Makaburu Wa Illovo Kilombero wamemuweka DC Mfukoni!

KING COBRA

JF-Expert Member
Nov 10, 2011
2,782
864
MAKABURU WA ILLOVO WA MUWEKA DC ELIAS TARIMO MFUKONI.
Imebainika kuwa Makaburu wa kampuni ya sukari Illuv iliyopo Kilombero wamemhonga Mkuu wa Wilaya Elias Tarimo kwa malengo ya kuandaa mazingira ya kuwalubuni wakulima ili wasikubali kushuka kwa bei ya sukali.
Makaburu wameshusha bei ya sukari kutoka Shs 65,340 kwa tani hadi Shs 58,716 kwa tani na mabadiliko haya yanafanya wakulima kuibiwa Zaidi ya Shs3,616,704,000.

Wanaotajwa kuhusika na mpango huu ni wafuatao:
1.DC Elias Tarimo ( 0787 976111)
2.Msabaha Rashid Nyembe(0715 110611/0787)
3.John Guninita
4.Hakimu Futa Kamba (Mkoa Moro)
5.Makaburu wa Illovo.


Ndugu Msabaha Rashidi Nyembe ni mwenyekiti wa Chama cha wakulima wa Miwa RCGA na baada ya kuhusika na wizi huu wanachama hawana Imani naye tena na kwa bahati nzuri Katiba ya chama hicho hairuhusu kiongozi kuongoza Zaidi ya miaka 6.
Ndugu Msabaha Rashidi Nyembe alianza kutawala tangia mwaka 2007 na sasa amemaliza mda wa kukaa madarakani.
NJAMA ZA KUBADILI KATIKA .
Mkuu wa Wilaya ameshirikiana na Makaburu kuhakikisha kwamba Ngd Msabaha Nyembe anagombea tena nafasi hiyo ili andelee Kuwabeba Makabauru.
Tarehe 29/3/2014 Mkuu wa Mkoa Joel Bendera alizuia kikao cha kubadili katiba na kuamuru kamati ya ulinzi na usalama kusmamia lakini DC Eliasi Tarimo aliruhusu kikao hicho kifanyike na kusema kwamba Ndg Msabaha ana rusiwa kugombea tena.
Tarehe 6/4/2014 DC Elias Tarimo aliruhu mkutano huo kwa yeye kufika kama mgeni rasimi akiwa na OCD Magessa ambaye aliwakamata wakulima wote waliokuwa wanahoji uhalali wa kubadili katiba.

Kufuatia hali hiyo DC ameamuru Uchaguzi ufanyike haraka Tarehe 25/5/2014 siku ya Jumapili na viongozi wote wa zamani wanagombea huku katiba yao ikipiga marufuku.

Hali ya wakulima Kilombero ni mbaya na mgogoro huo unaweza kuleta machafuko makubwa nap engine mauaji

Pia mgongano kati ya DC Tarimo na RC Joel Bendera unaonyesha kuwa Serikali ya JK ipo Ukingoni.

JOHN GUNINITA ni mwanasiasa lakini juzi ameonekana Dodoma akifanya lobbing kwa waziri wa mambo ya ndani huku akiambatana na Mtandao wa Msabaha Nyembe ambaye alikuwa na watu 15 waliosafiri kwa gari T862 APQ na kulala ROBERTHOTEL iliyopo Kizota DODOMA.

Habari kamili:
MGOGORO MKUBWA UMOJA WA WAKULIMA WA MIWA,VIGOGO NDANI YA SERIKALI WASHINDWA KUTATUA
MGOGORO Mkubwa umekikumba chama cha wakulima wadogo wa miwa cha Ruembe Cane Growers Association(RCGA) kilichopo wilaya ya Kilosa Mkoa wa Morogoro kutokana na Mwenyekiti wa chama hicho Msabaha Rashid Nyembe kutuhumiwa na wanachama kuwa ananga’ang’ania madaraka kwa kusaidiwa na baadhi ya vigogo ndani ya serikali.

