Elections 2010 Makada wa CCM kusini sasa ni vurugu ya migongano ya kisera: Komba vs. Abdul Aziz

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Leo kwenye Channel Ten jioni, Mheshimiwa Komba aahidi wanajimbo lake kuwa serikali ya CCM itajenga bandari kubwa na yenye heshima kuliko ile ya Malawi wakati ambapo chini ya wiki moja Mheshimiwa Abdul Aziz ambaye ni Mbunge aliyemaliza muda wake Lindi Mjini aliwakatisha tamaa wanajimbo hilo pale aliposema hawahitaji kujengewa bandari kubwa kwa sababu hakuna mizigo wala watu wa kusafirishwa.

Swali hapa ni je kama Lindi hawana mahitaji ya bandari mpya ambako bahari ya Hindi ipo itakuwaje Ruvuma wawe na mahitaji ya bandari kubwa hapo Mbaba-Bay kushindana na ile ya Khata kule Malawi?


Swali la muhimu zaidi ni hivi Mheshimiwa Mohamed Abdul Aziz haoni moja ya sababu za bandari ya Lindi kuwa haina bidhaa za kutosha ni kutokana na meli kubwa kushindwa kutia nanga hapo kutokana na ufinyu wa miundo mbinu hapo na kama bandari hiyo ikipanuliwa basi hata Malawi na sehemu za karibu za Msumbiji wataanza kuitumia kusafirishia mizigo yao?

Hata sisi, bara hususani wakaazi wa kusini tutapunguza kuitegemea bandari ya Dar-Es-Salaam na hivyo kupunguza msongamano wa bidhaa hapo?

 
Mpaka sasa huwa sielewi Majid na wenzake wanaona nini ccm ambacho hakionekani kwa macho ya kawaidia. Jamaa wengi walioko ccm ni vilaza wa kupindukia.
 
Back
Top Bottom