Makabrasha ya intelijensia tatu muhimu juu ya ujio wa Tundu Lissu yana nini ndani yake?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,632
697,749
Yamebakia masaa machache Tundu Antipasi Lissu, mwanachama kiongozi na mtia nia ya kugombea urais kwa tiketi ya CHADEMA atue nchini akitokea nchi ya Ubelgiji alipokuwa kwa ajili ya matibabu ya muda mrefu.

Ujio wake si wa kawaida kwakuwa inasemwa kuwa wale waliomsababishia madhila ya yote yaliyotokea mpaka sasa hawajakamatwa na hawajajulilana ni akina nani zaidi ya kuwepo tuhuma ambazo ziko pending.

Ujio huu una maandalizi mengi ya wazi na ya siri. Kuna intelijensia zinafanya kazi kubwa sana kwenye huu ujio na ziko intelijensia tatu muhimu; kila moja inajitahidi kucheza karata zake kwa umakini mkubwa. Intelijensia itakayokosea kidogo tu imekula kwake mazima.

1. Intelijensia ya chama chake
Je, imejiandaaje na ujio wake? Usalama wake? Baada ya kuwasili nchini? Na baada ya hapo? Habari za kuwa atawekwa ndani na bila dhamana hadi uchaguzi upite kutokana na kesi kadhaa zinazomsubiri za huko nyuma kabla hajaondoka nchini.

2. Intelijensia ya kwake mwenyewe
Je, amejiaandaje kwa lolote litakalomtokea? Ni wazi haji kiboya ndio maana anajiamini sana. Pengine escort anayokuja nayo ina options nyingi tayari na imeshajiandaa kwa lolote, kuanzia kukamatwa hadi kuwekwa kizuizini; kama ni kweli hili lipo, hapo kuna jumuiya ya kimataifa itahusishwa pakubwa.

3. Intelijensia ya mamlaka za nchi
Je, itafanya nini kwenye huu ujio? Ni kweli wamejiandaa kumkamata? Je, wameshapima athari zake juu ya hili? Na je, itakuwaje kama watapuuza na kumpa ulinzi wote toka airport mpaka kwake na baada ya hapo?

Kati ya intelijensia zote tatu hii ya mamlaka za nchi ndio inaangaliwa kwa karibu mno kwakuwa chochote itakachokifanya kitaonwa na kusikika kimataifa. Hapa ndio panahitajika kuwa na washauri wenye weledi mkubwa na hekima ya kuamua mambo ya kitaifa
Nu vema intelijensia hii ikazishauri mamlaka ziruhusu mapokezi bila fujo na bila kutunishiana misuli, watakuwa wamefanya jambo moja kubwa sana.

Kwenye jamii kuna kundi moja kubwa sana linapenda matukio na amsha amsha, hiyo ndio hobby yao
Likisikia Miss Tanzania anarudi, utalikuta airport
Likisikia SIMBA imeshinda michuano ya kimataifa, litaenda airport
Likisikia tukio lolote kubwa lazima liwepo kushuhudia

Ni nani anakumbuka ile misafara ya Mwalimu Myerere aliporudishwa nchini, msafara wa Lipumba ariporudi nchini Toma kwenye timu ya kurekebisha uchumi wa dunia, msafara wa kumpokea Ruge nk.

Hili kundi lime-miss hayo mambo. Si kila atakayeenda pale airport ni mwana CHADEMA ni kuwaacha wajipe raha wapunguze fukuto za changamoto za maisha ndani yao, a polisi wawepo kuhakikisha ulinzi na usalama wa TAL, waliokuja kumpokea, wasiohusika na mapokezi na mali za watu wote.

Weledi na utendaji kazi wa jeshi la polisi unaangaliwa kwa karibu mno siku hii ya leo ya kurejea kwa TAL.

Jr
 
Atakuwa kasoma kitabu cha Yerico Nyerere, UJASUSI WA KIDOLA, Bora arudi maana mahakama inamtaka kwa kuruka dhamana, ajibu shitaka lake.
 
Kikubwa polisi waache wafuasi wake marafiki zake na ndugu wakampokee mpendwa wao. Polisi ikiingilia kati watafua sura ya nchi kwanza kuna msiba mkubwa wa kitaifa.

Polisi wafanye kazi tu ya kulinda raia wake,isiende kuzuia watu, madam mlengwa anapokelewa keshasema anaenda kumuaga Mkapa haina haja ya kulumbana sana. Pi, wapokeaje ikiwa kutatolewa warning basi watii maagizo ya polisi.
 
Back
Top Bottom