Kwa mjibu wa maelezo ya wanachama wa chama hicho waliozungumza na gazeti hili jana kwa nyakati tofauti,walisema kuwa mgogoro huo ulianza kujitokeza mwezi februari mwaka huu baada ya mwenyekiti huyo kutangaza kuwania nafasi hiyo kwa mara ya tatu nje ya utaratibu wa katiba hiyo ambayo inamwezesha mwenyekiti kugombea muda wa vipindi viwili tu.

Walisema kuwa kutokana na hatua hiyo,kumekuwepo na msuguano mkali unaohusisha wanachama wa chama hicho na mwenyekiti huyo ambaye anadaiwa kusaidiwa na baadhi ya vigogo ndani ya serikali na mmoja wa wanachama maarufu wa CCM wilaya ya Kilombero ambaye anakusudia kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo la Kilombero kwa kipindi kijacho na ambaye ni mkulima wa miwa wa wanachama wa chama cha Harambee Cane Growers Association.

Walisema kuwa kigogo huyo mwenye makao yake jijini Dar es salaam anadaiwa akitumia umarufu wake ndani ya chama cha CCM kwa kushirikiana na mwenyekiti huyo kuhujumu jitihada ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na wakulima katika ngazi mbalimbali za serikali,kuanzia katika ofisi ya Mtendaji wa Tarafa ya mikumi,ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Kilosa na Mahakama ya Mkoa wa Morogoro.

Mmoja wa wanachama wa chama hicho cha RCGA, Alex Gwila kutoka kikundi cha wakulima wa miwa cha Indete alisema kuwa hali ya chama hicho kwa sasa ipo shakani kutokana na mgawanyiko mkubwa uliopo kati ya mwenyekiti huyo na wanachama wa chama hicho ambao wamekuwa wakiuza miwa katika kiwanda cha Sukari cha Kilombero ambapo kipo chini ya Kampuni ya Sukari ya Illovo inayomilikiwa na makaburi kutoka Afrika kusini.

Alisema kuwa Mwenyekiti huyo amekuwa akifanya hujuma za kutovuna miwa ya baadhi ya wakulima ambao wamekuwa wakihoji uharali wake wa kuendelea kubaki madarakani na kuwasababishia harasa kubwa na ameweza kusababisha makundi miongoni mwa wanachama na kuwa kuna baadhi ya wanachama wametishiwa kufukuzwa uanachama kutokana na kufuatia utendaji wake.

Kwa mjibu wa taarifa kutoka kwa wanachama hao,ni kuwa chama hicho kina wanachama zaidi ya 800 ambao ni hai na ambao wamekuwa wakiuza miwa yao katika kiwanda cha Sukari cha Illovo,ambapo mpaka sasa mwenyekiti huyo anadaiwa kuingiza wanachama mamruki kwa kuwapa vibari ambao wanaofikia zaidi ya 2000 kwa lengo la kuharalisha kuendelea kuwepo madarakani katika uchaguzi unaokusudiwa kufanyika Mei,25 mwaka huu.

Hata hivyo mpaka sasa baadhi ya wanachama wa chama hicho wanadaiwa kuandika barua ya pingamizi ya kususia uchaguzi huo kwa madai ya kutoridhishwa na utaratibu unaotumika na kuwa wanamuomba Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete kuingilia kati mgogoro huo ambao mpaka sasa unadaiwa kushindwa kutekelezwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Mathias Chikawe licha ya kupekelewa malalamiko hayo.

Pia wanachama hao walisema kuwa mwenyekiti huyo ameshapanga safu ya watu watakaosimamia uchaguzi huo,ambapo mmoja wa watu watakao simamia uchaguzi huo ni mwenyekiti wa uchaguzi Ben Makundi ambaye ni mmoja wa wadhanini wa chama cha RCGA ambaye anatajwa kuwa ni rafiki mkubwa wa mwenyekiti wa chama hicho.

Akizungumza kwa njia ya Simu na Gazeti hili,Mwenyekiti huyo Msabaha Rashid Nyembe alisema kuwa wanaolalamikia kutokana na hatua ya yeye kugombea nafasi ya uenyekiti kwa awamu ya tatu ni wahuni na kuwa kwa sasa kinachosubiriwa ni uchaguzi tu,ambapo amewatuhumu baadhi ya wanachama hao kupita katika ngazi mbalimbali za serikali bila ya mafanikio.

‘’Ndugu mwandishi tunachosubiri kwa sasa ni uchaguzi tu ambao utafanyika mei,25 mwaka huu,wanaolalamikia kuwa sifuati katiba ya chama ni wahuni wachache wasio na nia njema ’’alisema Nyembe kwa ujasili.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera baada ya kuzungumza na gazeti hili kwa njia ya simu alikiri kuufahamu mgogoro huo, na kuwa Mkuu wa wilaya ya Kilosa Elias Tarimo amekuwa akiushughulikia kwa mara kadhaa.

Aidha Bendera alisema kuwa kutokana na ukubwa wa mgogoro huo mwenye kuamua ni Waziri wa Mambo ya Ndani Mathias Chikawe kwa kuwa ndani ya Ofisi yake kuna watalaamu waliobobea katika mambo ya kisheria.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema tatizo kubwa linalowasumbua wakulima wadogo wa miwa wa umoja wa wakulima wa RCGA ni suala la muda wa uongozi wa vipindi viwili au vitatu,kwa hiyo ni suala la uamuzi tu wa kisheria ambalo lipo ndani ya uwezo wa Waziri wa mambo ya Ndani Mathias Chikawe.

Taarifa za uchunguzi za Gazeti hili ni kuwa kumekuwepo na msuguano mkali kati ya Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera ambaye anadaiwa kuwasaidia wakulima hao na Mkuu wa wilaya ya Kilosa Elias Tarimo ambaye anadaiwa kumezwa na genge la Mwenyekiti wa Umoja wa wakulima hao wa RCGA na kigogo wa maarufu wa CCM aliyopo katika mtandao ndani ya chama hicho cha ccm katika nafasi ya Ugombea urais.

Mpaka sasa taarifa kutoka ndani ya kampuni ya sukari ya Illovo zinaonyesha kuwa imeshusha bei ya sukari kutoka sh 65,340 kwa tani hadi sh 58,716 na kusababisha wakulima wengi kushindwa kujiendesha,ambapo hujuma hizo zinadaiwa kufanywa Mwenyekiti huyo ambaye pia ni mwenyekiti wa umoja wa wakulima wa Miwa Tanzania(TASGA).

Na hadi kufikia jana baadhi ya makundi ya watu wanaodaiwa kuwa mamruki walikuwa wamewasili wilayani kilosa kutoka wilaya ya Kilombero kwajili ya kampeni na kufikia katika hotel maarufu ambayo jina limehifadhiwa,na pia hadi kufikia jana Mwenyekiti huyo wa RCGA alikuwa mjini Dodoma kwa lengo la kuonana na mmoja wa vigogo wa serikali kwajili ya hatima ya katiba hiyo,hata hivyo jitihada za kumpata mkuu wa wilaya hiyo ya Kilosa Elias Tarimo hazikuweza kufanikiwa kutokana na simu yake kushindwa kupatikana.

Katika katiba ya awali ilikuwa ikimruhusu mgombea wa nafasi ya Uenyekiti kugombea kwa vipindi vitatu mfululizo hadi mwaka 2006 na baada ya hapo,katiba hiyo ilibatilishwa ambapo mwenyekiti anaruhusiwa kuwepo madarakani kwa muda wa miaka 6 tu.
 
Wasubiri waje kupigwa makofi kama yule mchina alompiga sijui nani kortini
 
Na hadi waziri wa mambo ya ndani karuhusu abadili katiba awe wa maisha na Rais Anajua.Hongera CCM Kwa Rushwa na wizi
 
Back
Top Bottom