MAGALEMWA
JF-Expert Member
- Jul 8, 2015
- 6,413
- 4,882
Kwa ambao umri wao hawakuona utawala wa Awamu ya Kwanza ya Mwalimu Nyerere mjue kwamba kulikuwa na mstari mwekundu kati ya serikali na chama tawala.
1. Serikali iliendeshwa kwa sheria kanuni na taratibu zake na "wataalamu" kwenye fani zao. Makatibu Wakuu walikuwa wamebobea kwenye fani ya utawala. Walifanya hivyo na wakaheshimiwa na wataalamu waliokuwa chini yao na vivyo hivyo wataalamu waliwaheshimu watawala (Makatibu Wakuu).
Kwa mfano Katibu Mkuu ni mtawala kwa fani na utendaji wizara ya afya, wakurugenzi kwenye wizara hiyo walikuwa watu waliobobea kwenye fani na taaluma ya afya. Hata ingekuwa msimamizi wa mafunzo kwenye wizara ya afya alikuwa na vimelea vya elimu ya afya ya kutosha.
2. Wansiasa waliochaguliwa hawakuwa watawala bali viongozi. Walisimamia yale waliyokuwa wamenadi kama vipaumbele vinavyohitajika na wapiga kura. Jikite tofauti iliyokuwepo WATAWALA HAWAKUWA VIONGOZI WA KISIASA. NA VIONGOZI WAKISIASA WALIHESHIMU SANA WATAWALA (SERIKALI) KWA TAALUMA ZAO.
Niseme hiyo ilikuwa kati ya misingi ya uadilifu iliyokuwa imesimikwa na Azimio la Arusha ambalo lilitambua serikali inatakiwa ifanye vipi kazi na wanasiasa wafanyeje kazi vipi. Kiurahisi kulikuwa na "CHECKS AND BALANCES' Na nguvu ya wanasiasa ilikuwa ni kama jicho linalofuatilia utendaji wa serikali.
3. Kukaja Azimio la Zanzibar utawala wa Awamu ya Pili. Hapo tulishuhudia uteuzi wa Makatibu wakuu nje ya taaluma ya Utawala wala fani ya sekta. Mengine hayafai kusema maana yalienda mbali kujaribu kufanya upendeleo kwa misingi isiyo ya kitaalamu wala uadilifu. Awamu hii hasa iliishia kwenye uteuzi wa makatibu wakuu katika utendaji wa serikali.
4. Awamu iliyofuata ikichagizwa na kuanza vyama vingi ilifikia uteuzi wa kisiasa (usiojali taaluma) kushuka kwenye ngazi ya Wakurugenzi.
5 Awamu ya nne tumeshuhudia uteuzi wa kisiasa (usiojali taaluma) ukitamalaki hadi kwa maRC na maDC
6. Awamu hii kila mtu anashuhudia jinsi ambavyo makada wa CCM wanavyoteuliwa kushika nyadhifa za kiserikali (usiojali taaluma) kuendeleza kukamata serikali kuwa kaidara ka chama
Kuna kujikanganya kwa kufanya hivyo. Ni rahisi kuona jinsi utaalamu utakavyoburuzwa kiutendaji na matakwa ya kisiasa. Tumeshuhudia jinsi wateule wanavyoingia jikoni kupika (kutenda kazi za serikali). Mambo yakienda ndivyo sivyo kisiasa watasema ni utendaji mbovu wa serikali. Kiserikali kama watumishi waaminifu watanyamaza kutetea nafasi zao. Sisi wananchi na ujinga na ushabiki wetu wa kivyama ni kulalamika siku zinaenda.
Nahitimisha tu kuonyesha jinsi ambavyo tumechanganya mno shughuli za kiserkali na kisiasa kiasi ambacho suala la uwajibikaji linakosa mwelekeo.
Pia cham kinachofanya ni kwa imani kuwa inataka kuhakikisha utendaji wa serikali, lakini utendaji wa kuifunga serikali mikono na miguu ni uuaji wa taaluma ambao hautaonekana hadharani lakini tutachekana mbele ya safari tutakapogundua tulikosea na ni too late kurekebisha.
Hoja hapa ni kuwa na serikali imara haitokani na siasa kuingilia utendaji wa serikali bali kuwa jicho la kuhakikisha utendaji adilifu wa serikali. Tutafukuzana sawa lakini matatizo ya msingi yatabaki bila kutatuliwa kwa mwendo huu