Majuu kwawaka moto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majuu kwawaka moto

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Mwiba, Nov 20, 2008.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Nov 20, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kama kuna wakati mtu anakumbuka kwao alikotoka basi kihoro cha hali ya uchumi duniani kinawafanya wakimbizi waanze kukumbuka walikotoka na pengine mambo yakiendelea watatafuta njia za kurudi makwao ,kila siku ziendavyo ndivyo mambu yanavyozidi kukacha na uchumi haukubaliani na population ya nchi za ulimwengu wa kwanza,serikali zimeanza kukata bajeti kila kona ,makampuni nayo yameanza kukata wafanyakazi na mengine yanafilisika ,shuguli za hapa na pale nazo zinazidi kuzorota kiasi cha kuwafanya wakimbizi wakose cha kufanya au kubangaiza jambo ambalo linawakosesha feza ya kuimudu siku.
  Ushauri wa bure watazame nchi walizotoka huenda wakaweza kuyamudu maisha japo nako kunafuka moshi.
   
 2. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #2
  Nov 20, 2008
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Hii hii hii hii!
  Hiyo ni general statement.

  Vipi wakimbizi wenye PhD na Masters zao?
  Vipi wakimbizi wa walimu wa University? University gani imefungwa kwa ukata.

  Ukiwaza neno Wakimbizi usifikirie wale tu wanao fanya kazi Grave hours( yaani wanasubiri watu waende kulala ili wao wapate nafasi ya kufanya kazi).
  Kuna wakimbizi wameenda shule za kutakata kwa shoka hata wenyeji wao hawapati fursa ya kufurukuta mbele yao.

  Ukisikia Tanzania kuna hali ngumu miongoni mwa walalahoi, usiende mbio ukadhani walalahoi wote hali zao ni mbaya.
  Wako waendeshao Baisikeli toka Kimanzichana mpaka Feli kila siku huku wamevaa machurupwete lakini, wanaishi kwenye nyumba zao nuzri tu, wanachakula cha kutosha pia wameweza kulipia ada za level ya University hata za wajukuu zao.

  Hali ya ughaibuni ni mbaya siku zote lakini wapi hali ni nzuri? Tanzania??

  Kila mtu aliye ughaibuni ana jambo lililompeleka huko na siku inakuja jambo litatokea la kumrudisha kule alikotoka.
   
Loading...