Makaburi yamewabeba watu muhimu sana ambao ulimwengu ulikua bado unayahitaji mawazo yao

justin mwanshinga

Senior Member
May 22, 2014
179
619
Siri ya Makaburi.

Bwana Gerald Magooge Reuben, katika kitabu chake cha ""Makaburi Yameelemewa Utajiri"" anafafanua kuwa watu wengi wanakufa na vipaji au tunu walizozaliwa nazo kwa kushindwa kuzifanyia kazi, hatimaye utajiri wa tunu hizo unaenda kujilimbikiza makaburini. Wengine hawajafa katika mpango wa kimungu bali ni kutokana na ukatili wa watu wabaya .

Ukiishi maisha halisi, unatumia nguvu na rasilimali za kawaida kufikia malengo yako. Yapo maswali ya msingi ya kujiuliza ili kujua je, unaishi maisha yako halisi katika kazi, ndoa, fani , biashara n.k au umeshikwa na mtego wa kuishi maisha ya mtu mwingine ??

Pamoja na hayo hali mbaya ya kiuchumi isikufanye ukaishi maisha ya kujidhalilisha kwa kufanya mwili wako kuwa pagala au akili yako kuonekana inawaza upumbavu zaidi kuliko mambo ya maana. Ni katika hilo inatupasa kuyaishi maisha yenye kufuata misingi ya haki ili kuepuka laana n.k.

Makaburi yamewabeba watu wa muhimu sana kama Martin Luther Jr, Alphonce Mawazo na Wengine weengi ambao ulimwengu huu ulikua bado unayahitaji mawazo yao na misimamo yao.


Mwanshinga Jr
 
Ungesema siri za marehemu,,, sasa lile shimo linabeba siri gani wakati kinachoingia mule ni marehemu haongei, hatendi n.k
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom