Makaburi ndani ya CCM: Mnakumbuka vijisenti vya Chenge? Mahakama ya mafisadu ni ya kina nani Tanzania?

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
MKIWEZA, FUKUENI NA MAKABURI HAYA;

...Mwaka 2008, aliyekuwa waziri wa miundombinu, Andrew Chenge, ambaye alikuwa mwanasheria mkuu wa Tanzania wakati wa sakata la manunuzi ya rada, alijiuzulu kufuatia tuhuma za kumiliki pauni 500,000, katika akaunti ya benki huko Jersey, Uingereza. Chenge hakukataa kumiliki fedha hizo lakini alikataa kuwa alilipwa na BAE system.

Akitumia nafasi yake ya mwanasheria mkuu wa serikali alishauri baraza la mawaziri la Tanzania kukubaliana na mradi wa manunuzi ya Rada. Zaidi alitamka kwamba mkopo wa kibiashara ambao ulipangwa kutolewa na benki ya Barclays, haukuwa kinyume na masharti ya kufutiwa deni la Taifa. Inasemwa kwamba, Sailesh Vithlani alituma kwenda Barclays nakala ya maoni ya Andrew Chenge aliyowasilisha katika baraza la mawaziri. Mara tu baada ya Vithlani kutuma nakala hiyo, yakafuata malipo ya fedha katika akaunti ya Chenge iliyopo huko Jersey.

Kwa mujibu wa taarifa za SFO (Serious fraud office) Andrew Chenge alipokea malipo ya fedha kwa awamu sita kutoka june 1997 hadi Aprili 1998, jumla ya fedha hizo zikiwa dola 1.5 milioni. Fedha hizo zilitoka ujerumani katika Benki ya Barclays, tawi la Franfurt na kuingizwa katika benki ya Barclays tawi la Jersey. Jina la akaunti ya Jersey lilikuwa Franton Investiment Limited, kampuni inayomilikiwa na Andrew Chenge kwa dhumuni maalumu la kuingizia fedha.

Mei 1998, Andrew Chenge, akiwa mwanasheria mkuu alihalalisha (Authorized) malipo ya dola 600,000 kwenda kwenye akaunti ya kampuni iliyoitwa Langley Investments Limited, ilioyomilikiwa na aliyekuwa gavana wa benki kuu wa Tanzania, Dr. Idrissa Rashidi. Rashidi ndiye alikuwa na jukumu la kupitisha (Approve)fedha za malipo ya rada, ambayo masharti yake yalikuwa kuifanya hazina za dhahabu zilizopo benki kuu kama dhamana ya mkopo kutoka Barclays.
Rashidi alikubali pia kwamba, ikiwa Tanzania itakiuka masharti ya mkopo huo, basi sheria zitakazotumika katika mgogoro utakaoibuka, ni za Uingereza na sio za Tanzania.

Septemba 20, 1999, Andrew Chenge, yeye mwenyewe alihalalisha kuhamisha fedha kiasi cha dola 1.2 milioni kutoka katika akaunti ya kampuni aliyomiliki ya Franton Investments Limited kwenda kwenye akaunti yake binafsi katika benki iliyoitwa ‘Royal bank of Scotland’ ya hukohuko Jersey, Uskochi. Taarifa hizi zilipovuja, Chenge hakuonesha kuguswa, badala yake aliziita fedha hizo vijisenti.
Wanasheria wa Andrew Chenge kutoka Uingereza na Marekani walikiri kwamba, mteja wao alihusika kutoa ushauri wa kisheria katika mradi wa manunuzi ya rada, lakini walikataa kwamba Chenge alisisitiza manunuzi hayo. Hata hivyo, haifahamiki ni vyanzo gani vya mapato alivyonavyo Andrew Chenge, vilivyomuwezesha yeye kuajiri wanasheria nguli na ghali kutoka Uingereza na Marekani.

Wakati wa majira ya vuli ya mwaka 2006, uchunguzi juu ya uhusika wa Andrew Chenge katika mradi wa rada, ulipamba moto. Norman Lamb alikutana na mawakala wa SFO na Wizara ya Ulinzi, katika jengo la Port Cullis ambamo linahodhi ofisi za baadhi ya wabunge wa Uingereza. Mpelelezi kutoka SFO alipendekeza kwamba mkutano huo ufanyike kwenye chumba tofauti na ofisi ya Lamb, kwa kuhofia kwamba ofisi hiyo inaweza kuwa imewekewa vifaa vya kunasa mawasiliano. Kusikia hivyo, Norman Lamb alighadhibika sana na tangu hapo akawa na hofu.

Tarehe 5 juni 2008, Lamb alimuandikia wakala yule wa SFO, Bw. Carl Brown akimkumbusha kauli yake wakati uchunguzi ukiendelea. Lamb aliandika; ‘Ulisema kuwa wakati uchunguzi ukiendelea, Kampuni ya BAE ilikuwa ikijua kinachoendelea na kwamba walikuwa na taarifa zako na mashahidi uliokuwa ukikutana nawo. Ulionesha kuwa BAE wanaweza kunasa mazungumzo yako ya siri uliyofanya na mashahidi”.
Wakala wa SFO alijibu kuwa, si kweli kwamba alikuwa akifahamu kuwa BAE wananasa mazungumzo yake, isipokuwa alishauri kutotumia ofisi na maeneo rasmi ya mashahidi kwa ajili ya mahojiano, kama angalizo tu katika taratibu za kiuchunguzi, ilikuwa jambo la busara kuchukua tahadhari.
Mbunge Norman Lamb, alijibu kuwa, matumaini yake ni kuwa hakukuwa na vinasa mawasaliano katika ofisi yake. Na kwamba hakuwa akifanya usafi katika ofisi yake kwasababu hakutaka kuoenekana kuwa na hofu ya kuwekewa vinasa mawasiliano.

Hata hivyo baadae taasisi ya SFO,ilidai kuwa, kampuni ya BAE iliajiri majasusi wa kufuatilia uchunguzi ule. Lakin kampuni ya BAE ilikana na kuita tuhuma hizo kuwa ni uzushi.
Inafahamika namna kampuni ya BAE system inavyofuatilia maadui zake, hasa katika biashara za silaha. Na hofu aliyokuwa nayo Norman Lamb inafanana na hofu aliyokuwa nayo Edward Hosea, aliyekuwa mkurugenzi wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) wa Tanzania. Mwaka 2007 Hosea aliwaambia wapelelezi kutoka Marekani kwamba; ‘maisha yangu yapo hatarini na kuongeza kuwa wanasiasa wa Tanzania hawagusiki katika sakata la mradi mchafu wa rada’. Hosea alikata tamaa ya kuwafikisha mahakamani vigogo waliohusika wa mradi wa rada lakini alikuwa na uhakika kwamba, wakuu wa vyombo vya ulinzi nawo walihusika katika kashfa hiyo. Hosea aliongeza kuwa amepokea vitisho kupitia ujumbe wa simu na barua, akitaarifiwa karibu kila siku, kuwa anapambana na watu matajiri na wenye nguvu. Hosea alieleza kuhusu vikao nyeti vya serikali vinavyosheheni ubabe na vitisho; “Unapoingia katika mikutano yao, wanataka ujione kuwa mdogo na wao uwaone kama miungu. Wanataka ufahamu kuwa wao ndio wamekuweka hapo. Usipokubaliana nawo, kuna hatari”.
Hosea alitanabaisha kuwa kama vitisho vitaendela juu yake, atahama nchi. Wakati huo hali ya nchi ya Tanzania ilikuwa tete katika uwanda wa demokrasia na imani ya wananchi kwa serikali yao. Usalama wa Hosea na baadhi ya wanasiasa waliokuwa mbele kutaka wahusika wachukuliwe hatua, ulitegemea zaidi nguvu ya taasisi ya SFO na vyombo vya kisheria vya Uingereza...

#Simulizi_za_wazalendo
 
Hao CCM ni wasanii tuu......

Hata hiyo Mahakama yao ya mafisadi ni ya kisanii tuu.......

Kwa kuwa kama kweli hao CCM wamedhamiria kwa dhati kuiunda mahakama hiyo ya mafisadi, basi hakuna hata kiongozi mmoja wa CCM atakayepona kuburuzwa kwenda kwenye Mahakama hiyo!

Hebu jaribu kuimagine, Ngeleja alikiri kupokea pesa ya rushwa shilingi milioni 40 toka kwa Rugemalira kwa pesa ya Escrow!

Hebu fikiria ni kwanini Rugemalira ndiyo bado yupo ndani zaidi ya mwaka sasa, wakati Ngeleja yupo uraiani akila raha??
 
Yaani siasa za ccm ni za kimalaya malaya
 
Tena katika awamu hii ya mtetezi wa wanyonge alikiri aisee jamaa anaendesha nchi kwa kujuana ngeleja angekuwa mpinzani angekiona cha moto hata nchi angeikimbia ukiwa ccm ukakiri wizi huna mashaka na maisha yako.
 
Jitu liko busy linapambana kudhibiti VYOMBO VINAVYOFICHUA RUSHWA.

Ni visasi, roho mbovu, akili ndogoo, ulimbukeni, ushamba na ukatili ndo vinafanya kazi.

- Tido Muhando yuko mahakamani, CHENGE anapewa MAVYEO tu.

- Polisi wanaambiwa WACHUKUE HELA YA KUBRASH VIATU

- JIWE linaongoza kutoa RUSHWA kuhonga PESA na VYEO kwa watu wakiwemo WABUNGE na MADIWANI.

hata upuuzi wa kupambana na rushwa awamu ya tano ni mtu anaeuamini ni zwazwa kuu
 
Jokate mwenye picha za uchi mitandaoni ,kapigwa mashine na Hashim thabit,Diamond,AY,Jux,Dogo Jbnga eti kazawadiwa ukuu wa wilaya,Yesu tuokoe
 
Akili za panzi hizi kwa hiyo bila kuweka ile list serikali haiwezi kuwashika? Kumbe tunaserikali mfu iliyozidiwa na chadema tuna takukuru wanalipwa pesa ambayo ni kodi ya mtanzania na ndio kazi yao kuchunguza haya mambo
Ndio maana tunataka ile list of shame ya mwembe yanga irudishwe kwenye tovuti ya chadema na ikumbushwe kila mara!
 
Mijitu iko busy kuhangaika kufunga wapinzani huku haya mahujumu uchumi yakilindwa na hapo hapo yanajiita
eti ni mzalendo!!!

Ovyoo!!
 
MKIWEZA, FUKUENI NA MAKABURI HAYA;

...Mwaka 2008, aliyekuwa waziri wa miundombinu, Andrew Chenge, ambaye alikuwa mwanasheria mkuu wa Tanzania wakati wa sakata la manunuzi ya rada, alijiuzulu kufuatia tuhuma za kumiliki pauni 500,000, katika akaunti ya benki huko Jersey, Uingereza. Chenge hakukataa kumiliki fedha hizo lakini alikataa kuwa alilipwa na BAE system.

Akitumia nafasi yake ya mwanasheria mkuu wa serikali alishauri baraza la mawaziri la Tanzania kukubaliana na mradi wa manunuzi ya Rada. Zaidi alitamka kwamba mkopo wa kibiashara ambao ulipangwa kutolewa na benki ya Barclays, haukuwa kinyume na masharti ya kufutiwa deni la Taifa. Inasemwa kwamba, Sailesh Vithlani alituma kwenda Barclays nakala ya maoni ya Andrew Chenge aliyowasilisha katika baraza la mawaziri. Mara tu baada ya Vithlani kutuma nakala hiyo, yakafuata malipo ya fedha katika akaunti ya Chenge iliyopo huko Jersey.

Kwa mujibu wa taarifa za SFO (Serious fraud office) Andrew Chenge alipokea malipo ya fedha kwa awamu sita kutoka june 1997 hadi Aprili 1998, jumla ya fedha hizo zikiwa dola 1.5 milioni. Fedha hizo zilitoka ujerumani katika Benki ya Barclays, tawi la Franfurt na kuingizwa katika benki ya Barclays tawi la Jersey. Jina la akaunti ya Jersey lilikuwa Franton Investiment Limited, kampuni inayomilikiwa na Andrew Chenge kwa dhumuni maalumu la kuingizia fedha.

Mei 1998, Andrew Chenge, akiwa mwanasheria mkuu alihalalisha (Authorized) malipo ya dola 600,000 kwenda kwenye akaunti ya kampuni iliyoitwa Langley Investments Limited, ilioyomilikiwa na aliyekuwa gavana wa benki kuu wa Tanzania, Dr. Idrissa Rashidi. Rashidi ndiye alikuwa na jukumu la kupitisha (Approve)fedha za malipo ya rada, ambayo masharti yake yalikuwa kuifanya hazina za dhahabu zilizopo benki kuu kama dhamana ya mkopo kutoka Barclays.
Rashidi alikubali pia kwamba, ikiwa Tanzania itakiuka masharti ya mkopo huo, basi sheria zitakazotumika katika mgogoro utakaoibuka, ni za Uingereza na sio za Tanzania.

Septemba 20, 1999, Andrew Chenge, yeye mwenyewe alihalalisha kuhamisha fedha kiasi cha dola 1.2 milioni kutoka katika akaunti ya kampuni aliyomiliki ya Franton Investments Limited kwenda kwenye akaunti yake binafsi katika benki iliyoitwa ‘Royal bank of Scotland’ ya hukohuko Jersey, Uskochi. Taarifa hizi zilipovuja, Chenge hakuonesha kuguswa, badala yake aliziita fedha hizo vijisenti.
Wanasheria wa Andrew Chenge kutoka Uingereza na Marekani walikiri kwamba, mteja wao alihusika kutoa ushauri wa kisheria katika mradi wa manunuzi ya rada, lakini walikataa kwamba Chenge alisisitiza manunuzi hayo. Hata hivyo, haifahamiki ni vyanzo gani vya mapato alivyonavyo Andrew Chenge, vilivyomuwezesha yeye kuajiri wanasheria nguli na ghali kutoka Uingereza na Marekani.

Wakati wa majira ya vuli ya mwaka 2006, uchunguzi juu ya uhusika wa Andrew Chenge katika mradi wa rada, ulipamba moto. Norman Lamb alikutana na mawakala wa SFO na Wizara ya Ulinzi, katika jengo la Port Cullis ambamo linahodhi ofisi za baadhi ya wabunge wa Uingereza. Mpelelezi kutoka SFO alipendekeza kwamba mkutano huo ufanyike kwenye chumba tofauti na ofisi ya Lamb, kwa kuhofia kwamba ofisi hiyo inaweza kuwa imewekewa vifaa vya kunasa mawasiliano. Kusikia hivyo, Norman Lamb alighadhibika sana na tangu hapo akawa na hofu.

Tarehe 5 juni 2008, Lamb alimuandikia wakala yule wa SFO, Bw. Carl Brown akimkumbusha kauli yake wakati uchunguzi ukiendelea. Lamb aliandika; ‘Ulisema kuwa wakati uchunguzi ukiendelea, Kampuni ya BAE ilikuwa ikijua kinachoendelea na kwamba walikuwa na taarifa zako na mashahidi uliokuwa ukikutana nawo. Ulionesha kuwa BAE wanaweza kunasa mazungumzo yako ya siri uliyofanya na mashahidi”.
Wakala wa SFO alijibu kuwa, si kweli kwamba alikuwa akifahamu kuwa BAE wananasa mazungumzo yake, isipokuwa alishauri kutotumia ofisi na maeneo rasmi ya mashahidi kwa ajili ya mahojiano, kama angalizo tu katika taratibu za kiuchunguzi, ilikuwa jambo la busara kuchukua tahadhari.
Mbunge Norman Lamb, alijibu kuwa, matumaini yake ni kuwa hakukuwa na vinasa mawasaliano katika ofisi yake. Na kwamba hakuwa akifanya usafi katika ofisi yake kwasababu hakutaka kuoenekana kuwa na hofu ya kuwekewa vinasa mawasiliano.

Hata hivyo baadae taasisi ya SFO,ilidai kuwa, kampuni ya BAE iliajiri majasusi wa kufuatilia uchunguzi ule. Lakin kampuni ya BAE ilikana na kuita tuhuma hizo kuwa ni uzushi.
Inafahamika namna kampuni ya BAE system inavyofuatilia maadui zake, hasa katika biashara za silaha. Na hofu aliyokuwa nayo Norman Lamb inafanana na hofu aliyokuwa nayo Edward Hosea, aliyekuwa mkurugenzi wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) wa Tanzania. Mwaka 2007 Hosea aliwaambia wapelelezi kutoka Marekani kwamba; ‘maisha yangu yapo hatarini na kuongeza kuwa wanasiasa wa Tanzania hawagusiki katika sakata la mradi mchafu wa rada’. Hosea alikata tamaa ya kuwafikisha mahakamani vigogo waliohusika wa mradi wa rada lakini alikuwa na uhakika kwamba, wakuu wa vyombo vya ulinzi nawo walihusika katika kashfa hiyo. Hosea aliongeza kuwa amepokea vitisho kupitia ujumbe wa simu na barua, akitaarifiwa karibu kila siku, kuwa anapambana na watu matajiri na wenye nguvu. Hosea alieleza kuhusu vikao nyeti vya serikali vinavyosheheni ubabe na vitisho; “Unapoingia katika mikutano yao, wanataka ujione kuwa mdogo na wao uwaone kama miungu. Wanataka ufahamu kuwa wao ndio wamekuweka hapo. Usipokubaliana nawo, kuna hatari”.
Hosea alitanabaisha kuwa kama vitisho vitaendela juu yake, atahama nchi. Wakati huo hali ya nchi ya Tanzania ilikuwa tete katika uwanda wa demokrasia na imani ya wananchi kwa serikali yao. Usalama wa Hosea na baadhi ya wanasiasa waliokuwa mbele kutaka wahusika wachukuliwe hatua, ulitegemea zaidi nguvu ya taasisi ya SFO na vyombo vya kisheria vya Uingereza...

#Simulizi_za_wazalendo
Mkuu Return Of Undertaker ya nini kujichosha na mambo yasiyo wezekana kwa sasa? We omba Mungu tuu akupe uhai uishi kuja kushuhudia yajayo baada ya kuondoshwa CCM.
Kesi za jinai hazina ukomo, kesi za hawa wanaolindwa na CCM sasa zitakuwa kama zile za GESTAPO ya Hitler. Watuhumiwa mpaka Leo wanagunduliwa huko walikojificha wengine Argentina, wengine Brazil wakiwa na 80s na 90s.
Hata hawa wasubiri tuu!
 
Akili za panzi hizi kwa hiyo bila kuweka ile list serikali haiwezi kuwashika? Kumbe tunaserikali mfu iliyozidiwa na chadema tuna takukuru wanalipwa pesa ambayo ni kodi ya mtanzania na ndio kazi yao kuchunguza haya mambo
Kwani kuna ubaya gani tukijikumbusha sisi chadema jinsi gani tulifanya kazi ya kufichua mafisadi kazi ya kuwakamata tuiachie serikali!
 
Nyinyi ni mijitu mijinga sana walahi!
Yaani baada ya kukaa na kutafuta maendeleo eti mnakwenda kufufua makaburi, pathetic DNA kwa kweli, hakika hapo mlipo mmvaa kibwebwe cha msutano kwa sababu ndio kazi yenyewe mnayo iweza, pathetics characters walahi!
Endeleeni kuvaa VIBWEBWE NA UMASKINI WENU WA MILELE WALAHI!
MAJITU MAZIMA OVYO KABISA walahi
 
Back
Top Bottom