Makaburu waliua, waliwakamata na kuwafunga wapigania uhuru lakini mwisho wa yote uhuru ulipatikana

Mghaka

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
320
126
Shoruba, mateso na manyanyaso wanayopata makamanda na wapenzi wa CDM walioko mstari wa mbele yote hayo ndiyo gharama ya kutafuta haki na uhuru wa kweli. Na bado CCM na Serikali yake watafanya mengi mabaya dhidi ya CDM na tunachoshuhudia leo ni trailor tu. Lakini tunaelewa hayo ni mateke ya ng'ombe anayechinjwa yanaumiza lakini hayaogofyi wachinjaji. Mwisho wa yote ng'ombe huyu atakubali yaishe ili tule nyama ya kweli katika usawa halisi na kwa manufaa ya watanzania wote. Wasome historia mkondo wa mabadiliko hauwezi kuzuiliwa na bundiki au risasi, polisi au jeshi.

Zao ni aibu zitawapata tu watakaposhuhudia kimbunga kikali cha mabadiliko. CCM tafadhali tengenezi mazingira mazuri ili mabadiliko hayo yasiwe ya umwagaji damu kwani mtasutwa milele. Historia inawapendelea CHADEMA na si CCM kwa sababu katika kila mjadala mnayokazi ya kueleza kwa nini si hivyo? Mkae mkijua kuwa hao watu mnao wahesabu kama waovu kwetu sisi ni mashujaa. Wakina Mandela, Steve Biko, Sisulu na wengine walionekana wahalifu mbele ya makaburu na serikali yao lakini walikuwa mashujaa mbele ya umma wa watu weusi na wapenda haki duniani.

Vivyo vivyo kwa makamanda wa CDM ni waovu kwa CCM na serikali yake lakini kwetu sisi they are our heroes and they will remain so until total freedom is achieved. Fredom that protects our rights and natural resources and creates equal opportunity for our development. Ukaburu wa ccm na serikali yake unapaza na kukuza umaarufu wa CHADEMA aksanteni endeleeni. Mlifanya hivyo bungeni mkatuzawadia umaarufu mtafanya hivyo nje ya bunge mtatuzawadia uhuru wa kweli, na kwa kila tendo lenu sisi tutakinga mikono kupokea zawadi zenu, tutatega migongo mtukalie tupate uhuru wetu, tutawapa maisha yetu ili damu yetu itakase nchi hii. We are very much focused, we know what we want to achieve, so act and behave in any manner we are there to resist and responsibly counteract your awarkward actions and thoughts.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom