayosikilizika kwa wananchi wangeipata wapi kwa ufanisi huo wa kudumu waSerikali ya CCM? Akina mama wa Gallapo pamoja na wananchi wenyemapenzi mema wanaishukuru Serikali kwa utekelezaji wake mahiri. Madhaifu yakiutekelezaji yatashughulikiwa na Mkuu wa Mkoa kwa hatua za ufuatiliaji. Wakati huo, muda ulikuwa Saa 10 jioni, alimbidi MheshimiwaMaghembe kwa heshima aombe ruhusa ya kuondoka mkutanoni kwenda Arusha nahatimaye KIA ambako atapanda ndege kwenda Dar-es-salaam na ndiyo sababu yakuomba asiulizwe maswali kwa mambo muhimu yafuatayo;1. Mudaulikwisha na hivyo asingeweza kuyajibu maswali ya wananchi kikamilifu na kwaufanisi. Hakutaka kulipua,2. Aliwapawataalamu maelekezo ya mambo ya kufanya kwa kuwa watu wanahitaji huduma ya majina wala sio maneno matupu,3. Taarifaya mgogoro wa maji Gallapo ilikwisha-kuwasilishwa kwake kwa maandishi,4. Maelekezoya Mkuu wa Mkoa yatatekelezwa mara arudipo kutoka msibani,5. Alitakiwakwenda Arusha na hatimaye KIA atakaporuka kwenda Dar. Ndege haisubiri pindimuda unapowadia,6. AliwaagizaWataalamu aliofuatana nao warudi kufanya uchunguzi wa tatizo la maji Gallapo kuanziasiku ya tatu na taarifa iwasilishwe kwake kabla ya ziara yake ya Gallapo,7. AlitoaAhadi ya kurudi tena Gallapo ndani ya Mwezi Desemba ili ashiriki katika uchambuziwa tatizo hadi ufumbuzi wa kudumu uapatikane huku tukiendea kipindi chautekelezaji wa mradi. Hakuna jambo la kuzomea hapa ila tu athari yamaandalizi ya vijana kwa ajili ya ziara ya Zitto Kabwe anayezuru Gallapo. Kwa mantikihii, hata wewe mwenyewe utajua kwamba tatizo hilo la maji ndiyo uhai na kiinicha ziara ya wapinzani Gallapo. Mtu kama Kabwe akiyajua haya, bila shakaatapuuza ziara hiyo na kwenda kwingineko! Mungu anatuelekeza kuijua kweliitakayotuweka huru na tukiitumia kweli tutakuwa huru kweli kweli.
 
Lucas usiogope nginja nginja dhidi ya chama cha majoka kwani ninyi ni wenye ndimi mbili.Enyi kizazi cha nyoa, wana wa majoka,mtaifilisi nchi yetu hadi lini?Tukimaliza zomea zomea na nginja nginja itafuata gwila gwila.
 
Na mimi nachukua fursa ya kuwazomea CCM wote watakaosoma ujumbe huu. Haooooooooooooooooooooooooooooo wezi Haoooooooooooooooooooo, wauaji Haooooooooooooooooooooooooooooooo, mafisadi haoooooooooooooooooooooooooo, Waongo Haooooooooooooooooooo.
 
Simiyu hakuna wanywa viroba kama wa huko mtwara huku simiyu hata hao cdm hajawahi kufanya mkutano wao wa m4c hata mmoja leo useme ccm itazomewa huku acha uongo wako
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom