Majuto ya P Funk Majani yanatufundisha nini Vijana ambao hatujaoa?

mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
56,293
2,000

Sasa tunafanyaje kama wajomba zake Paula
Mkuu mtoto unavyomlea ndivyo anavyokuwa
Mtoto ataiga eidha tabia za mama au baba
Ila inavyonekana mtoto huyu alikaa sana na mama na maisha ya mama kama unavyojua tena!
Na kwa mama aina hii wao wakiwa na binti wakimuona mrembo na wanaume wanamvizia au kumtaka wamama kama hawa wanaona kama ufahari,kikubwa aone mtoto wake anapata pesa,kapewa gari,mavazi,bata basi
Binafsi mm nawajua wamama wa aina hii ya mjinimjini kama 50 akili zao wanazijua wenyewe,hawaangali mbali wao wanangalia karibu

Ova
 
ROBERT HERIEL

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
2,788

Hatari sana mkuu
 
Scars

JF-Expert Member
Apr 8, 2017
17,582
2,000
kutoka kwa dizasta

A ngalia rafiki zangu, kisha ringanisha na rafiki zako hasa ambao wanamzungukka binti yangu.../

Hua nawaza wanachomfundisha ni nini, zaidi ya umbea kunywa pombe na kupiga vimini.../

Mama hao rafiki zako washaoza, hakuna mwenye afahali hata mmoja.../

Wanapenda sana maisha ghali, nilikupa taadhari ukae mbali hukukubali.../

Yule mrefu alishawahi kunitongoza anajua nimekuoa nimefunga mageti yangu, nisingemkubali hata angenikuta enzi zangu.../

Ananishika kila akinikuta peke yangu, anasema umemwambia kuhusu ukubwa wa nyeti zangu../

Aasa ndo nini?
 
Kuna Rais mmoja wa Marekani, anaweza kuwa ni Lincoln, alipata kusema kwamba, "If you want to test a man's character, just give him power"

Ipo hivyo

Ndio maana dhambi zote ni sawa au wema wowote ni sawa kwani watu hufanya kwa nafasi walizonazo ila ID/ nafsi zao zinafanana ila uwezo wa kicheo, kimamlaka, kiuchumi ndio tofauti
 
kichwa kikubwa

JF-Expert Member
Sep 24, 2013
2,200
2,000
Maisha ya Instagram. Mwanamke kamwe hawezi kuwa na busara. Ni wachache sana. Tena sana. 0.1% kati ya mia. Huyo sijui Kajala she's just a whore or a ho. Aina yake ni hatari katika jamii na wametungiwa mashairi na kila multiplatinum selling rapper kule Marekani.
Stunt
 
ROBERT HERIEL

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
2,788
2,000
kutoka kwa dizasta

A ngalia rafiki zangu, kisha ringanisha na rafiki zako hasa ambao wanamzungukka binti yangu.../

Hua nawaza wanachomfundisha ni nini, zaidi ya umbea kunywa pombe na kupiga vimini.../

Mama hao rafiki zako washaoza, hakuna mwenye afahali hata mmoja.../

Wanapenda sana maisha ghali, nilikupa taadhari ukae mbali hukukubali.../

Yule mrefu alishawahi kunitongoza anajua nimekuoa nimefunga mageti yangu, nisingemkubali hata angenikuta enzi zangu.../

Ananishika kila akinikuta peke yangu, anasema umemwambia kuhusu ukubwa wa nyeti zangu../

Aasa ndo nini?

Hizi Stanza sikuwahi kuzisikia Mkuu
 
fimboyaasali

JF-Expert Member
Jan 14, 2011
3,803
2,000
MAJUTO YA PFUNK MAJANI YANATOA FUNZO GANI KWA VIJANA AMBAO HAWAJAOA?

Na, Robert Heriel

Jana nilipata bahati ya kusikiliza mahojiano ya Clouds na PFunk Majani yaliyofanyika kwa njia ya simu. Nimeona niandike kidogo kwa lengo la wengine kujifunza kupitia kinachoendelea mitandaoni kwenye tasnia ya Burudani

Kaka Mkubwa Majani kwa maelezo yake amekiri dhahiri Shahiri kuwa alikosea njia kumchagua Kajala kama Mwenza na Mama wa watoto wake.

Majuto ya PFunk majani yanaenda mbali zaidi kuonyesha athari azipatazo yeye binafsi na familia yake kutokana na mienendo ya Kajala aliyekuwa mwenza wake hapo kale.

Si hivyo tuu, PFunk anaeleza namna matukio ya Kajala yanavyoathiri watoto wake huko shuleni na jamii kwa ujumla.

Kupitia mkasa huu lazima tupate cha kujifunza ili kuijenga jamii iliyobora

Wahenga walisema; Uzuri wa Mwanamke sio urembo au umbo Bali ni Tabia; hicho ndicho kinajitokeza katika mkasa huu.

Vijana wa sasa lazima tujichunge, tusidanganywe na tamaa ya macho tuwaonapo wanawake wazuri huku Tabia zao zikiwa chafu. Ni Hatari kwa ustawi wa ndoa na ukuaji wa familia katika jamii yetu na taifa kwa ujumla.

Unapooa mwanamke mzuri lakini anatabia mbovu sio kwamba atakuathiri wewe pekeako bali ataharibu jina la ukoo wenu, watoto wako na jamii kwa ujumla.

Kila siku naeleza humu, mwana wa nyoka huwa ni nyoka siku zote. Mtoto wa kike hurithi Tabia za Mama yake kwa 90% halikadhalika mtoto wa kiume hurithi Tabia ya Baba yake kwa 90%

Hivyo utakapo kuoa mtoto wa kike nenda kachunguze Historia ya Mama yake, hata kama Amekufa historia ni muhimu. Halikadhalika na kwa wanawake kama unataka kuolewa nenda chunguza Tabia ya Baba Mkwe.

90% hufuata mkondo wa wazazi wao kutokana na kurithi Tabia na mfumo. 10% ni wale Exceptional ambao wanakuwa tofauti kabisa na wazazi wao. Hawa 10% ni wachache sana hivyo usiwape Guarantee.

Kama Mama alikuwa Malaya ni rahisi watoto wake wa kike kuwa Malaya

Malaya Huzaa Malaya

Ukoo Malaya huzaa kizazi Malaya

Halikadhalika na sifa zingine kama uchoyo, uvivu, wizi, uchawi na ushirikina, ufupi, urefu, weupe, Weusi n.k.

Usihadaiwe na Makalio makubwa ya mwanamke, usichanganyikiwe na sura nzuri aj rangi nzuri. Angalia historia ya Tabia ya ukoo unaoenda kuolewa au kuoa

Upo uwezekano mkubwa kabisa kama umeoa kwa Mama aliyeachana na Mume wake(Baba mkwe) kuna uwezekano Na wewe ukaachana na Huyo mwanamke uliyenaye sasa.

Nimefanya uchunguzi katika hili, na majibu yameonyesha hivyo kuwa wengi tulivyo ni tunapitia kule kule walikopitia wazazi wetu.

Kasoro hao 10% ambao ni Exceptional.

Ni ngumu kudumu kwenye ndoa ikiwa wakwe wako walishindwa kudumu kwenye ndoa zao. Ni ngumu lakini inawezekana.

Nilishawahi kushuhudia kisa cha Mama mmoja jijini Dar es salaam akiwakuwadia watoto wake kwa mabwana wenye pesa. Huyo Mama mwenyewe sio lelemama ni wamoto hata ukimtazama kwa macho tuu.

Vijana unaweza ukapuuzia vitimbwi vya Mwenza wako baada ya kuachana lakini ni ngumu kupuuza vitimbwi vya watoto wako walioaharibiwa na mwenzi wako. Kwani hao wamebeba jina lako na damu yako.

Inauma sana kusikia sifa mbaya kutoka kwa watoto wako alafu ukijaribu kuonya na kukemea kama Baba, Mama mtu anamkingia kifua mtoto. Automatic mtoto ataungana na Mama Na wewe utashindwa in anyways

Angalia Makalio yasije yakakuponza huko mbeleni

Angalia sura na rangi visije vikakupa magonjwa ya moyo

Angalia sauti na umbo visije vikakubomoa.

Umalaya upo damuni wala mtu hajifunzi ndio maana malaya Hawaoni aibu kufanya kwani hawana wa kumhofia iwe ni mzazi wake au nani. Kwani wanajua kuwa wao wapo hivyo sema jamii ndio Haujui tuu.

Umalaya ni kama wizi, uchawi, ulevi, uvivu, ujambazi, n.k

Mtu hajifunzi bali anazaliwa nao.

Kwa waliosoma Psychology mtaungana na mimi hasa waliosoma Psychoanalysis. Mtu habadiliki bali anachofanya ndivyo alivyo

Waliosoma ID, EGo na Super EGo watakubaliana na mimi kuwa zipo Tabia za ndani kabisa ambazo mtu huwa nazo Tabia hizi hukaa kwenye ID. Mtu anapokatazwa jambo Fulani akiwa mtoto basi Tabia hiyo haifi isipokuwa inajificha kwenye ung’ amuzi bwete na siku akikua akapata uhuru Tabia hiyo hujitokeza

Ndio maana watu wapatapo hela ndio Tabia zao za ndani kabisa hudhihirika, au walikipata mamlaka au cheo. Wengi husema Fulani kabadilika kumbe hiyo ndio ilikuwa tabia yake tangu zamani akiwa ananyonya kwa mama yake.

Zamani kwa kulikua hili, ndio maana wazee walikuwa wanakuambia usioe ukoo ule au familia ile kwa mambo kama hayo.

Sasa Vijana wa siku hizi kwa kujifanya wajuaji tunawakatalia wazee na kuwaambia Huyu niliyenaye hana Tabia hizo; kumbe kaficha makucha yake siku ukija kugundua umeumia.

Zingatia Mbuzi hawezi zaa simba

Nyoka hawezi zaa Jongoo

Kuku hawezi Totoa Bata

Watu husema sijui Ukiomba Mungu sijui Yesu atabadilika, thubutu hakuna kubadilika kwa mambo kama hayo. Wengi hurudisha makucha umri ukiwa umechaenda na hawana jipya sasa huko sio kubadilika bali ile Tabia ya Asili imejihifadhi ndani ya ID kama zamani.

Mtu ashakuwa Mzee anaona hana ujanja wala jipya zaidi ya kurudisha makucha ndani kama awali.

Ndio maana Yesu alisema usifungwe Nida na wasioamini.

Mungu aliwaambia Waisrael wasizaliane na wamataifa kwani lazima mambo yataharibika.

Sasa wewe Oa Malaya alafu jipe kazi ya kuomba uone kama Hautaomba maisha yako yote. Utamuombea Mume/mke mhuni weee! Hatabadilika mpaka umri utakapomtupa mkono ndio atarejesha makucha yake ndani, hapo utakuwa hoi utasema walau sasa Kaacha Tabia mbaya lakini kabla hujapumzika unashangaa watoto nao hao wanafungua makucha yao. Utaanza tena kuomba kama Boya hivi mpaka unaingia kuzimu

Kumbe ungeolewa/kuoa Mwenza mwenye Tabia njema usingehangaika na Maombi ya wapuuzi. Ati atabadilika

Kama huwezi muombea mtu mfupi awe mrefu au mweupe awe mweusi ndivyo usivyoweza kuombea Tabia za asili. Maumbile ya Tabia Yapo ya asili ambayo hukaa ndani kabisa ya mtu ID, achana na haya ya kuiga ya EGo na Super EGo

Yesu alisema, watu Hawavuni Tini kwenye Zabibu.

Ndio maana hata kwenye kuomba kazi lazima CV yako izingatiwe.

Robert Heriel

Taikon wa Fasihi

0693322300

Kwa sasa Mikese, Morogoro
Ni ujinga wa pfunk majani mwenyewe,na wala asilaumu mtu
 
Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
14,963
2,000
Waliosoma ID, EGo na Super EGo watakubaliana na mimi kuwa zipo Tabia za ndani kabisa ambazo mtu huwa nazo Tabia hizi hukaa kwenye ID. Mtu anapokatazwa jambo Fulani akiwa mtoto basi Tabia hiyo haifi isipokuwa inajificha kwenye ung’ amuzi bwete na siku akikua akapata uhuru Tabia hiyo hujitokeza
Mkuu, basi ndio maana baadhi ya taasisi nyeti huangali tabia za watu miaka hata 10 nyuma kabla ya kumpa ajira.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom