Makabila zaidi ya 128 yanayopatikana Tanzania Bara

Wasimbiti ni kabla kubwa sana analotekea mama Maria nyerere

Ni kabila ambalo linapitikana wilaya ya rorya suba
 
Hii orodha ya makabila ya Tanzania inaweza
kuwa na matatizo kwenye majina kadhaa, kwa
sababu mbalimbali.
Orodha hii inatokana na orodha ya lugha za
Tanzania inayopatikana katika Ethnologue ,
pamoja na tovuti nyingine .
Inawezekana kwamba baadhi ya majina ya
makabila ni majina ya lugha au lahaja tu, badala
ya makabila, na labda majina mengine
yaliandikwa vibaya.
Juu ya hiyo, hakuna ufafanuzi wa wazi kusema
kikundi fulani ni kabila au siyo. Vikundi kadhaa
katika orodha hii vina wenyeji mamia tu, lakini
vikundi vingine vina mamilioni ya watu; labda kila
kikundi kinaitwa "kabila," lakini ni jamii za aina
tofauti kabisa. Vikundi katika ukurasa huu
vimeorodheshwa kuwa vikundi tofauti kutokana
na ushahidi kutoka Ethnologue kutofautisha
lugha zao.
Hii ni orodha ya makabila ya watu ambao
wamekuwa wanaishi tangu zamani katika eneo
ambalo sasa linaitwa Tanzania, pamoja na
makabila yaliyogawiwa na mipaka baina ya
Tanzania na nchi za jirani.
Orodha hii haizingatii makabila yanayoishi katika
Tanzania kama wakimbizi tu, hasa kutokana na
vita katika nchi za jirani. Vilevile ukurasa huu
hauorodheshi vikundi vya wahamiaji kutoka nchi
za kigeni, kama wahamiaji au wazao wao kutoka
Uarabuni au Uhindi.
Waakie
Waakiek
Waalagwa (pia wanaitwa Wasi)
Waarusha
Waassa
Wabarabaig (pia wanaitwa Wamang'ati )
Wabembe
Wabena
Wabende
Wabondei
Wabungu (au Wawungu)
Waburunge
Wachagga
Wadatoga
Wadhaiso
Wadigo
Wadoe
Wafipa
Wagogo
Wagoma
Wagorowa (pia wanaitwa Wafiome )
Wagweno
Waha
Wahadzabe (pia wanaitwa Wahadza na
Watindiga)
Wahangaza
Wahaya
Wahehe
Wahinda
Wahutu
Waikizu
Waikoma
Wairaqw (pia wanaitwa Wambulu )
Waisanzu
Wajaluo
Wajiji
Wajita
Wakabwa
Wakaguru
Wakahe
Wakami
Wakara (pia wanaitwa Waregi )
Wakerewe
Wakimbu
Wakinga
Wakisankasa
Wakisi
Wakonongo
Wakuria
Wakutu
Wakw'adza
Wakwavi
Wakwaya
Wakwere (pia wanaitwa Wanghwele)
Wakwifa
Walambya
Waluguru
Walungu
Wamachinga
Wamagoma
Wamahanji
Wamakonde
Wamakua (au Wamakhuwa )
Wamakwe (pia wanaitwa Wamaraba )
Wamalila
Wamambwe
Wamanda
Wamanyema
Wamasai
Wamatengo
Wamatumbi
Wamaviha
Wambugwe
Wambunga
Wameru
Wamosiro
Wampoto
Wamwera
Wandali
Wandamba
Wandendeule
Wandengereko
Wandonde
Wanena
Wangasa
Wangindo
Wangoni
Wangulu
Wangurimi (au Wangoreme )
Wanilamba (au Wanyiramba)
Wanindi
Wanyakyusa
Wanyambo
Wanyamwanga
Wanyamwezi
Wanyanyembe
Wanyasa
Wanyaturu (pia wanaitwa Warimi )
Wanyiha
Waokiek
Wapangwa
Wapare (pia wanaitwa Wasu )
Wapimbwe
Wapogolo
Warangi (au Walangi)
Warufiji
Warungi
Warungu (au Walungu)
Warungwa
Warwa
Wasafwa
Wasagara
Wasandawe
Wasangu (Tanzania)
Wasegeju
Washambaa
Washirazi
Washubi
Wasizaki
Wasuba
Wasukuma
Wasumbwa
Waswahili
Wataveta
Watemi (pia wanaitwa Wasonjo )
Watongwe
Watumbuka
Wavidunda
Wavinza
Wawanda
Wawanji
Waware (inaaminika lugha yao imekufa)
Wayao
Wazanaki
Wazaramo
Wazigula
Wazinza
Wazyoba

Kabila lako halipo?
 
Wamanda kwao Ludewa, sampo zao ni hawa akina Mtikila(RIP), sina hakika na Kolimba(RIP). Hayo mengine watakwambia wengine.
 
Wamanda kwao Ludewa, sampo zao ni hawa akina Mtikila(RIP), sina hakika na Kolimba(RIP). Hayo mengine watakwambia wengine.
Pia wapo kandokando ya ziwa Nyasa kuna sehemu inaitwa Manda. Mila na tamaduni zinafanana sana na Wangoni, Wamatengo, Wampoto. Wote hao ni kutoka mkoa wa Ruvuma. Ngoma yao kubwa ya asili ni Kihoda/Chihoda kama sijakosea.

Uvuvi, Ugali wa muhogo ndio chakula maarufu pande hizo za ziwa nyasa.

Kwa kiasi fulani wanafanana pia na jirani zetu wa Malawi.

Hayo makabila ya kusini kwa ujumla huwa wanajulikana kama Wangoni ingawa kuna utofaiti ukifuatilia kwa undani. Ni kama ilivyo makabila ya Kilimanjaro wote huitwa wachaga lakini kwa undani kuna wakibosho, wamachame, wauru, waold moshi, wamarangu, warombo nakadharika.

Huo ni ufahamu wangu.
 
Kabila la wasumbwa huwa sijawahi kuwaona shule mpaka chuo nilipomaliza sikuwahi kuwasikia hawa watu wanapenda sana kujificha,vipi humu pia mpo? Njoo tuzungumze kisumbwa jamani nilikulia huko!
 
Mtikila kwao ni kijiji cha Milo,siyo mmanda ni mpangwa!Makabila yaliyokando ya ziwa Nyasa kwa wilaya ya Ludewa ni Wakisi,Wamakonde na Wamanda na nyanda za juu ni Wapangwa!
 
Kuna mengine yanajaza tu hesabu, huku ikiwa ni kabila moja lugha moja lakini wamegawanyika kulingana na mazingira tu. Mfn mwarusha ni mmasai tu yule yule lugha ile ile, tofauti ni mazingira wanamoishi. Wabarbeik na wadatoga nao ni kabila moja tofauti mmoja anakaa kule mwingine kwingine.
 
Back
Top Bottom