Majuto ya P Funk Majani yanatufundisha nini Vijana ambao hatujaoa?

ROBERT HERIEL

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
2,248
2,000
Ni kweli, ni ngumu kumbadilisha mtu.

Kujibadilisha tuu kasheshe

Kuna wakati nilitaka niwe mtu wa mazoeziπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Basi nikaanza mazoezi sikufikisha hata wiki nikashindwa

Au kuna vijitabia mtu unakuwa navyo unahangaika kuviacha wewe binafsi kwa hiyari yako lakini bado unashindwa

Sembuse kumbadilisha mtu mwingine
 

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
57,607
2,000
Ujinga ni sehemu ya kazi ya Mungu aliyoiacha kwa viumbe wake, wanahiyari ya kuchagua ujinga au werevu
Sehemu ya kazi ya Mungu ni ujinga? Kwa nini Mungu afanye kazi yake iwe ujinga?

Kwa nini hakufanya kazi iliyojaa werevu wa kutukuka bila hata harufu ya ujinga?
 

Sisyphus

JF-Expert Member
Oct 8, 2015
2,096
2,000
Sema mwandishi umetufunga kamba eti mtoto wa kike anachukua tabia za mama yake asilimia 90 ...
 

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
14,775
2,000
Ni unconscious behaviour huwezi jua ila unaogopa wanawake wazuri ji-google vizuri type ya madem zako utaona jinsi usivyojiamini
Kama wewe unaona kuwa mimi sijiamini basi sawa ila ninaomba kurudia tena na tena kuwa SIPENDI DHARAU ZA MTOTO WA KIKE.
 

ngorokolo

Senior Member
Mar 3, 2021
132
250
Ninachoamini P funk anamchango wa kutosha kumuharibu huyo mtoto ukiangalia life style yao wakiwa pamoja huko nyuma
 

Fohadi

JF-Expert Member
Jul 24, 2020
591
1,000
MAJUTO YA PFUNK MAJANI YANATOA FUNZO GANI KWA VIJANA AMBAO HAWAJAOA?

Na, Robert Heriel

Jana nilipata bahati ya kusikiliza mahojiano ya Clouds na P Funk Majani yaliyofanyika kwa njia ya simu. Nimeona niandike kidogo kwa lengo la wengine kujifunza kupitia kinachoendelea mitandaoni kwenye tasnia ya Burudani

Kaka Mkubwa Majani kwa maelezo yake amekiri dhahiri Shahiri kuwa alikosea njia kumchagua Kajala kama Mwenza na Mama wa watoto wake.

Majuto ya PFunk majani yanaenda mbali zaidi kuonyesha athari azipatazo yeye binafsi na familia yake kutokana na mienendo ya Kajala aliyekuwa mwenza wake hapo kale.

Si hivyo tuu, PFunk anaeleza namna matukio ya Kajala yanavyoathiri watoto wake huko shuleni na jamii kwa ujumla.

Kupitia mkasa huu lazima tupate cha kujifunza ili kuijenga jamii iliyobora

Wahenga walisema; Uzuri wa Mwanamke sio urembo au umbo Bali ni Tabia; hicho ndicho kinajitokeza katika mkasa huu.

Vijana wa sasa lazima tujichunge, tusidanganywe na tamaa ya macho tuwaonapo wanawake wazuri huku Tabia zao zikiwa chafu. Ni Hatari kwa ustawi wa ndoa na ukuaji wa familia katika jamii yetu na taifa kwa ujumla.

Unapooa mwanamke mzuri lakini anatabia mbovu sio kwamba atakuathiri wewe pekeako bali ataharibu jina la ukoo wenu, watoto wako na jamii kwa ujumla.

Kila siku naeleza humu, mwana wa nyoka huwa ni nyoka siku zote. Mtoto wa kike hurithi Tabia za Mama yake kwa 90% halikadhalika mtoto wa kiume hurithi Tabia ya Baba yake kwa 90%

Hivyo utakapo kuoa mtoto wa kike nenda kachunguze Historia ya Mama yake, hata kama Amekufa historia ni muhimu. Halikadhalika na kwa wanawake kama unataka kuolewa nenda chunguza Tabia ya Baba Mkwe.

90% hufuata mkondo wa wazazi wao kutokana na kurithi Tabia na mfumo. 10% ni wale Exceptional ambao wanakuwa tofauti kabisa na wazazi wao. Hawa 10% ni wachache sana hivyo usiwape Guarantee.

Kama Mama alikuwa Malaya ni rahisi watoto wake wa kike kuwa Malaya

Malaya Huzaa Malaya

Ukoo Malaya huzaa kizazi Malaya

Halikadhalika na sifa zingine kama uchoyo, uvivu, wizi, uchawi na ushirikina, ufupi, urefu, weupe, Weusi n.k.

Usihadaiwe na Makalio makubwa ya mwanamke, usichanganyikiwe na sura nzuri au rangi nzuri. Angalia historia ya Tabia ya ukoo unaoenda kuolewa au kuoa

Upo uwezekano mkubwa kabisa kama umeoa kwa Mama aliyeachana na Mume wake(Baba mkwe) kuna uwezekano Na wewe ukaachana na Huyo mwanamke uliyenaye sasa.

Nimefanya uchunguzi katika hili, na majibu yameonyesha hivyo kuwa wengi tulivyo ni tunapitia kule kule walikopitia wazazi wetu.

Kasoro hao 10% ambao ni Exceptional.

Ni ngumu kudumu kwenye ndoa ikiwa wakwe wako walishindwa kudumu kwenye ndoa zao. Ni ngumu lakini inawezekana.

Nilishawahi kushuhudia kisa cha Mama mmoja jijini Dar es salaam akiwakuwadia watoto wake kwa mabwana wenye pesa. Huyo Mama mwenyewe sio lelemama ni wamoto hata ukimtazama kwa macho tuu.

Vijana unaweza ukapuuzia vitimbwi vya Mwenza wako baada ya kuachana lakini ni ngumu kupuuza vitimbwi vya watoto wako walioaharibiwa na mwenzi wako. Kwani hao wamebeba jina lako na damu yako.

Inauma sana kusikia sifa mbaya kutoka kwa watoto wako alafu ukijaribu kuonya na kukemea kama Baba, Mama mtu anamkingia kifua mtoto. Automatic mtoto ataungana na Mama Na wewe utashindwa in anyways

Angalia Makalio yasije yakakuponza huko mbeleni

Angalia sura na rangi visije vikakupa magonjwa ya moyo

Angalia sauti na umbo visije vikakubomoa.

Umalaya upo damuni wala mtu hajifunzi ndio maana malaya Hawaoni aibu kufanya kwani hawana wa kumhofia iwe ni mzazi wake au nani. Kwani wanajua kuwa wao wapo hivyo sema jamii ndio Haujui tuu.

Umalaya ni kama wizi, uchawi, ulevi, uvivu, ujambazi, n.k

Mtu hajifunzi bali anazaliwa nao.

Kwa waliosoma Psychology mtaungana na mimi hasa waliosoma Psychoanalysis. Mtu habadiliki bali anachofanya ndivyo alivyo

Waliosoma ID, EGo na Super EGo watakubaliana na mimi kuwa zipo Tabia za ndani kabisa ambazo mtu huwa nazo Tabia hizi hukaa kwenye ID. Mtu anapokatazwa jambo Fulani akiwa mtoto basi Tabia hiyo haifi isipokuwa inajificha kwenye ung’ amuzi bwete na siku akikua akapata uhuru Tabia hiyo hujitokeza

Ndio maana watu wapatapo hela ndio Tabia zao za ndani kabisa hudhihirika, au walikipata mamlaka au cheo. Wengi husema Fulani kabadilika kumbe hiyo ndio ilikuwa tabia yake tangu zamani akiwa ananyonya kwa mama yake.

Zamani kwa kulikua hili, ndio maana wazee walikuwa wanakuambia usioe ukoo ule au familia ile kwa mambo kama hayo.

Sasa Vijana wa siku hizi kwa kujifanya wajuaji tunawakatalia wazee na kuwaambia Huyu niliyenaye hana Tabia hizo; kumbe kaficha makucha yake siku ukija kugundua umeumia.

Zingatia Mbuzi hawezi zaa simba

Nyoka hawezi zaa Jongoo

Kuku hawezi Totoa Bata

Watu husema sijui Ukiomba Mungu sijui Yesu atabadilika, thubutu hakuna kubadilika kwa mambo kama hayo. Wengi hurudisha makucha umri ukiwa umechaenda na hawana jipya sasa huko sio kubadilika bali ile Tabia ya Asili imejihifadhi ndani ya ID kama zamani.

Mtu ashakuwa Mzee anaona hana ujanja wala jipya zaidi ya kurudisha makucha ndani kama awali.

Ndio maana Yesu alisema usifungwe Nida na wasioamini.

Mungu aliwaambia Waisrael wasizaliane na wamataifa kwani lazima mambo yataharibika.

Sasa wewe Oa Malaya alafu jipe kazi ya kuomba uone kama Hautaomba maisha yako yote. Utamuombea Mume/mke mhuni weee! Hatabadilika mpaka umri utakapomtupa mkono ndio atarejesha makucha yake ndani, hapo utakuwa hoi utasema walau sasa Kaacha Tabia mbaya lakini kabla hujapumzika unashangaa watoto nao hao wanafungua makucha yao. Utaanza tena kuomba kama Boya hivi mpaka unaingia kuzimu

Kumbe ungeolewa/kuoa Mwenza mwenye Tabia njema usingehangaika na Maombi ya wapuuzi. Ati atabadilika πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Kama huwezi muombea mtu mfupi awe mrefu au mweupe awe mweusi ndivyo usivyoweza kuombea Tabia za asili. Maumbile ya Tabia Yapo ya asili ambayo hukaa ndani kabisa ya mtu ID, achana na haya ya kuiga ya EGo na Super EGo

Yesu alisema, watu Hawavuni Tini kwenye Zabibu.

Ndio maana hata kwenye kuomba kazi lazima CV yako izingatiwe.

Robert Heriel

Taikon wa Fasihi

0693322300

Kwa sasa Mikese, Morogoro
Uko sahihi lakini kwa namna moja ama nyingine huna tofauti na motivational speakers ambao wanahimiza watu kujiajiri bila kuwapa njia za kujiajiri..

ilipaswa uje na mechanisms unazotumia kuwachunguza wakwe zako kabla hujaanzisha uhusiano na mwenza wako. Weka procedures hapa kuwa 1 2 3 au kama mkwe ametangulia mbele ya haki ukitaka kumchunguza nenda kaburini kwake fanya 123...

kwenye biashara wanasema idea ya biashara nzuri lazima iwe SMART...specific, measurable..Achievable...Realistic...Timely...

Je hoja yako ni SMART?, If YES, what are the procedures..tiririka mkuu acha fasihi kwenye mahusiano.
 

sheby dunia

Member
Jul 12, 2018
32
95
Kitini kimeeleweka! Ila too late!

Nyege nazo zinatiaga upofu! Nyege zikikolea hayo majuto huja baadaye!!

Cha msingi nikuomba Mungu! Lakini kwa akili zetu Hatuwezi tunadanganyana!
Daaaaah hili swala LA kitini au pamphlet linankumbusha mbali enz izo nko olevel bas ukiwa na vitin vitatu tyuu unaonekana mpenda shule
 

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
57,607
2,000
Ujinga ni sehemu ya kazi ya Mungu aliyoiacha kwa viumbe wake, wanahiyari ya kuchagua ujinga au werevu
Mkuu, unaruhusiwa kuamini unachotaka, kama sehemu ya haki yako ya kiutu na ya kuabudu.

Na mimi nitaitetea haki yako hii.

Lakini, kimantiki, kuamini Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, anayeumba ulimwengu unaoweza kuwa na ujinga, nao ni ujinga.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom